Mbowe: TAKUKURU ivunjwe!

Mbowe: TAKUKURU ivunjwe!

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,628
Reaction score
6,818
Mwandishi wa Mwananchi, Hanang’ | Novemba 14, 2012


MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amependekeza kuvunjwa kwa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwani badala yake kupambananayo inaipalilia.

Akifungua tawi ya Chadema Kata za Katesh linalopakana na ofisi za Takukuru Wilaya ya Hanang, Mkoa wa Manyara juzi, Mbowe alisema taasisi hiyo imeshindwa kazi.

Mbowe alisema Takukuru imeshindwa kudhibiti hata rushwa ya wazi ndani ya CCM kwenye chaguzi ambazo zilifanyika hivi karibuni.

“Hakuna ambaye hakujua rushwa ndani na CCM na jinsi ambavyo imeathiri chama hicho, lakini Takukuru wameshindwa kupambana na rushwa hiyo badala yake wanailea,” alisema Mbowe.

Alisema Rais Jakaya Kikwete ambaye anasimamia Takukuru iliyopo kwenye wizara yake, ameshindwa kuibana ndiyo sababu hata yeye amekuwa akilalamika.

Pia, Mbowe alifungua matawi kata za Endasaki na Ganana, alisema kutokana na Takukuru kushindwa kupambana na rushwa, isipovunjwa chama hicho kikiingia madarakani kitawatimua watendaji wote wa taasisi hiyo ili wafanye kazi nyingine.

Alisema Takukuru imeshindwa hata kusaidia kurejesha mabilioni ya fedha za Watanzania ambayo yamefishwa nchini Uswis.

“Hawa Takukuru walipaswa kuanza kufanya uchunguzi juu ya fedha hizo baada ya kupata taarifa na kusaidia taifa kuzipata, lakini wamekaa kimya,” alisema Mbowe.

Alisema kutokana na ukimya huo, ndiyo sababu Chadema kupitia Naibu Katibu Mkuu wake, Kabwe Zitto waliomba serikali kufanya uchunguzi na kutoa taarifa bungeni juu ya walioficha fedha na utaratibu wa kuzirejesha.

“Bunge lijalo, kama wasipoleta taarifa ya maana juu ya fedha za Uswis tunajua la kufanya, nadhani mmeona jinsi hoja hii ilivyoungwa mkono na watu wengi,”alisema Mbowe.

Awali, Mbowe alizitaka ofisi hizo za Chadema, alizofungua kuwa kimbilio la wanyonge kutoa kero zao na kusaidiwa badala ya kuwa maeneo ya kukaa viongozi pekee.
 
SAWA KUJUNJWA kwake . lakini kuvunjwa kwake kuwe ni kuingiza chombo kama TAKURu katika katiba na ambacho kitakuwa huru. Mkurugenzi wake apigiwe kura bungeni. Raisi atoe jina na upinzani utoe jina
 
SAWA KUJUNJWA kwake . lakini kuvunjwa kwake kuwe ni kuingiza chombo kama TAKURu katika katiba na ambacho kitakuwa huru. Mkurugenzi wake apigiwe kura bungeni. Raisi atoe jina na upinzani utoe jina
Mkuu, uko sawa.
Watu wote wanaowajibika kwa rais huyu wa sasa walishagundua kuwa hawezi kuwaadhibu kwa kosa lolote lile.
Hata akiombwa na wanananchi hawezi kuwajibisha mtu.
 
hawa jamaa wana jengo zuriii pale upanga, wana servailance camera kama ubalozi wa marekani vile, ndani ni ofisi bora karibia kuliko zote hapa bongo, lakini utendaji wake ni mbofumbofu kabisa. hata kuendesha kesi hawawezi, wanategemea wanasheria toka ofisi ya DPP waungane nao, kwasababu wao ni ma pp kama pp wa kipolisi tu pale mahakama za wilaya, hawana ujuzi, hawasomi kesi, nadhani nii mzigo hata kwa wanasheria wa serikali ambao wanaungana nao kuendesha kesi. wana kiburii, mishahara minonooo, lakini bado wanapokea rushwa. wanaendesha magari hakuna fara pale....ofisi ile ni ofisi ya kula hela tu haina lolote.
 
Kwanini asilete mswada wa mabadiliko ya sheria ya TAKUKURU Bungeni ili kuipa hiyo taasisi meno zaidi?
 
yani ukiwa na baba kama hosea mtaani ni aibu jinsi jk anavyomtikisa kama mdoli
 
Kwanini asilete mswada wa mabadiliko ya sheria ya TAKUKURU Bungeni ili kuipa hiyo taasisi meno zaidi?.......

Mkuu unamaanisha isiwe chini ya ofisi ya rais?au na uteuzi wa mkurugenzi wake uliofanywa na rais utenguliwe?kama ni mteule wa rais ataendelea kuwa puppet.
 
Kamanda hapo umeongea point naunga mkono hoja
 
mkuu unamaanisha isiwe chini ya ofisi ya rais?au na uteuzi wa mkurugenzi wake uliofanywa na rais utenguliwe?kama ni mteule wa rais ataendelea kuwa puppet.....

Sijui kwa kweli maana kama anataka ivunjwe bila ya shaka ana mawazo anayotaka kuiona TAKUKURU iwe.
 
Kwanini asilete mswada wa mabadiliko ya sheria ya TAKUKURU Bungeni ili kuipa hiyo taasisi meno zaidi?.......

Hata wakipewa meno haitasaidia sana kwani watatafuna na kumeza kujaza matumbo yao. Cha muhimu ni kuweka misingi ya uadilifu, vinginevyo hakuna kitu.
 
Takukuru ivunjwe haraka kama ilivyokuwa kwa scorpion ya south africa.
 
Wa kuvunja hiyo sijui takukuru yuko wapi?
 
Tatizo ni kwamba wanaopaswa kuivunja, hawawezi kuishi bila ya rushwa. Takukukuru ni Taasisi ya Ki-jingaa kabisa. Nikikumbuka Nchambi alivyowatumia maafisa wa Takukuru kugawa hela kwenye chaguzi za kura za maoni za Magamba! Sina hamu nayo. Si kwamba ivunjwe tu bali viongozi wake wawekwe ndani na kufikishwa mahakamani ili kutenda haki kwa walivyoinajisi kodi ya Wananchi.
 
Wakanada 5 hayo mashamba yalikuwa mfano kuigwa Afrika. Watanzania 5000, mashamba yakafa na yakajaa panya wa ajabu.

Leo mnayataka tena baada ya kuona wawekezaji wanayafufuwa tena!

Laana tuliyopigwa si ndogo.
 
Takukuru ivunjwe haraka kama ilivyokuwa kwa scorpion ya south africa.

Wakuivunja nani na ili iweje? Hilo dudu linawasidia sna Watawala kwenye maigizo yao ya kupambana na rushwa ili kupata sifa kwa Wafadhili kuwa wanapambana na ufisadi.
Mwaka 2015, CCM wakishinda, Rais ajaye ataibadilisha jina. Mkapa alianza na PCB, Kikwete akaja na PCCB, 2015 itakuwa PCCBB!
 
Mbowe amajuwa hao hawataishia Uswisi, itabidi wapite Uingereza na Dubai. Hapo sasa!
 
Kweli mkuu. Yenyewe tu ni "Ofisi ya Rais" iko chini ya Ikulu, DG huchaguliwa ra Rais mwenyewe....Kazi iko!!.
Wakuivunja nani na ili iweje? Hilo dudu linawasidia sna Watawala kwenye maigizo yao ya kupambana na rushwa ili kupata sifa kwa Wafadhili kuwa wanapambana na ufisadi.
Mwaka 2015, CCM wakishinda, Rais ajaye ataibadilisha jina. Mkapa alianza na PCB, Kikwete akaja na PCCB, 2015 itakuwa PCCBB!
 
Takukuru ni kituko mbunge mmoja juzi alisema eti kwenye kipindi cha kampeini ukiwapigia simu kuwa kuna mgombea anagawa rushwa mahali fulani kabla yakufika kwenye tukio wanampigia simu mtoa rushwa kuwa wanakuja kwa hiyo asitishe zoezi la kutoa rushwa kabla hawajafika! hayo ndiyo maajabu ya Takukuru.
 
Mbowe amajuwa hao hawataishia Uswisi, itabidi wapite Uingereza na Dubai. Hapo sasa!

Kumbe kwa mzunguko huo bilioni zetu sisi ( Mimi na Zomba) zitapona. Maana sisi tuliweka visiwani, kule alikoweka AC vijishilingi vyake !
 
Back
Top Bottom