Mbunge wa Ulanga, Salim Almas agawa Smartphone 63 (Milioni 7) kwa Wajumbe wa CCM Wilaya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,908
945

MBUNGE SALIM ALMAS AGAWA SMARTPHONE 63 KWA WAJUMBE WA CCM

Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mhe. Salim Almas amegawa simu janja (smartphone) 63 zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Saba (07) kwa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ulanga ili kurahisisha mawasiliano na kupeana taarifa zinazohusu shughuli za kimaendeleo jimboni hapo.

Viongozi 63 wa Kata zote 21 za Wilaya Ulanga Wenyeviti, Makatibu na Waenezi wamepatiwa Simjanja(Smartphone) na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano baina ya viongozi hao na mbunge ili kurahisha utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi.

Hafla ya kugawa simu janja hizo imefanyika kwenye tamasha la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan ambalo limeandaliwa na Umoja wa Vijana UVCCM katika Wilaya ya Ulanga

Katika hatua nyingine Mbunge Salim ametoa bima za Afya kwa wajumbe wa Chama cha Mapinduzi kutoka katika Kata 21 za Wilaya hiyo ili ziwasaidie kupata matibabu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Hasham amesema, Amechukua uamzi huo baada ya kukosekana kwa namna bora inayowaweka pamoja katika kufanya majadiliano ya haraka katika kuwahudumia wananchi, ambapo kupitia simu kushindwa group la pamoja katika mtandao wa kijamii wa whatsapp utakaofungua ukurasa mpya kwa pamoja kwa viongozi hao.

Mbali na simujanja, viongozi hao wamekabidhiwa bima za afya kila mmojakwa ajili ya kuwawezesha kupata huduma za afya ambapo baadhi yao wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kushindwa kumudu gharamaza matibabu huku akiahidi pia kuwapatia wajumbe wote wa matawi CCM Bima za afya.

Kwa upande wao viongozi wa UVCCM Wilaya ya Ulanga walioandaa tamasha hilo akiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Wilayani hapo Shahista Kuyela pamoja na Katibu wa hamasa Thomas Machupa Wamemshukuru Mhe. Rais Samia pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo kwa kutekeleza vyema ilani ya Chama hicho jimboni hapo.


hqdefaultsawert.jpg
WhatsApp Image 2023-06-13 at 10.44.42.jpeg
WhatsApp Image 2023-06-13 at 10.44.42(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-06-13 at 10.44.42(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-06-13 at 10.44.42(4).jpeg
WhatsApp Image 2023-06-13 at 10.44.43.jpeg
IMG-20220306-WA0009.jpg
IMG-20220306-WA0011.jpg
 
Sasa hapo kawanunulia simu gani 😀😀😀kama zote zinafanana maana yake kila simu imemcost laki moja na Elfu kumi (110k) au ndo kawanunulia kwa bei ya jumla Kariakoo.
 
1686658767498.png


Kuna mjumbe amebadili muondoko kwaajili ya simu ya rushwwa
 
Hivi mbona mkoa wa Morogoro wanapenda kuchagua wabunge wahindi na waarabu hakuna wazawa wenye uwezo wa kuwa wabunge?
 
Back
Top Bottom