Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani?

Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani?

Sina nia mbaya kukumbusha. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 'alianzisha' vita dhidi ya madawa ya kulevya mkoani Dar es Salaam na sasa vita hiyo imetapakaa Tanzania nzima. RC Makonda alikuwa akiongea kwa kujiamini, kutaja na kuagiza. Alikuwa akisubiriwa kwa hamu pale alipokuwa akitakiwa kutokeza na kuzungumza.

Siku alipotajwa Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa pamoja na Manji na Gwajima, mambo yakabadilika. Kwanza, kila aliyetajwa hapo akazungumza na waandishi wa habari. Mbowe akaenda mbali zaidi na kutamka kuwa hatakwenda kuripoti Central Police kwakuwa aliyemwita (Makonda) hana mamlaka ya kumwita.

Baada ya tamko hilo la Mbowe, mambo yakachachamaa. Wakajitokeza watanzania kwa maelfu wanaomuunga mkono Mbowe na wale wanaompinga. Kilichofuata ni kuteuliwa kwa Kamishna Mkuu wa Kamisheni ya Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini ambaye kimsingi ndiye sasa ameyachukua majukumu yake ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Kuanzia siku alipotajwa Mbowe wa CHADEMA vita ya madawa ya Makonda ikapata dhoruba kali kwa kumbadili kiongozi wa vita hiyo. Kuanzia siku alipotajwa Mbowe, hakujawahi kuwepo na kutajwa washukiwa wengine wa matumizi au kuingiza madawa ya kulevya. Siku aliyotajwa Mbowe wa CHADEMA ikawa ndiyo turning point.

Yawezekana kutajwa kwa Mbowe kukasababisha hata mashauri ya madai dhidi ya RC Makonda kuhusu udhalilishaji kama ambavyo Mbowe anapanga kuanza kufanya hivyo. Kimsingi, najiuliza, Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani hadi 'kubadili' upepo wa mambo yote hayo?
Mbowe ni kiongozi kipenzi cha watanzania asiye lazimisha kuombewa wala kuungwa mkono
 
hana upekee wowote...
 
Mkuu nikusahihishe, aliyetajwa na makonda ni philemony mbowe, sijui kwanini freeman anahamaki?

Huyo mbunge wa hai anasakwa na kamanda sirro kwa sababu ambazo jeshi la polisi halijasema, inawezekana ni madawa au kuhusu kauli za tundu lissu au masuala yake ya kibiashara au ni sababu anazozijua yeye sirro.
Maccm hoiiiiiiii
 
Hapo ndipo tunapata picha jinsi gani wafaidika na biashara ya unga walivyo na nguvu,lakini hawataweza kuitisha serikali
 
Jibu ni moja tu, hii vita ya madawa aliyoianzisha Makonda ni feki, wameanzia kwa wasanii, wakaja sijui kwa akina nani, lakini lengo lao kuu ni Mh. Mbowe.

Na huu ni mkakati maalum, usidhani Makonda aliamka tu asubuhi akaanzisha haya maigizo. Ni mkakati ambao ulisukwa kwa lengo la kudhoofisha upinzani wakilenga kumchafua Freeman Aikael Mbowe maana ni moja ya watu ambao ni tishio kwa chama dola. Na mkakati huu una baraka zote kutoka juu.

Na ndio maana hutasikia Makonda akiendelea kutaja tena majina maana mlengwa mkuu tayari ameshatajwa. Bahati mbaya mikakati yao huwa haifanikiwi, maana ni ya kishetani.
Mkuu umemaliza kila kitu
 
Unapokuwa safarini kwenye gari unatazama mwenendo wa gari ikitokea linakwenda ndivyo sivyo basi unamkagua dereva na leseni yake.
 
Majibu yenyewe kama ndiyo haya, basi mkoloni akiamua kurudi Barani Afrika ni rahisi sana kututawala tena!! Oh yes - we're disorganised lot mpaka tunasahau kabisa kuwa wamoja katika vita ya ku-save nguvu kazi ya Taifa letu dhidi ya madawa ya kulevya, badala yake mnakimbilia kumtetea MBOWE wakati hamjui alikuwa anaitwa Kituo cha Polisi kwa kosa gani? - masaa yote kutumbukiza siasa kwa kusingizia Serikali kwamba inakadamiza demokrasia na kudhoofisha upinzani Nchini, actually yeye kama Kiongozi wa upinzani alipashwa kuonyesha mfano bora kwa kuiitikia wito wa Polisi kuliko kubishana bishana nao, kwani walio itikia mwito wa Polisi kawazidi nini?
Wewe ndio unaongea irrelevance mkuu sio huyo unayemquote.... kwanza mbowe sio muuzaji wa madawa maana so far ushahidi hakuna so usiseme tunatetea MUUZA MADAWA.

Pili, MBOWE alikubali kutoa ushirkiano ila sio kwa mfumo ule aliotumia makonda whether gwajima or azzan walienda bado haifanyi ni halala sheria kuvunjwa...... yaani kwa kuwa magari yanatoa rushwa kwa traffic barabarani na mimi naye nitoe??? R u serious

Tatu, hoja ya serikali kukandamiza upinzani inaweza kuaminika maana iweje baada ya mbowe kutajwa na zoezi la kutajana likaishia hapo?? Huoni walijenga impression kuwa upinzani au CHADEMA ni chama cha wauza unga ili labda watanzania wasiwaamini tena??? Je kweli Mbowe wa chadema ndio kikwete alishindwa kumtaja katika ile list yake ya IKULU???

WAZO ZURI UTEKELEZAJI MBOVU
 
Kwanza inatakiwa uelewe kitu, toka hii vita imeanzishwa na Makonda ilikuwa haina tofauti na ile vita ya kushika madangulo ya makahaba na wale mashoga, wakati hii ya madawa ya kulevya haikuhitaji mfumo wa mapigano hayo.

Na ndio maana toka imeanza baadhi ya watu walipongeza ila waliponda approach aliyotumia bwana mdogo.

Sasa alikuja kuharibu zaidi kuita watu wenye uelewa na wajuvi wa sheria katika suala la kumuita mtuhumiwa na kumfanyia investigation, kitu ambacho kinatakiwa kiwe kisheria zaidi kuliko ki propaganda, kama alivyokuwa akifanya mwanzo.

Kwahiyo upekee wa Mbowe una kuja kwamba alikuwa anaelewa taratibu na sheria za kuitwa kwake kama mtuhumiwa, kitu ambacho hakikufuatwa, na zaidi ni kama alitaka kuwaweka sawa katika suala zima la approach ambavyo ilitakiwa kuwa.

Kama unakumbuka vizuri siku anaongea na waandishi wa habari aliwaambia ni nini hasa hawezi kwenda kutokana na mbinu illegal waliyotumia kumuita, japo alisema pia yupo tayari kutoa ushirikiano wa kutosha katika vita hii ya madawa ya kulevya.

Na hili pia lilichangia, mpaka kumwamsha Rais kutoka usingizini, mpaka kuhoji sheria husika ya kudhibiti madawa ya kulevya ilipokuwa imefichwa, ili iweze kutolewa na kufanya kazi.
Kilicho shangazi zaidi ni kuwa wahusika walikuwepo pale pale ila hawajijui kama walikuwa sehemu ya usimamizi wa hiyo sheria yenyewe. Sasa sijui kule Bungeni walikuwa wamelala kipindi inapitishwa?
Ndiyo oooooooo
 
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alipata kusema "Mwenye Ngoma baba sio mtoto".

Mbowe ndio baba wa Upinzani.

Na hata sisi tunajua hayo anayopitia ni haki yake, Kama ilivyokuwa haki kwa mitume kuteswa na kuuwawa.
Mungu akubariki mkuu
 
Mkuu nikusahihishe, aliyetajwa na makonda ni philemony mbowe, sijui kwanini freeman anahamaki?

Huyo mbunge wa hai anasakwa na kamanda sirro kwa sababu ambazo jeshi la polisi halijasema, inawezekana ni madawa au kuhusu kauli za tundu lissu au masuala yake ya kibiashara au ni sababu anazozijua yeye sirro.
Mjinga uliembali kabisa na matukio, umesahau RC alibadilisha jina na kusema ni mbunge wa hai tena Freeman Mbowe acha mahaba ya kitoto.
 
Nilikuwa namjibu mleta mada maswali aliyouliza, pili naombà nikujibu na wewe kuwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama haina maana usifuate sheria na taratibu katika kutekeleza majukumu yako. Kumbuka inapoishia haki yako kama kiongozi ndipo haki ya mwenzio inapoanzia. Na kwa mantiki hiyo makonda alishindwa kujua mipaka ya haki na wajibu wake kama mkuu wa mkoa na kwa hali hiyo akawa ameingilia haki za mtu mwingine. Kumbuka Tanzaniai ilisaini na ikaridhia tamko la kimataifa la haki za binadamu na ibara ya 30 ambayo ndiyo ibara ya mwisho inaweka ulinzi wa tamko hilo kuwa hakuna mwanachama yeyote atakayekuwa na mamlaka ya kubadili au kufanya marekebisho yoyote ktk tamko hilo. Hata sheria zetu za nchi pia zins hicho kitu.
Umeandika mengi lakini ni mihemko ile ile. Mbowe aliitwa central kama mkazi wa Dar sio kama mbunge au kiongozi wa chama cha upinzani bungeni.

Mmeumizwa na namna ambavyo heshima yake imechafuliwa, vipi kuhusu yale majina ya list of shame, wale wahusika hawakuumizwa na jinsi yalivyotamkwa hadharani?.

Mbowe ni mkazi wa Dar, na sio malaika pia, mbona Iddi Azzan na wale wamiliki wa mahoteli walikwenda central?.
 
Mkuu, Mbowe anaishi Mikocheni Dar. Makonda ni mkuu wa mkoa wa Dar, kwanini asiwe na mamlaka ya kumuita mkazi wake aende central police. Kina Iddi Azzan na wengine mbona walikwenda central na mambo yakaisha?.

Mzee Mtei ambaye ndiye mwanzilishi wa CDM kasema Mbowe ajitafakari hapa alipofikia, kwani kutajwa jina lake ni doa kwa chama ambacho yeye Mzee Mtei alikianzisha.

Tatizo ambalo ni la msingi ni baadhi ya wanasiasa kushindwa kubadilika kadri ya muda unavyokwenda. Siasa za kuvimbiana zilifanyika enzi zile za JK aliyeweza kumchekea yoyote yule aliye mbele ya macho yake. Awamu ya tano haivimbiwi kipuuzi tu.
Wewe na njaa yako ya kulazimisha uteuzi inakupeleka hovyo
 
Majibu yenyewe kama ndiyo haya, basi mkoloni akiamua kurudi Barani Afrika ni rahisi sana kututawala tena!! Oh yes - we're disorganised lot mpaka tunasahau kabisa kuwa wamoja katika vita ya ku-save nguvu kazi ya Taifa letu dhidi ya madawa ya kulevya, badala yake mnakimbilia kumtetea MBOWE wakati hamjui alikuwa anaitwa Kituo cha Polisi kwa kosa gani? - masaa yote kutumbukiza siasa kwa kusingizia Serikali kwamba inakadamiza demokrasia na kudhoofisha upinzani Nchini, actually yeye kama Kiongozi wa upinzani alipashwa kuonyesha mfano bora kwa kuiitikia wito wa Polisi kuliko kubishana bishana nao, kwani walio itikia mwito wa Polisi kawazidi nini?
Tuwachieni Mbowe wetu
 
Back
Top Bottom