Mbowe vs Ndugai live on TBC1

Mbowe vs Ndugai live on TBC1

nalaani huu ukiukwaji wakanunu kwa njia za kinyemela lakini kama chama makini ha2shndwi na jambo..
 
Hawa jamaa wameisha vuruga mambo mengi kwa kipindi cha siku moja tu wakitumia wingi wao bungeni. Wanakejeli, wanatukana, wanatuona Watanzania wote ni vilaza hatuwezi kutafasili maana ya wanayo yafanya. Uzuri wake wajumbe wetu ingawa ni wachache watazidi kutoa changa moto bila kukubali uozo unaofanywa na hao mafisadi. Hili bunge inaonyesha litakuwa ruber stamp ya SISIEM pomoja na spika wao.

Kweli kabisa mkuu,Hawa wanasiasa uchwara wanadhani wanapambana na cdm tu na wanafikiri wananchi wanafikiri hivyo kuwa ni siasa tu na wanataka kuaminisha umma kuwa yanayoendelea ni maslahi ya wanasiasa tu na si mwamko wa wananchi na kuna kama taswira fulani inataka kujengwa juu ya siasa ili wananchi wapuuzie wasemayo wana siasa.Mambo mengi ambayo cdm wameyafanya yakawa na mwamko kwa umma wanataka eti tuachie umma uamue (sijui kwa njia ipi bila kuchakachuliwa) ili mradi cdm wakae pembeni then tupite watakapo na hapo kumbuka serikali ni yao! mfumo utawapa zaidi fursa fulani fulani ndio maana wanaanzia bungeni kutengeneza taswira na mtizamo fulani kwa cdm.makamanda wa cdm nyinyi ndio front solder wetu piganeni hadi mwisho ipo siku wananchi wengi wataelewa tu.
 
:coffee:ndugu yaangu, chadema kuunda kambi haimaanishi kwamba wanapewa haki ya kuongoza kamati muhimu ndani ya bunge. CCM na vyama vingine vya upinzani wanataka tafsiri ile ya kambi rasmi ambayo kimsingi jana wameibadilisha inawaruhusu wao pamoja na kuwa Chadema itaongoza kambi ya upinzani, maamuzi muhimu katika zile kamati za fedha yasiamliwe na chadema. Kwani kamati hizo zitakuwa zimepenyezewa mamluki wa CCM na wale Cuf ambao kwa sasa ni ccm pia kwa sababu wanaunda serikali? Unapozungumzia CUF leo hii unaitofautishaje na CCM iwapo wote wanaunda serikali?
 
Huu muungano wanaoulazimisha sasa hivi hauna maana... kwa sababu nakumbuka kuna vyama vilijitoa kugombea uraisi 2010 na wakasema wafuasi wao kura za uraisi wampe kikwete.. Bunge la sasa hivi linaendeshwa kitaarabu/kimipasho!!! Mijitu mizima inazomea kama waimba taarabu.. na kiongozi wao akiwa hadija kopa(makinda) ndivyo ninavyolifananisha.....Kuna siku nitageuka undertaker niwavamie wote CCM na vibaraka vyao niwapigishe vichwa chini halafu wakija kuamka wawe na adabu..
 
Ukiangalia lengo la CCM hapa ni kutumia hizo kamati za bunge kama hongo kwa wabunge wa vyama vya Upinzani ili kuweza kuwanyamazisha na kuua nguvu ya upinzania bungeni.
Na kwa sasa ni kuwakomoa CDM kwa sababu wao hawatapewa hizo nafasi na kuweza kuibua uozo kwenye mashirika na taasisi zinazosimamiwa na kamati hizo.


Ni move ya kupingwa ingawa watu wanaweza wasiione kwa sasa, huu ni usindi kwa CCM kwa kufanikiwa kubadili hiyo tafsiri.
 
.....Kuna siku nitageuka undertaker niwavamie wote CCM na vibaraka vyao niwapigishe vichwa chini halafu wakija kuamka wawe na adabu..

Ungekuwa mbunge ingebidi tukuandalie haraka pambano la masumbwi na yule Mbunge wa Mtera.
 
Naona CCM wanaweweseka sana this time wanafanya kila liwezekanalo kuwadhoofisha CDM

CCM wanadhani wanawakomoa CDM, kumbe ndo wameanza kutengeneza njia kwa mwaka 2015. Hongera CDM, tupo nyuma yenu.
 
Sasa mbona naskia Cheyo ameshachaguliwa kuwa mwenyekiti wa PAC, hii nayo inakuwaje?
 
hili suala linakuzwa sana, mimi sioni kama kuna ukandamizaji ni vizuri wapinzani wapewe haki sawa katika kupambana na chama tawala.
ikitokea kuna mpinzani anapendelea CCM basi iwekwe wazi na atengwe kutokana na ushahidi huo na si kulaumu kwa hisia.
sasa hivi ni kutafuta njia ya kujenga spirit ya ushirikiano na si kushabikia utengano

kwa mnao kumbuka hotuba ya Nyerere RIP alisema mtu/chama anayelilia utengano ni hatali kwani mwisho wake baada ya utengano si mzuri. CDM watakuja kuona si wamoja (mf. wazee kwa vijana - dalili zipo) watatofautiana na tatizo litaendelea
 
Chadema, hayo mazumbukuku kama yanang'ang'ania huto tuvyeo twao twa kijinga jinga, WAPENI! Msipoteze nguvu zenu bure. Nyinyi mkiwa na jambo muhimu hasa la kutuambia tumieni njia yetu ile ile ya siku zote....MWEMBE YANGA! Ndio kiboko yao. halafu sisi wanachi ndio tutafanya maamuzi. Inaweza ikachukua miaka lakini hatimaye nguvu ya wananchi ITASHINDAA....!!
 
Sijui Kama ni CCM kubanwa; ispokuwa kwa mtu makini atajiuliza maswali yafuatayo.

1. Siku zote Bunge husema kwamba linaheshimu mihimili mingine ya dola ikiwemo mahakama na hata hoja ya Dowans imetupiliwa mbali kwa sababu kesi iko mahakamani. Kazi ya mahakama ni kutafisri sheria zilizotungwa au zitakazotungwa na bunge baada ya miswaada/ bills kutoka serikalini kupelekwa huko kujadiliwa.
Swali: Tangu lini Bunge likawa ni sehemu ya kutunga sheria, kanuni na taratibu na pia likawa ni sehemu ya kuzitafsiri sheria hizo, kanuni hizo, na taratibu hizo... ? Mbona hapa linaingilia kazi ya kutafsiri wakati kazi hii ni kazi ya mahakama...?

2. Nani aliwaambia wabunge wa CCM kwamba CDM inahitaji msaada wa kulahisisha utafisilishaji wa kanuni hiyo iliyofanyiwa marekebisho?

3. Ni nini maana ya kuwa na serikali kivuri/opposition government kama sio wao wapinzani wenyewe kujiamulia mambo kwa mujibu wa kanuni zilizowekwa na zilizokuwa zinajulikana kabla hata ya bunge hili la 10?

4. Kuna haja gani kanuni hiyo kuhitaji tafisili mpya tofauti na ile iliyokubalika ktk mabunge likiwemo lile la 9 kama sio mbinu chafu za kuudhofisha upinzani hasa unaounda serikali kivuli? Hii pia inaonesha kwamba wabunge wa ccm hawana uwezo wa kupambanua mambo ndo maana wanakimbilia matusi na utani ambao watu kama vijana na watoto hawategemi kuoneshwa na waheshimiwa

5. Ni kwa nini tafsiri hiyo mpya isiwe effective katika bunge la 11 na na iwe effective sasa?

6. Wabunge hao wanaozomeazomea CDM watajisikia vipi kama na wao siku moja wakiwa kwenye receiving end kama mambo haya hayatarekebishwa?

7. Na hao Zomea zomea wanataka kutoa taswira gani ya nchi yetu, wapiga kura wao na heshima yao wanayopewa kwa kuitwa waheshimwa kama hawana tofauti na watu wa vijiweni? na hao wanasema kwamba watu watwangane makonde...? hivi siku hizi tumekuwa kuku au jogoo wa kupigana bila mpango?

8. Ushauri: CDM endeleeni kue-exercise democracy with inteligence and intergrity nasi tutawasaidia kueleza ndugu zetu jinsi CCM inavyotaka kuwabuluzeni NA CCM NYIE endelezeni Ukihiyo wane kwa zomeazomea hata bila kujua ni nini kinacholalamikiwa...ipo siku mambo yatawageukia na kulamba matapishi yenu...

CCM wanasahau kuwa the same person ambaye ndiye key ya hii discussion leo ya kuleta tafsiri ambayo haikutumika hapo alipo weka mkazo wa 'kambi rasmi' na pengine tafsiri ya wakati ule ndo amekuwa victim of his own verdict....Sasa kama this is not a good lesson to them basi wasubiri siku ambayo they would be kambi ya upinzani rasmi na pengine wasiwe na power ya kuweka wenyeviti kwenye hizo same positions ambazo leo CDM wanazitaka ili waweze kuwa effective kambi rasmi Bungeni ...na kwao wakati huo that and that only would be the only hope ya kuonyesha uwezo wao ili pengine voters waweze kurudisha imani baada ya kuipoteza na ku loose election na hivyo ili kuwa rudisha into power....What is the the importance of Histroty? Swali la form two......

The word of God makes me wise even when am foolish......Ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga CCM wait for the history ndo mta kuwa humbled by the grace!

You have made me hate you! Its a sin I know but may be the holly sin for this also affects the well being of the poor rural community.......

Inaonekana mnaenda kwa ideology ya 'we will cross the bridge when we reach....okay continue!
 
WABUNGE WACHADEMA WATAANZA LINI KUTUMIA AKILI ZAO ? Mbowe anaamua kila kitu maana yake nini ? chadema siyo chama cha Kilimanjaro ni cha watanzania wote ! imefika wakati sasa Mbowe asituongoze kwa kila jambo ! Kamwe kutoka nje ya Bunge hakutatusaidia kamwe ! Chadema siyo wa kwanza kwa utaratibu huu wa kipuuzi ! umekuwepo kwa miaka kadhaa ! Ni sawa na mtoto wako anapogoma kula chakula then baada ya siku moja anakuja anaomba chakula baada ya uvumilivu kumshinda.

CHADEMA NI CHAMA CHA WATANZANIA WOTE ! SUGU ANAJUA SABABU YA KUTOKA NJE ?
 
hebu nielezeni kidogo hapa! !sasa chadema walitoka bungeni kwa hoja ipi kama leo inasemwa ni ruksa kwako kuunda kambi ya upinzani Bungeni??

Kabla ya mabadiliko ya tafsiri ya kambi ya upinzani Bungeni ilikuwa Wenyeviti wa kamati za POC, LAC na PAC wote watoke CHADEMA kama chama kikuuu cha upinzani. Mabadiliko hayo yameruhusu wabunge wa vyama vingine nao kuwa na haki ya kugombea
 
WABUNGE WACHADEMA WATAANZA LINI KUTUMIA AKILI ZAO ? Mbowe anaamua kila kitu maana yake nini ? chadema siyo chama cha Kilimanjaro ni cha watanzania wote ! imefika wakati sasa Mbowe asituongoze kwa kila jambo ! Kamwe kutoka nje ya Bunge hakutatusaidia kamwe ! Chadema siyo wa kwanza kwa utaratibu huu wa kipuuzi ! umekuwepo kwa miaka kadhaa ! Ni sawa na mtoto wako anapogoma kula chakula then baada ya siku moja anakuja anaomba chakula baada ya uvumilivu kumshinda.

CHADEMA NI CHAMA CHA WATANZANIA WOTE ! SUGU ANAJUA SABABU YA KUTOKA NJE ?

Mara ngapi wapinzani wamegomea bajeti kwa kutoka nje chini ya uenyekiti wa Mh. Hamad? Ile ni kuonyesha kutokubaliane na jambo linalopigiwa kura kwa 100%
 
Kwa wote wasioelewa kilichofanyika kama ndugu Katavi ni kwamba chamba rasmi cha upinzani (CHADEMA) kimeondolewa haki ya kuongoza kamati muhimu tatu zinazo husiana na matumizi ya mapesa yetu siye wananch, badala yake CCM wamejipa kura ya veto kwa uwingi wao kumchagua wanaye mtaka wao hataka kutoka chama chochote kingine cha upinzani imaradi jina lake likiwemo katika wagombea. Hapo awali chama rasmi pinzani kilikuwa na haki ya kupendekeza jina mbunge wake na kupigiwa kura na wabunge wote likiwa peka yake.

Swala la kuunda baraza kivuli la mawaziri halija badirishwa bali uamuzi wa kuwashirikisha wabunge wa vyama vingine vya upinzani umebaki kwa chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kwa sasa.

kama kuna mtu bado hajaelewa basi arudi darasani kuongeza ufahamu wa kuelewa.
 
MZAHA WA CUF KUWA 'CHAMA TAWALA' NA 'CHAMA CHA UPINZANI' KWA WAKATI MMOJA KWA KIPINDI KILE KILE NDANI YA TAIFA MOJA!!!




22.JPG

525 × 700 - David Kafulila, Kigoma Kusini. Mkutano

Ni gharama kubwa sana kwetu sisi wapigakura kuchagua baadhi ya vijana wasiokua na msimamo thabiti kwenda bungeni kutuwakilisha.

Nilimtaza huyu Ndugu Kafulila kwa uchungu mkubwa sana jinsi alivyokua anaongea bungeni kutaka kulazimisha ndoa ya kisiasa kati ya CHADEMA na CUF wakati anafahamu fika kwamba CUF ni chama tawala ndani ya mipaka yetu hii ya Tanzania kwa mujibu wa mwafaka wake na CCM.

Mtu asitfute njia ya mkato wa kutafuta CHADEMA kusaidia kusafisha uchafu wa utawal wa kisheria na kidemokrsia kama ambavyo CCM na CUF walivyojisababishia kwa MWAFAKA WA MAKAMBA kule Visiwani na sasa Mwafaka huo ulivyowaletea mikanganyiko ndani ya bunge la Muungano na hata kutishia kuvunja muungano wetu misingi ya kisheria itakapolazimika kuzingatiwa.

Kwa mtaji wa kitendo tu cha bunge letu tukufu kule Dodoma ITAKAPOSHAWISHIKA KULAZIMISHA KUBADILISHWA KWA KANUNI YA BUNGE inayozungumzia sifa na muundo wa chama rasmi cha Upinzani bungeni basi moja kwa moja tangu hapo tujue kwamba taifa letu litakua limeingia moja kwa moja KATIKA MGOGORO WA KIKATIBA ambayo matokea yake huenda yasipendeze sana kwa wengi wwetu.

Hakika mara baada ya CCM kulazimisha ndoa kati ya CUF na CHADEMA huku bara wakati wakijua kwamba kula Zanzibar ndoa ni kati ya CUF na CCM basi naona kuna uwezekano mkubwa wa WA KUZUKA KWA MISURURU YA KESI JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA NA KUHITAJIKA KWEPO KWA MAHAKAMA YA KIKATIBA NCHINI AU WATU NA VIKUNDI VISIVYOAFIKI HIYO HALI KULAZIMIKA KWENDA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KUTAFUTA HAKI ILI KUNUSURU MUUNGANO WETU TANZANIA.

Mhe Kafulila, ulichukua angalau muda wako kuyafikiria haya kabla ya kuanza na mazungumzo yako kule bungeni???????????? Jamani tusipende kuleta majibu rahisi sana kwa swala ngumu kama hili.

Mwafaka wa Zanzibar ulikua na nia nzuri kwa kutulete utulivu kule visiwani lakini kwa kuwa wahusika huenda walikosa ushauri mzuri kisheria na matokeo ya utekelezaji wa mwafaka wenyewe ndani ya muungano wetu hasa kwa vyama vingine ambavyo havikuhushishwa kwenye mwafaka huo ndio leo hii imetufikisha hapa.

Nakumbuka sana Mhe James Mbatia alilipigia sana kelele wakati ule akitaka vyama vyote vya upinzani vihusishwa lakini kwa bahati maya sana hakusikilizwa na CCM. Inamaana Mbatia hakumpa briefing mbunge wake Kafulila juu ya ukwel huo???

Kwa mantiki hii hata mtu akilazimisha kubadilisha kanuni za mchezo bungeni wakati timu tayari ziko uwanjani tayari kucheza, jamba ambalo kwanza si la kawaida na ni ukiukwaji mkubwa wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi ndani ya himaya ya nchi za jumuiya ya madola, pamoja na yote CUF bado haingii kisheria ndani ya kambi ya upinzani mpaka kwanza ama:

(1) CUF kijivue kutoka ndani ya mwafaka na CCM kule visiwani.

(2) au Serikali itangaze wazi kwamba kwa mwafaka wa CCM na CUF basi tayari walishavunja Muungano wetu na Zanzibar ili Watanzania tujue kabisaa kwamba kumbe mpaka sasa hatuna muungano ndipo CUF ipate kukubalika Bara kama chama cha upinzani bila kutupa jicho kwamba kule Visiwani chama hiki kimekaeje bungeni huko.

(3) Na kama hoja namba mbili ndio ukweli wa mambo ulivyo nchini mwetu basi kabla CUF haijavuka sakafu la bunge letu la muungano kule Dodoma kuja upande wa upinzani, kwa maana ya kwamba yanayoendelea bunge la Zanzibar sasa ionekane kana kwamba haituhusu huku Bara, basi kwanza ni sharti wabunge wote wa Zanzibar waondoke bungeni hapo bila kujali chama kilichomleta hapo bungeni.

Watanzania tuliowengi sana hatupendi hata kidogo tunu letu 'Muungano' kuvunjwa na mtu yeyote lakini mantiki hoja yenyewe inatuelekeza hivyo kwamba CUF kuingia kambi ya upinzani huku bara basi maana yake Muungano ulishavunja na wabunge wote kutoka Visiwani ni sharti waondoke bungeni Dodoma.
 
Usingizi huwa ni faraja kwa walio na huzuni,na hii ndo hali inayowastahili hao wabunge wa Cuf,TLP na UDP. Maana wanahuzuni yakukosa viti vingi katika uchaguzi mkuu 2010, wamelala wamejisahau hayo wanayofanya ni ndoto wamelala ila wakijakushituka watashangaa maana hawatakuwa napakushika unadhani CCM watawapenda au kuwalipa fadhila hawajui wanadhoofishwa bila kujijua wakidanganywa ni warembo kwa ndoa za vichochoron mwisho wa safari wataitwa malaya.
Chadema mnaujua mchezo huu nawao CCM ni mabingwa wa michezo michafu chezeni nao hivyo mwisho wataaibika wenyewe.
Wanadhani yai likichafuka nje na kifaranga kilichoko ndani kitachafuka. Sheria,kanuni zipo wanataka kupindisha wanadhani hii ni ile dunia ya babu zetu.
The Public power is all we stand through. Chura na kobe hawawezi kuzaa iweje wawachanganye? Kwanza CUF NI WANAFIKI PAPA utakuaje mtawala alafu hapohapo unajiwekea upinzani mwenyewe?
 
Back
Top Bottom