Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 137,707
- 272,594
Bilionea Mbowe ni jabali la kisiasa la Tanzania , kumtumia kidagaa Bashite apambane naye ni kupoteza muda tu !Jibu ni moja tu, hii vita ya madawa aliyoianzisha Makonda ni feki, wameanzia kwa wasanii, wakaja sijui kwa akina nani, lakini lengo lao kuu ni Mh. Mbowe.
Na huu ni mkakati maalum, usidhani Makonda aliamka tu asubuhi akaanzisha haya maigizo. Ni mkakati ambao ulisukwa kwa lengo la kudhoofisha upinzani wakilenga kumchafua Freeman Aikael Mbowe maana ni moja ya watu ambao ni tishio kwa chama dola. Na mkakati huu una baraka zote kutoka juu.
Na ndio maana hutasikia Makonda akiendelea kutaja tena majina maana mlengwa mkuu tayari ameshatajwa. Bahati mbaya mikakati yao huwa haifanikiwi, maana ni ya kishetani.
Mfano hai ni huu hapa , WAKATI KIDAGAA BASHITE KIKIKAUKA JUANI NA KUSUBIRI KICHUKULIWE NA KUNGURU , JABALI MBOWE LINASONGA MBELE .