Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani?

Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani?

Wewe ndio wale wanaoitwa prophets of doom. Manabii wa vifo. Nchi itatawalika tu, hiyo mikwara pelekeni huko kwenye mikutano yenu ya ndani.
Mkuu ni rahisi sana kuorodhesha mengi ambayo mnaona hayafanyiki, lakini kumbukeni kwamba hata kuja na wazo moja zuri ni sehemu ya kuijenga Tanzania yenye neema.
Kusema kwamba kaka mkubwa anayo haki ya kukataa wito ni haki yake kufanya hivyo, kama ambavyo mamlaka ya mkuu wa mkoa yanavyomruhusu Makonda kumuita central mkazi yoyote wa Dar kwa ajili ya mahojiano.
Wewe njaa zako zimekuondolea ufahamu
 
hahahahah!!
Ingekuwa hivi unavyosema asingeende kupekuliwa nyumbani kwake. Hata hivyo sidhani kama ni njia sahihi ambazo polisi na Makondo kama zilikuwa sahihi. huwezi kumhisi mtu na dawa za kulevya then unatangaza kwenye vyombo vya habari na baada ya hapo unamuita polisi eti baadaye ndo unaenda kupekeu. Hata kama mtu anahusika mzigo utakuwa ushahamishwa.
"Hawa jamaa wanaofanya biashara za namna hii ambazo ni hatari huwa hawaachi TRACE "
 
Sina nia mbaya kukumbusha. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 'alianzisha' vita dhidi ya madawa ya kulevya mkoani Dar es Salaam na sasa vita hiyo imetapakaa Tanzania nzima. RC Makonda alikuwa akiongea kwa kujiamini, kutaja na kuagiza. Alikuwa akisubiriwa kwa hamu pale alipokuwa akitakiwa kutokeza na kuzungumza.

Siku alipotajwa Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa pamoja na Manji na Gwajima, mambo yakabadilika. Kwanza, kila aliyetajwa hapo akazungumza na waandishi wa habari. Mbowe akaenda mbali zaidi na kutamka kuwa hatakwenda kuripoti Central Police kwakuwa aliyemwita (Makonda) hana mamlaka ya kumwita.

Baada ya tamko hilo la Mbowe, mambo yakachachamaa. Wakajitokeza watanzania kwa maelfu wanaomuunga mkono Mbowe na wale wanaompinga. Kilichofuata ni kuteuliwa kwa Kamishna Mkuu wa Kamisheni ya Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini ambaye kimsingi ndiye sasa ameyachukua majukumu yake ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Kuanzia siku alipotajwa Mbowe wa CHADEMA vita ya madawa ya Makonda ikapata dhoruba kali kwa kumbadili kiongozi wa vita hiyo. Kuanzia siku alipotajwa Mbowe, hakujawahi kuwepo na kutajwa washukiwa wengine wa matumizi au kuingiza madawa ya kulevya. Siku aliyotajwa Mbowe wa CHADEMA ikawa ndiyo turning point.

Yawezekana kutajwa kwa Mbowe kukasababisha hata mashauri ya madai dhidi ya RC Makonda kuhusu udhalilishaji kama ambavyo Mbowe anapanga kuanza kufanya hivyo. Kimsingi, najiuliza, Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani hadi 'kubadili' upepo wa mambo yote hayo?
Kiafrika, mkubwa hata akikosea huwa haombi msamaha...kawaida yetu kiafrika Afrika ni kuwa mkubwa wako akikukosea utaona tu anabadirisha mwelekeo na matendo yake. Kwa mtoto/mdogo mwenye hekima huona na kutambua kuwa hapa mkubwa wangu kakubari kukosea na tayari keshajirekebisha.
Inawezekana kabisa kulikuwa na utashi wa kupambana na hayo madawa na binafsi naunga mkono kabisa vita hiyo, tatizo lilikuja kwenye approach na hapo ndo walipotajwa hao watu (akiwemo Mbowe) waliona huo mwanya na wakaamua kuutumia kupita.
Kauli zilikuja nyingi toka kwa watendaji wa serikali wakipiga kelele juu ya approach...kiafrika tukajua kuwa mkubwa kakubari alikosea....
 
Wale maaskofu waliopenyeza ile orodha ya awali walisema kabisa hawakumtaja Freeman Mbowe personally; bali Billicanas Club.

Conductor alipomtaja Mbowe ndo watu wakashtuka kwamba hii vita ni ya visasi na kukomoana tu na si vinginevyo
 
d2842251d3df64d2987366ae6b18a5fb.jpg
 
Mkuu, Mbowe anaishi Mikocheni Dar. Makonda ni mkuu wa mkoa wa Dar, kwanini asiwe na mamlaka ya kumuita mkazi wake aende central police. Kina Iddi Azzan na wengine mbona walikwenda central na mambo yakaisha?.

Mzee Mtei ambaye ndiye mwanzilishi wa CDM kasema Mbowe ajitafakari hapa alipofikia, kwani kutajwa jina lake ni doa kwa chama ambacho yeye Mzee Mtei alikianzisha.


Tatizo ambalo ni la msingi ni baadhi ya wanasiasa kushindwa kubadilika kadri ya muda unavyokwenda. Siasa za kuvimbiana zilifanyika enzi zile za JK aliyeweza kumchekea yoyote yule aliye mbele ya macho yake. Awamu ya tano haivimbiwi kipuuzi tu.
Oli bishansha
 
Hahahaha Wema Sepetu na Mzee ENL hao ndio wanachama wetu muhimu. Kazi kwelikweli.
Upekee alionao ni kukinyima chama changu ccm usingizi mwisho tumeamua kuendesha nchi kama Chama kipya kinachotangaza sera zake kijana katushika kubaya ndo maana hatuishi kumtaja mtu ambaye hanaga maneno mengi. Huyu ndo Mbowe bwiji la Siasa za Tanzania ni kweli hatupati usingizi kwa ajili ya huyu kijana mwenye siasa za kuunganisha taifa bila kubagua itikadi yoyote. Hongera Mbowe kwa kuliamusha taifa hili kubwa la Tanzania

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Upekee alionao ni kukinyima chama changu ccm usingizi mwisho tumeamua kuendesha nchi kama Chama kipya kinachotangaza sera zake kijana katushika kubaya ndo maana hatuishi kumtaja mtu ambaye hanaga maneno mengi. Huyu ndo Mbowe bwiji la Siasa za Tanzania ni kweli hatupati usingizi kwa ajili ya huyu kijana mwenye siasa za kuunganisha taifa bila kubagua itikadi yoyote. Hongera Mbowe kwa kuliamusha taifa hili kubwa la Tanzania

Post sent using JamiiForums mobile app
Huyu ni mmoja wa wale waliopiga deki barabara mwaka 2015. Anasubiri tu aambiwe lini aingie mtaani. Aina hii ndio mitaji ya wanasiasa wa kiafrika.
 
Back
Top Bottom