kichwamaji
JF-Expert Member
- Dec 1, 2006
- 232
- 13
MBOWE NI KAMA MREMA WOTE NI MADIKTETA
Mtikisiko unaokikumba chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), ni kielelezo cha kwanza kufumuka hadharani kuhusiana na udikteta alionao mwenyekiti wake Freeman Mbowe
Hatua ya kusimamishwa uongozi kwa makamu mwenyekiti wa chama hicho, Chacha Wangwe ni jambo lililokuwa likitazamiwa tangu siku nyingi kutokana na tabia ya mbowe kutotofautiana na ile ya mwenyekiti wa taifa wa TLP, Augustine Mrema ambapo wote ni madikteta.
Kama alivyo mrema, Mbwe naye anataka kuiongoza Chadema kwa misingi ileile ya kidikteta ya kutotaka changamoto inayokinzana na mawazo yake hata kama anayetoa mwelekeo tofauti atakuwa anafanya hivyo kwa ajili ya maslahi ya chama.
Kelele za chini kwa chini zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema kuhusu ruzuku inavyotafunwa kwa fujo na "vigogo" wa chama hicho makao makuu wakiongozwa na Mbowe, hazikuwa za siri kama anavyofikiri.
Kilichokuwa kinapungua ni nani angesimama hadharani na kuusema uoza huo wa siku nyingi.
Mbowe na kikundi chake chenye watu kama Dk. Wilbroad Slaa, Zitto Kabwe, John Mnyika, Anthony Komu na marafiki wengine wachache ndio waliokuwa wakitumia kisingizio cha kulipana madeni, kulipia gharama za helikopta na kadhlika, kujitwalia mamilioni ya ruzuku huku ngazi za chini kuanzia mikoa, wilayani, kata na matawini kukiwa hakupelekwi hata senti tano.
Tunamshukuru Chacha Wangwe kwa kutokuwa mnafiki, kiongozi ambaye msimamo wake wa kutaka fedha za ruzuku zipelekwe wilayani unaungwa mkono na kila mwenye mapenzi mema na chama chake.
Uongo wa mbowe na kamati kuu iliyohongwa unaodai eti Wngwe anatoa siri za chama anaandaa, kufadhili na kushiriki vikao vya kukihujumu chama hicho hauwezi kuaminika popote isipokuwa pale ambapo pamejaa fitina, viyisho na uzandiki.
Wanachama wa Chadema wanafahamu wanavyohangaika kutafuta fedha za kulipia ofisi matawi ni, kata, wilayani na mikoani huku milioni 66 za ruzuku inayotolewa na serikali kila mwezi zikiishia mifukoni mwa Mbowe na viongozi wenzake wa makao makuu wasiokuwa na nia njema kwa chama.
Wangwe aliyeanza kupigwa vita tokea mapema wakati akigombea umakamu mwenyekiti mapema mwaka huu ndiye shujaa wa chama kutokana na msimamo wake wa kutetea haki na demokrasia.
Waliokuwa hawaujui udikteta wa Mbowe na unafiki wa viongozi kama Slaa, Zitto na Mnyika waanze sasa kutambua ukweli.
Lazima wanachama na viongozi wa Chadema waliopo ngazi za mikoa, wilaya, kata na matawi washikamane kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha kuwa "wanakufa" na Wangwe.
Huyo ndiye shujaa na mkombozi wa kweli wa jasho lao walilotoa mwaka 2005 na kukiwezesha chama hicho kupata ruzuku ya shilingi milioni 66 kila mwezi hivi sasa.
Aluta continua
Huu ujanja wenu kawapelekee wajinga wenzenu. Historia imeshatufunza mengi, na sasa tunajua mnakotaka kuelekeza mawazo ya Watanzania. Hakika mtaendelea kujiuma na kuumana, hamtafanikiwa kuwadhoofisha wapiganaji na wanaharakati wote. Tutaendelea kupambana na ufisadi wenu CCM hata kama mtajivika makoti ya wengine na kutumia pesa hizo kuvuruga wananchi. Katika hili, mmenoa. Hebu tafuteni mkakati mpya!