Mbowe: Sikumtangaza Dr. Slaa mgombea urais 2015

Mbowe: Sikumtangaza Dr. Slaa mgombea urais 2015

hakuna makundi ila kuna tofauti ya mitizamo maana yake ni nini?????
 
Mtela Mwampamba facebook page 10:34am Jan 3

Ulisema slaa anatosha urais 2015 leo unasema umelishwa maneno lakini unaendelea kubaka demokrasia eti utahakikisha unasimamia kumpata mgombea urais 2015 ukiwa mwenyekiti kana kwamba unahati miliki ya uenyekiti! Hivi hizi nguvu za uungu watu zinatoka wapi yaani mtu unakuwa na uhakika wa kuhodhi uenyekiti ndani ya chama cha demokrasia!
 
Tanzania Daima sio gazeti lenye kuaminika.

Sisi tunaamini yale yaliyonukuliwa na Mwananchi kuwa "MBOWE KASEMA NI DR SLAA 2015" na mmiliki wa NGO mzee mtei akamalizia kuwa vikao vimeshaamua full stop na "wachumia tumbo" wengine kama lema na heche wakaweka wazi maamuzi ya ukoo.
 
Mimi mwenyewe nilikuwa mbulu mbowe hakusema silaa ndiye mgombea nilishangaa sana kesho yake kusoma mwananchi kichwa cha habari mbowe amtangaza silaa kugombea uraisi 2015.mwananchi nao wameungana na uhuru.habari leo mtanzania na jambo leo kushambulia chadema.
 
Jamani wanabodi heshima mbele wakuu...

Nimekuwa ninafuatilia kwa makini Gazeti la Mwananchi na suala zima la mgombea urais kwa kupitia mgongo wa CHADEMA 2015, kwa kweli hawa jamaa wameifanya kuwa ndiyo ishu ya kuwafanya wauze magazeti yao, na kulivalia njuga suala hilo kama hawana akili nzuri!!

Tido Mhando ulipokuwa TBC 1 kuna wakati uliwatibua akili wasomi wa Tanzania hasa hasa wapenda mabadiliko, jinsi ulivyokuwa unakiendesha chombo hicho tofauti na ulivyokuwa unafanya kazi zako ukiwa BBC kwa weledi mkubwa!! Wadau walikupigia "kelele" mpaka ukabadilika na sasa umeanza tena kuruhusu gazeti lako kupoteza "neutrality" na kukomalia ishu ya Mgombea kupitia CHADEMA, hivi habari kama hizo toka CCM, NCCR MAGEUZI, CUF nk mbona huzipi coverage? Whats so special with CHADEMA? Tido angalia kuna kundi la wasomi linaelewa nini kinaendelea kupitia gazeti lako...!!
 

Attachments

  • mtei_kabwe.jpg
    mtei_kabwe.jpg
    23.7 KB · Views: 56
Kwani ww haupo????, Hongereni sana maana ndicho mlichokuwa mnatafuta. poor mwananchi newspaper & all those behind the scene.

Wana CHADEMA msiwe kama CHADOMO wekeni hiyo video ya mkuano wa Mbowe hapa tuone kama amelishwa maneno au anataka kutudanya. Mbona issue ni ndogo tu. Tatizo liko wapi hamku record mkutano wa Karatu? Hiki chama kina watu makini kwa upande mmoja ambao ni watazamaji na waanzilishi Mbowe na Mkwewe kwa upande mwingine wako kwenye driving seat! Wakisema, wana CHADEMA wote, hewala bwana! CHADEMA needs major overhaul ya kiuongozi kupata taasisi ya kisiasa badala ya NGO.
 
Mimi mwenyewe nilikuwa mbulu mbowe hakusema silaa ndiye mgombea nilishangaa sana kesho yake kusoma mwananchi kichwa cha habari mbowe amtangaza silaa kugombea uraisi 2015.mwananchi nao wameungana na uhuru.habari leo mtanzania na jambo leo kushambulia chadema.

Upload hiyo video ya mkutano weka humu uwaumbue masalia. Tatizo ni nini? Mnyika si yupo au hakurecord mkutano?
 
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema baadhi ya vyombo vya habari vimemlisha maneno, na hivyo kupotosha kauli yake aliyoitoa katika mkutano wa hadhara jimboni Karatu hivi karibuni.



Chanzo: Tanzania Daima

Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.
 
Mwananchi si lakuaminika tena Tido keshalirudisha Magambani Ccm hoyeeeeeeeeee
 
taarifa kama hii ilitakiwa iandikwe na magazeti yasiyo na mrengo wa chama flani mfano tanzania daima...ingeeleweka kwa wananchi lakini hivi sasa inazidisha maswali kwamba mh.menyekiti hana msimamo
 
Mkuu, gazeti la mwanachi waliamua kupotosha hiyo habari kwa sababu zao.

Ndio maana wengi wetu hum Jf tulihoji utofauti wa hiyo habari kati ya mwananchi na Tanzania daima.

Wengi wenu hamkuhoji uhalali wa habari, ila mlimsupport mwenyekiti; Mbowe kwamba ana vision! Rejea ile thread, JF huwa hawafuti. Msiwe Mandumilakuwili. Jee na hii ya Mtei ya mwananchi ya leo vipi, imechakachuliwa?
 
one of my senior lecturer alinifundisha kitu inaitwa Dictatorship democracy....and here it is
 
Naona wenye chama (mtu na mkwe) wameshafanya maamuzi siku nyingi wengine subiri siku ya kura mtekeleze maamuzi yao.

We gamba MJIMPYA, kwa hizi kauli zako utapata aibu siku si nyingi. Wenye CHADEMA ni sisi Watanzania tulioamka. CCM mmeshachokwa na more than 60% ya watanzania. Hamna jipya, hata mtoe propaganda ipi. Ninyi ni kama mgonjwa mahututi ambaye hata maji ya drip yamegoma kuingia kwenye mishipa akisubiri kifo tu
 
Kinachohitajiwa na wanachi si kulisha au kulishwa maneno ila ni mfumo mzuri wa kulitoa taifa letu hapa lilipokwama ili tusonge mbele so mi nafikiri hata kwa Mh mwenyekiti angesema kuwa dr. Slaa anafaa bado si tatizo ni haki yake kama mwanachama kuona mtu gani anafaa.
 
3. Nia ya Mwananchi si kuongeza tu readership/circulation, bali ni kupotosha kwa malengo wanayoyajua wao. Mfano Habari ya Mh. Arfi, Habari ya Lema. Habari ya Mh. Lema
Ngoja tuwafatilie wakizingua tuna watupa kabini kama uhuru na habari leo....
 
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo.” Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.
 
All in All fuateni demokrasia ndani ya chama chenu lakini the issue is 2015 "we need Dr. Slaa to be CDM Presidential candidate" simple as that - hatumun'gunyi maneno wala hatupapasi macho.
 
Back
Top Bottom