Mbunge David Mathayo agawa magari ya wagonjwa kwa kila kata jimboni kwake

Mbunge wa Same Magharibi Mh David Mathayo amekabidhi magari ya wagonjwa kwa kila kata katika jimbo lake.

Mathayo amesema magaru hayo imara sana ameyanunua yeye mwenyewe ili kuwasaidia wapiga kura wake na hasa akina mama ukizingatia Same ni eneo lenye milima.

Source: Upendo TV

Maendeleo hayana vyama!
Ndo katoa vile virikuu?
 
Anaacha kujenga viwanda watu wapate ajira ili wajitibu wenyewe, anatoa magari ya wagonjwa kana kwamba wakazi wote wa huko kwake ni wagonjwa!
Daah! Waswahili bana mwingine alitoa magari ya kubebea maiti watu wakaanzaa oooh anaacha kutoa gari ya wagonjwa anatoa ya maiti haya huyu nae anajitolea gari la wagojwa mmekuja na jingine.
 
Mathayo huwa hafanyi chochote jimboni mpaka karibu na uchaguzi ambapo hupitapita na kuwahonga wajumbe. hayo magari ya wagonjwa ilikuwa ayagawe karibu ni kipindi cha kampeni za uchaguzi lakini takukuru wakayazuia. majimbo ya same magharibi na same mashariki yana changamoto kubwa za miundombinu na huduma za kijamii ukilinganisha na majimbo mengine ya mkoa wa kilimanjaro.

pia wilaya ya same ndiyo kubwa kuliko wilaya zote katika mkoa wa kilimanjaro, lakini ukiangalia hali ya maendeleo yako nyuma. jimbo la same mashariki linazalisha mazao mengi ikiwemo mpunga,mahindi, na tangawizi, lakini miundombinu ya barabara ni mibaya sana. ukiacha barabara za milimani, kuna barabara kuu ya mkomazi--kihurio--ndungu--gonja--kisiwani--same ambayo imekuwa ni kilio cha wananchi wa same toka nchi hii ipate uhuru.

la mwisho ni suala la ELIMU. wilaya ya same imekuwa ikishika mkia ktk matokeo ya mitihani yote ya kitaifa katika mkoa wa kilimanjaro. tatizo hili viongozi wanalifahamu lakini hawajishughulishi nalo. same ina matatizo mengi, lakini hili la elimu naamini lisiposhughulikiwa kwa haraka litakuwa na madhara makubwa kwa wilaya yetu kwasababu ardhi ya kilimo inazidi kupungua wakati idadi ya watu inaongezeka.

1614961751151.png
 
Anaacha kujenga viwanda watu wapate ajira ili wajitibu wenyewe, anatoa magari ya wagonjwa kana kwamba wakazi wote wa huko kwake ni wagonjwa!
Kwahili mkuu (umeghafirika)......bila shaka utakuwa umezaliwa na kukulia hapo ilala boma.......kama yataenda kutumika vizuri yatasaidia wengi sana katika hayo maeneo......kuna vitu tupongeze mtu anapofanya jambo kwa maslahi ya jamii
 
Kumbe binadamu ni kazi kuwaridhisha,kuwapa watu magari ili ikitokea mtu kazidiwa awahishwe kwenye matibabu kumbe ni zambi?
Mbona 2015 hadi 2020 wakikuwa wanakamatwa wakitoa hiyo misaada??
 
Asante kwa kumbukizi, nilishikwa na mshangao ni lini wabunge wa ccm wameanza kuwa na huruma na wananchi?

Kumbe ilikuwa ni rushwa ya kuwalaghai wanaccm ili ashinde kura za maoni.

Long live JF.
 
Kwahili mkuu (umeghafirika)......bila shaka utakuwa umezaliwa na kukulia hapo ilala boma.......kama yataenda kutumika vizuri yatasaidia wengi sana katika hayo maeneo......kuna vitu tupongeze mtu anapofanya jambo kwa maslahi ya jamii

Sijawahi kupongeza jizi lolote la kura, na sintokaa.
 
Unaweza kuorodhesha hapa kuwa hilo jimbo la Same magharibi lina kata ngapi na uzitaje hizo kata kwa majina?
 
Kata za Same Magharibi: Bangalala, Chome, Gavao Saweni, Hedaru, Kisiwani, Kisima, Makanya, Mabilioni, Mshewa, Mhezi, Msindo, Mwembe, Same Mjini, Ruvu, Njoro, Suji, Stesheni, Tae, Vudee, Vumari.
 
Ameshanirudishia, ila majizi ya kura huwa sijipendekezi nayo.
Zitumie basi kufikiria ili uone kwamba hata sisi huku vijijini tunastahili kupata huduma ya kuwahishwa hospitali tukizidiwa badala ya kwenda kwa bodaboda. Tatizo lenu watu wa mjini huwa hamtufikirii sisi walala puu wa huku vijijini: sisi tunapata magari ya kutuhudumia, wewe unaona hiyo hduma haitustahili!
 
Back
Top Bottom