Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Sina nia mbaya kukumbusha. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 'alianzisha' vita dhidi ya madawa ya kulevya mkoani Dar es Salaam na sasa vita hiyo imetapakaa Tanzania nzima. RC Makonda alikuwa akiongea kwa kujiamini, kutaja na kuagiza. Alikuwa akisubiriwa kwa hamu pale alipokuwa akitakiwa kutokeza na kuzungumza.
Siku alipotajwa Freeman Mbowe, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa pamoja na Manji na Gwajima, mambo yakabadilika. Kwanza, kila aliyetajwa hapo akazungumza na waandishi wa habari. Mbowe akaenda mbali zaidi na kutamka kuwa hatakwenda kuripoti Central Police kwakuwa aliyemwita (Makonda) hana mamlaka ya kumwita.
Baada ya tamko hilo la Mbowe, mambo yakachachamaa. Wakajitokeza watanzania kwa maelfu wanaomuunga mkono Mbowe na wale wanaompinga. Kilichofuata ni kuteuliwa kwa Kamishna Mkuu wa Kamisheni ya Kudhibiti na Kuzuia Madawa ya Kulevya nchini ambaye kimsingi ndiye sasa ameyachukua majukumu yake ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.
Kuanzia siku alipotajwa Mbowe wa CHADEMA vita ya madawa ya Makonda ikapata dhoruba kali kwa kumbadili kiongozi wa vita hiyo. Kuanzia siku alipotajwa Mbowe, hakujawahi kuwepo na kutajwa washukiwa wengine wa matumizi au kuingiza madawa ya kulevya. Siku aliyotajwa Mbowe wa CHADEMA ikawa ndiyo turning point.
Yawezekana kutajwa kwa Mbowe kukasababisha hata mashauri ya madai dhidi ya RC Makonda kuhusu udhalilishaji kama ambavyo Mbowe anapanga kuanza kufanya hivyo. Kimsingi, najiuliza, Mbowe wa CHADEMA ana upekee gani hadi 'kubadili' upepo wa mambo yote hayo?