Mbunge Condester Sichalwe aendesha Semina ya Kilimo Chenye Tija Kata ya Myunga JImbo la Momba

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Mbunge wa Jimbo la Momba Mkoa wa Songwe, Mhe. Condester Mundy Michael Sichalwe leo tarehe 02 Julai, 2023 amefanya kikao cha ndani kilichowakutanisha viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Kata ya Myunga na Mtaalamu wa Kilimo kutoka Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na Benki ya NMB

Mbunge Condester Sichalwe amesema kuwa lengo la kikao na mikutano anayofanya kuwakutanisha wananchi na viongozi na Wataalam wa Kilimo ni ili kuwasaidia wazawa wa Komba kunufaika na Uwekezaji wa Kilimo chenye tija kwani wanaonufaika na Ardhi ni wageni wanaokuja kuwekeza

Kikao cha ndani Kata ya Myunga kimefanyika Ukumbi wa Chuo cha DIT kikiwa na lengo la kuwapa semina wakulima kutoka kwa Afisa Kilimo Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwa kushirikiana na Taasisi ya Kifedha ikiwemo Benki ya NMB ili kuwapa Elimu ya mikopo inavyoweza kuwasaidia wakulima.

Ndugu Marco Jacob Ndonde amewafundisha wakulima kuhusu Kilimo cha Mkataba, Pembejeo za Kilimo (MboleanaMbegu), Dhamana ya kuchukua mikopo, Bima ya Mashamba, kuunda vikundi vya ushirika ili wavitumie kama dhamana ya kuchukua mikopo kutoka Benki.

Ndugu Marco Jacob Ndonde amesema mikopo ya Benki kwa wakulima inatolewa kwa mtu mmoja kama atakuwa na Hekari kuanzia 50 na kama mtu pekee hawezi kumiliki Hekari 50 basi wanatakiwa kuunda kikundi cha watu kuanzia 20 na kuunganisha mashamba yao ili iwe rahisi kukopesheka kutoka Benki

Aidha, Ndugu Marco Ndonde amesema mkulima kama akitumia Kilimo chenye tija na ufanisi kwa Hekari moja ya Mahindi anaweza kuvuna Gunia 25 na kuendelea za Mahindi endapo ataweka Mbolea ya kutosha, Kupanda na kupalilia shamba kwa wakati.

Afisa wa Benki ya NMB Tunduma amesema upo uwezekano mkulima akapata Mkopo kwaajili ya kuendesha shughuli za kilimo na kujiunga na Bima ya Mashamba ili kuondoa hasara endapo majanga yamejitokeza kwenye msimu wa Kilimo kama Ukame, Mifugo kula Mazao, Mafuriko ya Mvua, Wadudu na majanga asili endapo yametokea.

Mbunge Condester Sichalwe amesema kuwa semina za kuwaelimisha wakulima juu ya Kilimo chenye tija kitakuwa ni endelevu na kuwasisitiza kuhudhuria mafunzo ya Kilimo yanayotolewa na Maafisa Kilimo watakapokuja kuwafundisha wananchi wote.

20230802_142748.jpg
20230802_141943.jpg
20230802_141754.jpg
20230802_142819.jpg
20230802_142900.jpg
20230802_142859.jpg
20230802_142911.jpg
20230802_162357.jpg
20230802_162352.jpg
 
Back
Top Bottom