Mbunge huyu anatafuta nini?

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,217
712
Ni juma la pili sasa Mbunge wa viti Maalum kutoka Mbeya Dr.Mary Mwanjelwa akijaribu kutafuta "Media Attention"toka kwenye Runinga,Magazeti na sasa kwenye blogs juu ya michango anayotoa kwa jamii mara yupo Hospitali akitoa magodoro mara sijui anasalimiana na nani,mara anatembelea wafungwa hivi nini hasa anataka kutuonyesha kuwa yeye anajali sana jamii au anampango wa kujizolea umaarufu wa kisiasa ili aonekane anafaa kwa cheo fulani!Yatosha tu kujitolea kimya kimya sio mpaka uwe na misururu merefu pamoja na waandishi wa habari kila upitapo hebu tumia elimu yako vizuri na sio kujitafutia umaarufu kwa njia hii
 
SOBY

JF-Expert Member
Sep 19, 2011
1,268
456
Amefanya hivyo vitu?..... kama amefanya, don't worry about it.
 
Duble Chris

JF-Expert Member
May 28, 2011
3,482
564
anampango wa kugombea ubunge kutipia ccm hajui kuwa MWAN'GONDA bado ana nguvu ktk jimbo la Mbeya ndani ya CCM
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,434
Ni juma la pili sasa Mbunge wa viti Maalum kutoka Mbeya Dr.Mary Mwanjelwa akijaribu kutafuta "Media Attention"toka kwenye Runinga,Magazeti na sasa kwenye blogs juu ya michango anayotoa kwa jamii mara yupo Hospitali akitoa magodoro mara sijui anasalimiana na nani,mara anatembelea wafungwa hivi nini hasa anataka kutuonyesha kuwa yeye anajali sana jamii au anampango wa kujizolea umaarufu wa kisiasa ili aonekane anafaa kwa cheo fulani!Yatosha tu kujitolea kimya kimya sio mpaka uwe na misururu merefu pamoja na waandishi wa habari kila upitapo hebu tumia elimu yako vizuri na sio kujitafutia umaarufu kwa njia hii
Simlaumu siasa ndivyo zilivyo ili ukubalike katika jamii(kisiasa) lazima kitu kizuri unachokifanya kiwe publicized kwa watu, mimi naweza nikatoa msaada nikawa kimya nikiamini Mungu anaona mema niyafanyayo lakini mwana siasa anataka watu wajue mema ayafanyayo, hebu jaribu kufikiria, Dr Slaa angepambana na mafisadi kimya kimya yaani angekuwa anapeleka malalamiko yake polisi kimya kimya leo hii mimi na wewe tungemfahamu kwamba ni mtu muhimu?
 
rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,895
3,391
anajenga umaarufu iwe rahisi kumtoa sugu 2015,magamba wana idea za kizamani sana
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,510
2,400
Simlaumu siasa ndivyo zilivyo ili ukubalike katika jamii(kisiasa) lazima kitu kizuri unachokifanya kiwe publicized kwa watu, mimi naweza nikatoa msaada nikawa kimya nikiamini Mungu anaona mema niyafanyayo lakini mwana siasa anataka watu wajue mema ayafanyayo, hebu jaribu kufikiria, Dr Slaa angepambana na mafisadi kimya kimya yaani angekuwa anapeleka malalamiko yake polisi kimya kimya leo hii mimi na wewe tungemfahamu kwamba ni mtu muhimu?
Sio yeye tu. Lowassa, Maghufuli, Makamba Yusuph, JK, Kova,......, wote hawa hawana raha ya kuhutubia, kufanyakazi kama jamaa wa luninga hawako mbele yao. Yupo pia Zitto ambaye juzi aliandika magazeti mengi, akatembelea vituo vya redio vingi kuzungumzia ajali ya meli kule Zanzibar na jinsi TBC1 ilivyolishughulikia suala hili. Sasa hivi ni sema UONEKANE, USIKIKE na USOMEKE ati.
 
OTIS

JF-Expert Member
Sep 7, 2011
2,244
806
Sijaona tatizo hapo.
Labda useme hupendi anavyotoa misaada.
Ulitaka taarifa zake zisipewe nafasi kwenye media na apewe nani.
OTIS
 
mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
619
Ni juma la pili sasa Mbunge wa viti Maalum kutoka Mbeya Dr.Mary Mwanjelwa akijaribu kutafuta "Media Attention"toka kwenye Runinga,Magazeti na sasa kwenye blogs juu ya michango anayotoa kwa jamii mara yupo Hospitali akitoa magodoro mara sijui anasalimiana na nani,mara anatembelea wafungwa hivi nini hasa anataka kutuonyesha kuwa yeye anajali sana jamii au anampango wa kujizolea umaarufu wa kisiasa ili aonekane anafaa kwa cheo fulani!Yatosha tu kujitolea kimya kimya sio mpaka uwe na misururu merefu pamoja na waandishi wa habari kila upitapo hebu tumia elimu yako vizuri na sio kujitafutia umaarufu kwa njia hii
Huyo ndiyo mgombea wa ccm mwaka 2015 jimbo la mbeye mjini.....haya unayoyaona ni maandalizi tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom