Mbunge Juliana Masaburi Aahidi Makubwa kwa Vijana UVCCM Tarime Kiuchumi

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

MBUNGE JULIANA MASABURI ACHANGIA UJENZI NYUMBA YA KATIBU UVCCM TARIME, AAHIDI MAKUBWA KWA VIJANA KIUCHUMI​

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi tarehe 14 Julai, 2023 ameambatana na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mara Ndugu Wambura P. Igembya pamoja na viongozi waandamizi wa UVCCM Mkoa wa Mara na kufanya ziara katika Wilaya ya Tarime na kukutana na Baraza la Vijana.

Changamoto ambazo Vijana wamemueleza Mbunge huyo wa Vijana ni pamoja na kukosa Mradi wa kuwajumuisha kwa pamoja; Ukosefu wa Vifaa vya Ofisi kama kompyuta na Mashine ya kuchapisha (Photocopy Machine); Ukosefu wa Nyumba ya Mtumishi na Ukosefu wa Sare za Vijana wa Itifaki na changamoto zingine za kijamii

Mhe. Juliana Didas Masaburi ameahidi kuendelea kushirikiana na vijana wa UVCCM Tarime ili kutatua changamoto kwa vijana ambapo kwa kuanzia amewapatia vifaa vya Ofisi ambavyo ni Kompyuta, Mashine ya kuchapisha (Computer 🖥, Photocopy Machines and Printer 🖨.

Aidha, Mhe. Juliana Masaburi ametoa tofali 1,000 kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi; Mashine ya Kufyatulia Matofali kama mradi jumuhishi kwa vijana; Viatu pea 30 kwa ajili ya Vijana wa Itifaki na mbali na hayo ameahidi kuendelea kushirikiana na vijana wote ili Kujikwamua kiuchumi.

Lakini pia Mhe. Juliana Masaburi amezidi kuwaasa vijana kuendelea kuwa na nidhamu, wakipende Chama Cha Mapinduzi kwa Kazi kubwa sana inayofanywa na Serikali inayosimamiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

"KAZI NA MAENDELEO"

Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge wa Vijana Taifa
Mhe. Juliana Didas Masaburi
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.46.57.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.46.57.jpeg
    147.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.46.54.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.46.54.jpeg
    155.1 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.46.25.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.46.25.jpeg
    86.5 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.46.32(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.46.32(1).jpeg
    89.9 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.45.46.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.45.46.jpeg
    105.5 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.45.26.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.45.26.jpeg
    91.5 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.45.27.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.45.27.jpeg
    115.3 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.45.37.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-15 at 13.45.37.jpeg
    167.3 KB · Views: 5

MBUNGE JULIANA MASABURI ACHANGIA UJENZI NYUMBA YA KATIBU UVCCM TARIME, AAHIDI MAKUBWA KWA VIJANA KIUCHUMI​

Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Juliana Didas Masaburi tarehe 14 Julai, 2023 ameambatana na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mara Ndugu Wambura P. Igembya pamoja na viongozi waandamizi wa UVCCM Mkoa wa Mara na kufanya ziara katika Wilaya ya Tarime na kukutana na Baraza la Vijana.

Changamoto ambazo Vijana wamemueleza Mbunge huyo wa Vijana ni pamoja na kukosa Mradi wa kuwajumuisha kwa pamoja; Ukosefu wa Vifaa vya Ofisi kama kompyuta na Mashine ya kuchapisha (Photocopy Machine); Ukosefu wa Nyumba ya Mtumishi na Ukosefu wa Sare za Vijana wa Itifaki na changamoto zingine za kijamii

Mhe. Juliana Didas Masaburi ameahidi kuendelea kushirikiana na vijana wa UVCCM Tarime ili kutatua changamoto kwa vijana ambapo kwa kuanzia amewapatia vifaa vya Ofisi ambavyo ni Kompyuta, Mashine ya kuchapisha (Computer , Photocopy Machines and Printer .

Aidha, Mhe. Juliana Masaburi ametoa tofali 1,000 kwa ajili ya ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi; Mashine ya Kufyatulia Matofali kama mradi jumuhishi kwa vijana; Viatu pea 30 kwa ajili ya Vijana wa Itifaki na mbali na hayo ameahidi kuendelea kushirikiana na vijana wote ili Kujikwamua kiuchumi.

Lakini pia Mhe. Juliana Masaburi amezidi kuwaasa vijana kuendelea kuwa na nidhamu, wakipende Chama Cha Mapinduzi kwa Kazi kubwa sana inayofanywa na Serikali inayosimamiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)

"KAZI NA MAENDELEO"

Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge wa Vijana Taifa
Mhe. Juliana Didas Masaburi
Hizo computer zinatoa vipi ajira kwa vijana? Ni.za ku bun CD? au kuchezesha Game?
Amesema.chochote kule North Mara wanao chukua Dhahabu huku raia wakibakia masikini?
 
Back
Top Bottom