Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 289
- 489
Dk Tulia Ackson ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu.
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Hamisi Nderiananga wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda.
Katika swali lake Mwakagenda aliuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini ambalo linaongozwa na Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson kutokana na ukubwa wake.
Kutokana na ombi hilo kumeibuka mvutano wa mawazo baadhi ya wananchi wakihoji umuhimu wa ombi hilo.
Kwanini Jimbo ligwanywe? (zitolewe sababu zenye mashiko) ambazo zitakidhi ombi hilo kwa umma wa Watanzania.
kwa Jimbo lililopo (Mbeya Mjini) lina changamoto gani za kimaendeleo, na ikiwa zipo, kuligawanya ndio suluhisho?
Kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya 2022, Mbeya Mjini si miongoni mwa majimbo 10 ya uchaguzi yenye watu wengi Tanzania, hivyo hata wapiga kura hawawezi kuwa wengi Kama hayo majimbo 10 yenye watu wengi.
Taifa linapitia kipindi cha ufisadi na matumizi makubwa yasiyo ya lazima ya fedha za umma, je kwanini bunge liendelee kuongeza idadi ya wabunge jambo ambalo litafanya kuongezeka kwa Bajeti ya matumizi ya bunge badala ya kuwekeza kwenye mambo mengine ya maendeleo?.
Je Mbunge wa Mbeya Mjini na wananchi wengine wanaopendekeza jimbo ligawanywe wameona jimbo ni kubwa hivyo linampa mzigo Mbunge kuliongoza na kutimiza ajenda za uwakilishi bungeni?.
[emoji2398] Peter Mwaihola