Mbowe: Sikumtangaza Dr. Slaa mgombea urais 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe: Sikumtangaza Dr. Slaa mgombea urais 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SEBM, Jan 3, 2013.

 1. S

  SEBM JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 496
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amenukuliwa akikanusha kutanganza kuwa Dkt. Slaa atakuwa mgombea wa Urais kupitia CHADEMA 2015. Alifafanua kuwa, alichokisema katika Mkutano wa hadhara Karatu mwishoni mwa wiki ni kuwa;

  1. CHADEMA haina Mgogoro bali ni mitazamo tofauti baina ya watu (hali ya kawaida panapokuwa na wengi)

  2. Hana nia ya kugombea urais 2015.

  3. Yeye na Dkt Slaa hawagombanii urais 2015. Dkt Slaa amefanya mengi katika Chama na hata uchaguzi wa 2010 alisaidia kupatikana kwa wabunge wengi.

  4. Akiwa Mwenyekiti wa Chama, atasimamia upatikanaji wa wagombea bora wa urais, ubunge na udiwani.

  Source: TANZANIA DAIMA 03/01/2013.

  MY TAKE

  1. Gazeti la Mwananchi limekuwa mstari wa mbele kuandika habari za upotoshaji kuhusu CHADEMA.
  2. Gazeti la Mwananchi huibua habari bila ya ku-balance mambo au kutupa mwendelezo(continuity).
  3. Nia ya Mwananchi si kuongeza tu readership/circulation, bali ni kupotosha kwa malengo wanayoyajua wao. Mfano Habari ya Mh. Arfi, Habari ya Lema. Habari ya Mh. Lema
   
 2. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2013
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  gazeti la mwananchi wameanza kulewa sifa sasa wanaharibu
   
 3. E

  ESAM JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Mimi nilijua tu Mbowe na busara zake asingeweza kusema kama media zilivyoripoti. Sasi sana mwenye kiti kwa ufafanuzi
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2013
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hili gazeti limeshanunuliwa na magamba!
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2013
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Litakuwa limeingia kwenye payrol ya nepi
   
 6. s

  sabas matata Member

  #6
  Jan 3, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  waandishi makanjanja hao!
   
 7. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,331
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Hivi Mwananchi sisi si ndio tulioipandisha Chati baada ya Masumbuko Lamwai kuleta za kuleta na Majira yao. Mnaonaje kilichoitokea majira kirudi Mwananchi. KWA PAMOJA TUNAWEZA. dawa ni kulisusia tu kama inavyofanyika kwa majira, Uhuru, Mzalendo na mengine mengi ya Kidaku.
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2013
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,165
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Unapojibu habari unatengeneza habari. Ila kisiasa sio mbaya kila habari inatengenezwa kwa maana maalum.

  Nilijifunza hili mwaka 1998 mwezi August tarehe 28.

  Hivi vyama sijui vimelogwa?, Naibu katibu anabwabwaja, Mwenyekiti naye anabwabwaja, Angalau katibu!

  Nitaendelea kubakia bila chama kwa kweli
   
 9. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,678
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hilo gazeti ni kipenzi chama kiongozi mmoja wa juu wa CDM.
   
 10. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #10
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,604
  Likes Received: 1,887
  Trophy Points: 280
  - Nice sasa amesoma alama za nyakati na kujua kwamba alipotoka kuamua nani awe mgombea, all under Operation Chaos lakini the damage is done tayari!! too late!

  Le Mutuz!
   
 11. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,331
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Au Tiddo anataka kurudi TBC?
   
 12. M

  Mzee wa fund JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2013
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 520
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chezea propaganda za magamba ninyi?Eee!!!
   
 13. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #13
  Jan 3, 2013
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kina TUNTEMEKE Ritz na TandaleOne wana mkanda walio mrekodi Mbowe ngoja waje watusikilizishe.

  Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,678
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  ngoma ni ile ile 2015 Dkt.Slaa for presidency mpaka mkae.
   
 15. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Inanikera sana pale mtu mzima wa miaka 45+ anapokua anategemea "ugali wa kengere".... yeye anachofanya ni u-PIMP TU...
   
 16. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,678
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Mkuu huyo TUNTEMEKE sijui huwa ni chama gani kwani kazi yake yeye ni kupotosha tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2013
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,234
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  Hivi na wewe uwa Chadema? Haya siyo maneno yangu namnukuu Molemo,

  "Familia imeishaamua Dr Slaa ndiyo mgombea urais 2015 kupitia Chadema. Dr Slaa atosha" Molemo wa JF.

  Wewe na Mtei nani mwenye chama?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2013
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema baadhi ya vyombo vya habari vimemlisha maneno, na hivyo kupotosha kauli yake aliyoitoa katika mkutano wa hadhara jimboni Karatu hivi karibuni.

  Alisema kuwa upotoshaji huo umeibua mjadala kwa baadhi ya wanasiasa na vyombo kadhaa vya habari wakijaribu kupotosha kuwa ndani ya chama hakuna demokrasia.

  Mbowe alifafanua kauli yake jana wakati akizungumza na Tanzania Daima na kueleza kile alichokisema katika mkutano wake huo ili kuondoa upotoshaji unaoendelea.

  Alisema kuwa chimbuko la kauli yake lilikuwa ni baada ya kusikia watu wakisema kuwa kuna makundi ndani ya chama ambayo yanawaunga mkono yeye, Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu (Bara), Zitto Kabwe yakiwataka wagombee urais 2015.

  "Nilichokisema ni kwamba hakuna makundi katika chama, ila kuna mitazamo tofauti katika mambo mbalimbali jambo ambalo ni la kawaida sana," alisema.

  Mbowe alifafanua kuwa, aliwaambia wananchi kuwa hawana makundi, bali wana utofauti wa mtazamo na kwamba hakuna ugomvi kati yake na Dk. Slaa kwa sababu ya urais 2015.

  "Nilisema sigombei, hivyo hatugombanii vyeo, tunaheshimiana na tunaelewana. Niliongeza kuwa 2010 sikugombea, tulimtuma Dk. Slaa na alitosha katika nafasi ile na hakuna anayebisha kuwa hakutosha maana alitupatia wabunge wengi.

  "Niliwaambia kuwa mimi ni mwenyekiti, nitasimamia kanuni na taratibu za kuwapata wagombea wazuri, tangu rais, wabunge na madiwani, na nikasema ni vema tukawatambua wagombea mapema kwani hatutakubali wale wanaojiunga mwishoni kutoka CCM kwani tumegundua ni mamuluki.

  "Hao wananilisha maneno kwa kunitolea kauli tofauti na niliyoisema kulingana na malengo yao," alisema.

  Mbowe alisema kuwa anaomba Watanzania waelewe kuwa yeye ni mwenyekiti wa chama na anaelewa umuhimu wa vikao na kuheshimu uamuzi wa vikao hivyo.

  "CHADEMA si mali ya Mbowe, ni mali ya wanachama, hivyo siwezi kupinga suala la uamuzi wa pamoja ambao mimi mwenyewe ndio nawashauri wengine," alisema.

  Alisema kuwa yeye ni mmojawapo wa waasisi, na amekuwa mjumbe wa Kamati Kuu zaidi ya miaka 20 sasa, na kwamba anajua maana na umuhimu wa kufanya kazi kama timu, lakini akaomba kuwa tafsiri za watu binafsi au baadhi ya vyombo vya habari zisipotoshe alichokisema.


  Chanzo: Tanzania Daima
   
 19. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2013
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,558
  Likes Received: 2,196
  Trophy Points: 280
  Too late azma yao imeshajulikana mgombea wa CHADEMA lazima atoke kaskazini.
   
 20. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2013
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,209
  Likes Received: 1,983
  Trophy Points: 280
  ...si nilisikia hili gazeti la mwananchi huwa linapelekewa habari na kiZito flani baada ya kuziandika mwenyewe....!!Nilisikia tu.
   
Loading...