Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani?

Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani?

Mkuu ina maana ni kweli huoni utofauti wa manji, gwajima, mbowe na watu wengine? basi kama binadam wote ni sawa nitukane mimi alafu mtukane mtukufu uone kitatokea nini
 
Petro E. Mselewa

Kila mtu ana upekee na anastahili heshima kama ilivyoainishwa katika katiba na sharia.

Mbowe kaamua tu kutumia haki yake, kwa hivyo, hana upekee zaidi ya huo wa kutumia haki yake.

Watanzania wengi tukuiona tunaonewa tunakuwa warahisi kusema "hewalla, mungu atalipa". Mbowe anaondokana na dhana hiyo.
 
Sina nia mbaya kukumbusha. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 'alianzisha' vita dhidi ya madawa ya kulevya mkoani Dar es Salaam na sasa vita hiyo imetapakaa Tanzania nzima. RC Makonda alikuwa akiongea kwa kujiamini, kutaja na kuagiza. Alikuwa akisubiriwa kwa hamu pale alipokuwa akitakiwa kutokeza na kuzungumza.

Siku alipotajwa Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa pamoja na Manji na Gwajima, mambo yakabadilika. Kwanza, kila aliyetajwa hapo akazungumza na waandishi wa habari. Mbowe akaenda mbali zaidi na kutamka kuwa hatakwenda kuripoti Central Police kwakuwa aliyemwita (Makonda) hana mamlaka ya kumwita.

Baada ya tamko hilo la Mbowe, mambo yakachachamaa. Wakajitokeza watanzania kwa maelfu wanaomuunga mkono Mbowe na wale wanaompinga. Kilichofuata ni kuteuliwa kwa Kamishna Mkuu wa Kamisheni ya Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini ambaye kimsingi ndiye sasa ameyachukua majukumu yake ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Kuanzia siku alipotajwa Mbowe wa CHADEMA vita ya madawa ya Makonda ikapata dhoruba kali kwa kumbadili kiongozi wa vita hiyo. Kuanzia siku alipotajwa Mbowe, hakujawahi kuwepo na kutajwa washukiwa wengine wa matumizi au kuingiza madawa ya kulevya. Siku aliyotajwa Mbowe wa CHADEMA ikawa ndiyo turning point.

Yawezekana kutajwa kwa Mbowe kukasababisha hata mashauri ya madai dhidi ya RC Makonda kuhusu udhalilishaji kama ambavyo Mbowe anapanga kuanza kufanya hivyo. Kimsingi, najiuliza, Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani hadi 'kubadili' upepo wa mambo yote hayo?
Upekee alionao Mbowe ni mkubwa sana kama ulionao wewe kwavile tu hujajua haki zako na jinsi ya kuzidai
Hadhi ya mtanzania ni kubwa sana kuvunjwa kienyeji hadharani kwa mtu mmoja mwenye mamlaka.
Haki ya kuheshimiwa
Haki ya kusikilizwa
Haki za kikatiba hizi ni za wote pamoja na wewe.
 
mbowe ni mtu potential sana
kama si yeye chadema ingekuwa chalii
Kesho utasema Baca bila mesi ingekua chali

Wafwaaaa

Tanzania bila Nyerere chalii

Hata mimi zamaniiiii nilidhani kama unavyodhani wewe but dunia hii no body in is indispensable
 
Jibu ni moja tu, hii vita ya madawa aliyoianzisha Makonda ni feki, wameanzia kwa wasanii, wakaja sijui kwa akina nani, lakini lengo lao kuu ni Mh. Mbowe.

Na huu ni mkakati maalum, usidhani Makonda aliamka tu asubuhi akaanzisha haya maigizo. Ni mkakati ambao ulisukwa kwa lengo la kudhoofisha upinzani wakilenga kumchafua Freeman Aikael Mbowe maana ni moja ya watu ambao ni tishio kwa chama dola. Na mkakati huu una baraka zote kutoka juu.

Na ndio maana hutasikia Makonda akiendelea kutaja tena majina maana mlengwa mkuu tayari ameshatajwa. Bahati mbaya mikakati yao huwa haifanikiwi, maana ni ya kishetani.
Sina la kuongeza. Hii Nchi watu wenye hekima wamepotea. Ikiwa Nchi zenye akili na utajiri wa kila namna wanaheshimu upinzani, itakuaje sie ombaomba tuukatae? Nahisi hii Nchi inaongozwa na RAIA wa kigeni! Watanzania hawakuwa hivi! Serikali haiwezi kuwabadilikia Watanzania kiasi hiki kwa muda mfupi tu. Kauli zenye utata mwingi, kejeli na kiburi zimetamalaki hadi kwa Vijana wadogo kisa wameokota uongozi! Nasema wameokota. Namaanisha.
 
Mkuu nikusahihishe, aliyetajwa na makonda ni philemony mbowe, sijui kwanini freeman anahamaki?

Huyo mbunge wa hai anasakwa na kamanda sirro kwa sababu ambazo jeshi la polisi halijasema, inawezekana ni madawa au kuhusu kauli za tundu lissu au masuala yake ya kibiashara au ni sababu anazozijua yeye sirro.
BAADA YA KUSOMA HILO jina uliloandika hapo, alifafanua kuwa ni mbunge wa Hai lakini ana makazi pia hapa Dar. Ungemuuliza Makonda alimaanisha nini kuandika hivyo na kumtaja kuwa ni mbunge wa hai??? kakosea au kisiasa zaidi kuchanganya hilo jina na mbunge wa HAI. msianze kuyumbisha muelekeo wa upepo.
Aise wajanja nyie nani kawatuma! baada ya kuona kapekuliwa na hakuna kitu, wakakwapua visivyohusika na madawa sasa mnaangalia namna ya kumpachikia kitu (kosa). eti Sirro alikuwa anamtafuta kwa sababu azijuazo. Haya lete hizo sababu mana tayari mmezipanga
 
Mbowe ni jabali la siasa za Tanzania , sasa mzee wa kutumwa Makonda akijua hana ushahidi wowote akaamua kumburuza Sirro ili wajaribu kulisukuma jabali , kilichowakuta na kitakachoendelea kuwakuta watajuta kuzaliwa .

Shukrani kubwa zimwendee Tulia Ackson kwa kumnusuru Kasim Majaliwa na swali la papo kwa papo , kuhusu mpango wa kishamba wa ccm kufuta vyama vingi Tanzania .
 
Kwani magufuli ana upekee gani hata I we nongwa kusemwa? Wanasemwa Obama,Trump,Merkel,Sarkoz, Mugabe,Kenyatta,kikwete sembuse yeye? Kama unaona Mbowe ni wa kawaida hata huyo n simple vile vile!
 
All in all Mbowe ni kiongozi wa kambi ya upinzani Mr Peter wewe kama mwanasheria unaelewa hadhi ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Pili Mbowe Ni mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini na pia hapo Mr Peter unajua tosha. Tatu Mbowe Ni mwakirishi wa wananchi wa Jimbo la Hai tofauti na wengine wote waliopata kutajwa na huyo chizi. Sifa hizo tatu hakuna aliyenazo hata moja kati ya wale wote waliotajwa. Na kwa mantiki hiyo unapotaka kumdharirisha mtu kama huyu aidha kwa makusudi au kwa kutojua lazima uonyeshwe njia halali ya kufuata kwani kwa kukuacha na ukaendelea kuvunja heshima za watu wanaoongozwa na huyo mtu ni kuonyesha ujingà.
 
Mkuu, Mbowe anaishi Mikocheni Dar. Makonda ni mkuu wa mkoa wa Dar, kwanini asiwe na mamlaka ya kumuita mkazi wake aende central police. Kina Iddi Azzan na wengine mbona walikwenda central na mambo yakaisha?.

Mzee Mtei ambaye ndiye mwanzilishi wa CDM kasema Mbowe ajitafakari hapa alipofikia, kwani kutajwa jina lake ni doa kwa chama ambacho yeye Mzee Mtei alikianzisha.

Tatizo ambalo ni la msingi ni baadhi ya wanasiasa kushindwa kubadilika kadri ya muda unavyokwenda. Siasa za kuvimbiana zilifanyika enzi zile za JK aliyeweza kumchekea yoyote yule aliye mbele ya macho yake. Awamu ya tano haivimbiwi kipuuzi tu.
Hayo ndo siku moja watu watalala na mkeo na kwakuwa jamaa ni wababe hutowafanya kitu sababu huwa hawajaribiwi karagabahu mkubwa ww.
 
Sina nia mbaya kukumbusha. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 'alianzisha' vita dhidi ya madawa ya kulevya mkoani Dar es Salaam na sasa vita hiyo imetapakaa Tanzania nzima. RC Makonda alikuwa akiongea kwa kujiamini, kutaja na kuagiza. Alikuwa akisubiriwa kwa hamu pale alipokuwa akitakiwa kutokeza na kuzungumza.

Siku alipotajwa Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa pamoja na Manji na Gwajima, mambo yakabadilika. Kwanza, kila aliyetajwa hapo akazungumza na waandishi wa habari. Mbowe akaenda mbali zaidi na kutamka kuwa hatakwenda kuripoti Central Police kwakuwa aliyemwita (Makonda) hana mamlaka ya kumwita.

Baada ya tamko hilo la Mbowe, mambo yakachachamaa. Wakajitokeza watanzania kwa maelfu wanaomuunga mkono Mbowe na wale wanaompinga. Kilichofuata ni kuteuliwa kwa Kamishna Mkuu wa Kamisheni ya Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini ambaye kimsingi ndiye sasa ameyachukua majukumu yake ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Kuanzia siku alipotajwa Mbowe wa CHADEMA vita ya madawa ya Makonda ikapata dhoruba kali kwa kumbadili kiongozi wa vita hiyo. Kuanzia siku alipotajwa Mbowe, hakujawahi kuwepo na kutajwa washukiwa wengine wa matumizi au kuingiza madawa ya kulevya. Siku aliyotajwa Mbowe wa CHADEMA ikawa ndiyo turning point.

Yawezekana kutajwa kwa Mbowe kukasababisha hata mashauri ya madai dhidi ya RC Makonda kuhusu udhalilishaji kama ambavyo Mbowe anapanga kuanza kufanya hivyo. Kimsingi, najiuliza, Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani hadi 'kubadili' upepo wa mambo yote hayo?
Watu wanamwamini na walijua ilikuwa ni character assassination tu
 
All in all Mbowe ni kiongozi wa kambi ya upinzani Mr Peter wewe kama mwanasheria unaelewa hadhi ya kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni. Pili Mbowe Ni mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini na pia hapo Mr Peter unajua tosha. Tatu Mbowe Ni mwakirishi wa wananchi wa Jimbo la Hai tofauti na wengine wote waliopata kutajwa na huyo chizi. Sifa hizo tatu hakuna aliyenazo hata moja kati ya wale wote waliotajwa. Na kwa mantiki hiyo unapotaka kumdharirisha mtu kama huyu aidha kwa makusudi au kwa kutojua lazima uonyeshwe njia halali ya kufuata kwani kwa kukuacha na ukaendelea kuvunja heshima za watu wanaoongozwa na huyo mtu ni kuonyesha ujingà.
Mkuu, tambua kuwa Mbowe pamoja na vyeo vyake vyote ni mkazi wa mikocheni Dar. Makonda ni mkuu wa mkoa wa Dar na moja kwa moja ni kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama.

Kumbuka jinsi ambavyo Kubenea alivyoswekwa ndani baada ya kubishana na Makonda.

Mkuu wa mkoa ni extended arm of the president. Sasa usimuangalie Makonda kama rafiki yako unayeweza kumnunulia soda mkikutana disco usiku ukamlinganisha na Makonda mkuu wa mkoa wa Dar.
 
Majibu yenyewe kama ndiyo haya, basi mkoloni akiamua kurudi Barani Afrika ni rahisi sana kututawala tena!! Oh yes - we're disorganised lot mpaka tunasahau kabisa kuwa wamoja katika vita ya ku-save nguvu kazi ya Taifa letu dhidi ya madawa ya kulevya, badala yake mnakimbilia kumtetea MBOWE wakati hamjui alikuwa anaitwa Kituo cha Polisi kwa kosa gani? - masaa yote kutumbukiza siasa kwa kusingizia Serikali kwamba inakadamiza demokrasia na kudhoofisha upinzani Nchini, actually yeye kama Kiongozi wa upinzani alipashwa kuonyesha mfano bora kwa kuiitikia wito wa Polisi kuliko kubishana bishana nao, kwani walio itikia mwito wa Polisi kawazidi nini?
Ukijua sheria umejua haki zako za msingi usiwe wa kuburizwa tu.
 
Sina nia mbaya kukumbusha. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 'alianzisha' vita dhidi ya madawa ya kulevya mkoani Dar es Salaam na sasa vita hiyo imetapakaa Tanzania nzima. RC Makonda alikuwa akiongea kwa kujiamini, kutaja na kuagiza. Alikuwa akisubiriwa kwa hamu pale alipokuwa akitakiwa kutokeza na kuzungumza.

Siku alipotajwa Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa pamoja na Manji na Gwajima, mambo yakabadilika. Kwanza, kila aliyetajwa hapo akazungumza na waandishi wa habari. Mbowe akaenda mbali zaidi na kutamka kuwa hatakwenda kuripoti Central Police kwakuwa aliyemwita (Makonda) hana mamlaka ya kumwita.

Baada ya tamko hilo la Mbowe, mambo yakachachamaa. Wakajitokeza watanzania kwa maelfu wanaomuunga mkono Mbowe na wale wanaompinga. Kilichofuata ni kuteuliwa kwa Kamishna Mkuu wa Kamisheni ya Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini ambaye kimsingi ndiye sasa ameyachukua majukumu yake ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Kuanzia siku alipotajwa Mbowe wa CHADEMA vita ya madawa ya Makonda ikapata dhoruba kali kwa kumbadili kiongozi wa vita hiyo. Kuanzia siku alipotajwa Mbowe, hakujawahi kuwepo na kutajwa washukiwa wengine wa matumizi au kuingiza madawa ya kulevya. Siku aliyotajwa Mbowe wa CHADEMA ikawa ndiyo turning point.

Yawezekana kutajwa kwa Mbowe kukasababisha hata mashauri ya madai dhidi ya RC Makonda kuhusu udhalilishaji kama ambavyo Mbowe anapanga kuanza kufanya hivyo. Kimsingi, najiuliza, Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani hadi 'kubadili' upepo wa mambo yote hayo?
Mkuu, Mbowe ni Mwenyekiti wa chama kikubwa cha upinzani chenye wafuasi zaidi ya ccm, ila Kwa ubovu wa katiba ndo maana ccm inajitangazia ushindi.
Iko wazi kabisa kuwa, tuhuma za Mbowe na manji ni za kisiasa, na lengo ni kuharibu upinzani.
Kama kweli serikali ya Magufuli inatenda haki.
1.Kwanini hajarudisha mabilioni ya pesa za umma yaliyofichwa nje ikiwepo na pesa za rushwa za chenge?
2.Kwanini hataki kushughulika na dubwasha linaloitwa IPTL?
3.Mbona ishu ya ESCROW kaikaushia?
4.Kwanini hataki kuajiri na wakati anajua kuwa watu wakikosa ajira ndo uhalifu unazidi.
5.Kwanini amebariki wizi wa pesa za mifuko ya jamii? mtu analipa kodi kila mwezi halafu na pesa zake unampora na wakati serikali haina hata cent ktk hizo pesa.
Kutenda haki huwa ni ngumu Sana, anaishia kuonea watu tu wasio na hatia na anasahau kuwa aliapa hadi Kwa push up kuwa kamwe hataweza kutunguasha, Leo katugeuka utadhani siyo yeye.
 
Mkuu, tambua kuwa Mbowe pamoja na vyeo vyake vyote ni mkazi wa mikocheni Dar. Makonda ni mkuu wa mkoa wa Dar na moja kwa moja ni kiongozi wa kamati ya ulinzi na usalama.

Kumbuka jinsi ambavyo Kubenea alivyoswekwa ndani baada ya kubishana na Makonda.

Mkuu wa mkoa ni extended arm of the president. Sasa usimuangalie Makonda kama rafiki yako unayeweza kumnunulia soda mkikutana disco usiku ukamlinganisha na Makonda mkuu wa mkoa wa Dar.
Nilikuwa namjibu mleta mada maswali aliyouliza, pili naombà nikujibu na wewe kuwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama haina maana usifuate sheria na taratibu katika kutekeleza majukumu yako. Kumbuka inapoishia haki yako kama kiongozi ndipo haki ya mwenzio inapoanzia. Na kwa mantiki hiyo makonda alishindwa kujua mipaka ya haki na wajibu wake kama mkuu wa mkoa na kwa hali hiyo akawa ameingilia haki za mtu mwingine. Kumbuka Tanzaniai ilisaini na ikaridhia tamko la kimataifa la haki za binadamu na ibara ya 30 ambayo ndiyo ibara ya mwisho inaweka ulinzi wa tamko hilo kuwa hakuna mwanachama yeyote atakayekuwa na mamlaka ya kubadili au kufanya marekebisho yoyote ktk tamko hilo. Hata sheria zetu za nchi pia zins hicho kitu.
 
Back
Top Bottom