Mbunge Chiku Abwao apata ajili, anusurika kifo

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,879
1,250
MBUNGE CHIKU ABWAO ANUSURIKA KUFA AJALI YA GARI

DSCF0307.JPG
DSCF0308.JPG
DSCF0316.JPG
DSCF0300.JPG

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha Demokrasia na maendeo (Chadema) Chiku Abwao amenurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 252 BSX VX ambalo alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kuja Iringa kukwanguliwa na fuso katika eneo la Doma mkoani Morogoro usiku wa leo

Akizungumza na Francis Godwin, leo mbunge huyo alisema kuwa lori hilo aina ya fuso lilimfuata upande wake na kumgonga na kuendelea na safari na kuwa bila umakini wa dereva wake hali ya usalama wake ulikuwa mdogo sana.

Kwani alisema kuwa lori hilo baada ya kukwangua upande wa dereva halikuweza kusimama liliendelea na safari na wao kupelekea taili la moja lilipasuka na kupelekea gari lao kuhama njia.

Hata hivyo alisema katika gari hilo walikuwa yeye na dereva wake na kuwa hakuna aliyejeruhiwa kutokana na kufunga mikanda na kuwa mikanda na mwendo mzuri wa dereva wake ndio umesaidia kupona katika ajali hiyo.
 
OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,971
2,000
Naanza kupata hofu huenda umafia unarejea Tanzania! Itabidi jumuiya ya kimataifa isaidie maana wakipewa hii kazi TISS ni walewale tu!!
 
Rejao

JF-Expert Member
May 4, 2010
9,237
2,000
Kwenye ile list ya kurithi nafasi ya viti maalum nani anafuatia? Naona CDM wanamalizana wenyewe kwa wenyewe taratiiibu, mbaya zaidi kwa staili ile ile ya ajali!!
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,069
0
MBUNGE CHIKU ABWAO ANUSURIKA KUFA AJALI YA GARI

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha Demokrasia na maendeo (Chadema) Chiku Abwao amenurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 252 BSX VX ambalo alilokuwa akisafiria kutoka Dodoma kuja Iringa kukwanguliwa na fuso katika eneo la Doma mkoani Morogoro usiku wa leo

Akizungumza na mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima leo mbunge huyo alisema kuwa lori hilo aina ya fuso lilimfuata upande wake na kumgonga na kuendelea na safari na kuwa bila umakini wa dereva wake hali ya usalama wake ulikuwa mdogo sana.

Kwani alisema kuwa lori hilo baada ya kukwangua upande wa dereva halikuweza kusimama liliendelea na safari na wao kupelekea taili la moja lilipasuka na kupelekea gari lao kuhama njia .

Hata hivyo alisema katika gari hilo walikuwa yeye na dereva wake na kuwa hakuna aliyejeruhiwa kutokana na kufunga mikanda na kuwa mikanda na mwendo mzuri wa dereva wake ndio umesaidia kupona katika ajali hiyo.

Ajali haina kinga, kisa cha kutoka Dodoma ukapita Doma? wakati kuna njia Dodoma - Iringa, shortcut kabisa. Una VX halafu unaona ubahili kulipitisha rough road, faida yake nini kuwa na gari kama hilo?

Distance between Iringa and Dodoma is 177.66 km

Dodoma - Morogoro 224 km - Iringa 242 km Total: 466 k,
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,356
2,000
Ajali haina kinga, kisa cha kutoka Dodoma ukapita Doma? wakati kuna njia Dodoma - Iringa, shortcut kabisa. Una VX halafu unaona ubahili kulipitisha rough road, faida yake nini kuwa na gari kama hilo?

Distance between Iringa and Dodoma is 177.66 km

Dodoma - Morogoro 224 km - Iringa 242 km Total: 466 k,
Mkuu huenda alikuwa na mambo yake huko Moro. Halafu pamoja na kwamba Dom - Iringa ni karibu lakini barabara si nzuri watu wanaepusha viuno na migongo yao. Ajali zitatumaliza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom