Mbowe: Sikumtangaza Dr. Slaa mgombea urais 2015

Mbowe: Sikumtangaza Dr. Slaa mgombea urais 2015

Mbowe katika kuizima kashfa ya ufisadi wa mradi wa maji akaona awapoze wana Karatu kwa kuwaambia Babu atakuwa raisi ajaye 2015.
 
MSIJARIBU kulikwepa hili, wachangiaji wengi humu jf, hasa wale wenye mrengo wa CDM bila kufikiri kwa kina WALIGEUKA na kuwa sawasawa na gazeti hilo La MWANANCHI. kwa kuandika wakipongeza maamuzi hayo yakupotoshwa ya MH mbowe, TUJIFUNZE tuwe wa kwanza kukataa, kile ambacho tunaamini ni kinyume cha taratibu maana leo hii tungekuwa tunapongezana kwa kile tulichokosoa. heri yangu nilipinga .
 
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: "Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo." Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.

Wanaounga mkono

Mtei alisema anaunga mkono kauli ya Mbowe akisema kiongozi huyo hajakosea kumtangaza Dk Slaa kuwania urais mwaka 2015.

"Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama," alisema Mtei.

Ingawa Mtei hakuwa tayari kusema ni kikao gani kilichopitisha jina la Dk Slaa kuwania nafasi hiyo, alisisitiza: "Kuna vikao vya Kamati Kuu vimefanyika hivi karibuni, vinaweza kuwa vimefanya uamuzi huo. Mwenyekiti hawezi kuzungumza jambo bila baraka za vikao vya chama."

Hata hivyo, kauli hiyo ya Mtei inapingana na ile aliyoitoa Oktoba 6, mwaka huu baada ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kutangaza kutogombea tena ubunge badala yake kusema anataka kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kuwania urais mapema kungesababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama hicho.

Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

"Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga."

Alisema mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 kumekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.

Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais huku akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.

Hata hivyo, Zitto jana alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: "Nimesikia hata mimi kwenye vyombo vya habari ila sina cha kuzungumza kuhusu hilo."

Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alisema kauli hiyo Mbowe siyo yake binafsi, bali ni ya wananchi.

"Ni kauli na maoni ya Watanzania wanaomwamini Dk Slaa kuwa anaweza kumudu kuliongoza taifa hili kama walivyoonyesha kwa kumpigia kura nyingi kuliko mgombea yeyote wa upinzani katika nafasi ya urais (mwaka 2010)," alisema Heche.

Heche alisema ingawa ndani ya Chadema kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kuliongoza taifa, nyota ya Dk Slaa bado inang'ara.

Msimamo wa Heche uliungwa mkono na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alisema ni sahihi Dk Slaa kugombea urais mwaka 2015.

Lema alisema katika historia ya chaguzi za vyama vingi nchini, hakuna mgombea wa upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kama Dk Slaa mwaka 2010 akadai kwamba ndiyo maana hivi sasa CCM kinafanya kila njama kumdhoofisha.

Lema alisema hatua ya kumtangaza Dk Slaa kuwa mgombea wa urais mwaka 2015, itaondoa harakati za chinichini zilizokuwa zikifanywa na watu ndani na nje ya Chadema kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama hicho, hasa Mbowe na Dk Slaa.

Wanaopinga

Wakati Mtei akieleza kuwa Mbowe amepata Baraka za chama, Profesa Baregu alisema kutangazwa kwa jina la Dk Slaa kuwania urais ni maoni binafsi ya mwenyekiti huyo.

"Hayo ni maoni yake, lakini vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuteua jina la mgombea urais na havijakaa," alisema Profesa Baregu.

Alipoulizwa maoni yake kuhusu sababu za Mbowe kumtangaza mgombea urais sasa kabla ya wakati, Profesa Baregu alisema: "Mbowe atakuwa amefanya hivyo kwa sababu watu wengi walikuwa wanadhani kwamba yeye pia anawania nafasi hiyo ya urais."

"Hivyo ili kuweka mambo sawa ameamua kutangaza mapema kuwa hatawania urais na kwamba Dk Slaa ndiye anayefaa kuwania nafasi hiyo," alisema.

Profesa Baregu alisema haoni tatizo kwa wanachama wa Chadema kutangaza nia mapema kwa sababu hiyo ni haki yao kwa mujibu wa katiba... "Hata kama watu wengi watatangaza nia ya kuwania urais, siyo jambo baya katika ujenzi wa demokrasia, lakini uamuzi wa mwisho ni wa vikao vya chama."

Kauli ya Profesa Baregu kuhusu vikao iliungwa mkono na Dk Mkumbo ambaye alisema kwamba anachojua vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuhusu uteuzi wa wagombea wa ngazi ya urais.

Dk Mkumbo alionyesha shaka kama kweli Mbowe alimtaja Dk Slaa kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo akisisitiza: "Ninachofahamu ni kwamba yeye ametangaza kuwa hatagombea nafasi hiyo."
 
Mbowe katika kuizima kashfa ya ufisadi wa mradi wa maji akaona awapoze wana Karatu kwa kuwaambia Babu atakuwa raisi ajaye 2015.

Hujui unenalo. Huwezi kufanya japo utafiti kidogo tu, kabla hujaamua kubisha, achilia mbali kujenga hoja kinzani dhidi ya hoja nyingine au mtu mwingine usiyekubaliana naye!
 
Hujui unenalo. Huwezi kufanya japo utafiti kidogo tu, kabla hujaamua kubisha, achilia mbali kujenga hoja kinzani dhidi ya hoja nyingine au mtu mwingine usiyekubaliana naye!
Makene viongozi wako hawana dhamana utawatetea sana lakini haisaidii kitu.Suala hapa si kujenga hoja au utafiti tatizo ni matamko na jazda za jukwaani za viongozi wako wakilenga kuiteka hadhira mwisho wake wanajikuta wameharibu.
 
Tunapaswa kuwa makini sana na magazeti yetu, yanaandika kile kitakachouza magazeti yao hata kama ni UONGO bila kuwaza athari mbaya zitakazotokea. Shetani ana tabia hiyo hiyo ya kusema ukweli 99% na kuchomeka uongo 1% ambayo ita-distort content & context ya habari yote. TUNAPASWA KUWA MAKINI SANA. Nadhani CDM wanapaswa kuwaandikia magazeti yaliyopotosha habari hii na kuwapa onyo na iwapo watarudia kufanya yanayofanana na haya watangaze kuwa haya magazeti sio adilifu ili wananchi tuyakwepe.
 
Ina maana aliongea kichaga au kiswahili kama ni kiswahili aliyasema hayo anayoshutumiwa nayo
 
MSIJARIBU kulikwepa hili, wachangiaji wengi humu jf, hasa wale wenye mrengo wa CDM bila kufikiri kwa kina WALIGEUKA na kuwa sawasawa na gazeti hilo La MWANANCHI. kwa kuandika wakipongeza maamuzi hayo yakupotoshwa ya MH mbowe, TUJIFUNZE tuwe wa kwanza kukataa, kile ambacho tunaamini ni kinyume cha taratibu maana leo hii tungekuwa tunapongezana kwa kile tulichokosoa. heri yangu nilipinga .
Mkuu lufungulo,asante kwa udadavuzi leo wanakana walichokinena wao wenyewe.Tatizo la pro CDM ni kuunga mkono kila linalosemwa na viongozi wao hata kama ni la kipuuzi .
 
source Tz Daima?
Hili ni gazeti lake kaona alichemka kaamua kutumia gazeti lake kujisafisha

Poleni sana wapenzi wa viongozi. Mtadanganywa sana
 
Kwa hiyo hajatangaza kumwunga mkono Slaa.Mbowe nashukuru kwa kusahihisha makosa
 
Hii kazi ilipaswa kufanywa mapema na haraka sana baada ya kuwa imetoka kwa kupotoshwa na baadhi ya magazeti hasa Mwananchi. Kuacha habari potofu isambae kama petroli kwa muda mrefu huku ikizua mijadala hasi dhidi ya chama miongoni mwa watu makini ni kupoteza imani kwa Wananchi. Ni vizuri akina John Mnyika na Tumaini Makene wawe sharp katika counter attacking.
 
Last edited by a moderator:
Tunapaswa kuwa makini sana na magazeti yetu, yanaandika kile kitakachouza magazeti yao hata kama ni UONGO bila kuwaza athari mbaya zitakazotokea. Shetani ana tabia hiyo hiyo ya kusema ukweli 99% na kuchomeka uongo 1% ambayo ita-distort content & context ya habari yote. TUNAPASWA KUWA MAKINI SANA. Nadhani CDM wanapaswa kuwaandikia magazeti yaliyopotosha habari hii na kuwapa onyo na iwapo watarudia kufanya yanayofanana na haya watangaze kuwa haya magazeti sio adilifu ili wananchi tuyakwepe.

mbowe umesema kweli na ninashukuru kwa kukanusha haya kwani kuna magazeti hata ukiwa na elfu moja ya vocha tu,wanaweza wakaandika utakacho.haya magazeti yana waandishi ambao wamepikwa na genge la walanguzi na wahuni wa mjini hata vyeti hawana,wanachojua ni kiswahili tu na kuwasilisha ripoti ndo maana wakipelekwa mahakamani hawajui kujijitetea.
 
Im verry dispointed na mbowe, angeweza sema aliteleza ulimi kwakuwa ni kweli aliongea.atatia aibu cku ukiwekwa mkanda wa kideo hapa na mtakosa namna ya kumtetea. Halafu jf mna mambo,watu washabadilika humu,mlikuwa mnamtetea na kusifia alichosema leo kageuka na nyie mnageuka, mejiabisha kwakweli.
 
Na haya ni maneno ya mkweMWASISI wa CHADEMA,Edwin Mtei amemtaka Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kumwachia Katibu Mkuu wake, Dk Willbrod Slaa fursa ya kuwania tena urais mwaka 2015 kwa madai kuwa ndiye chaguo la watu kwa sasa.

Kauli hiyo ya Mtei inakuja siku kadhaa baada ya kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwamba Dk Slaa awanie tena urais katika uchaguzi ujao huku yeye akijiondoa katika orodha ya viongozi watakaowania nafasi hiyo kupitia CHADEMA.

Akihojiwa na gazeti hili, Mtei alisema Zitto anapaswa kumwachia Dk Slaa apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao kwa kuwa ndiye chaguo la wengi.

"Zitto atagombea baada ya Dk Slaa na kwa sasa amwachie katibu mkuu atupeperushie bendera ya chama katika uchaguzi ujao kwani ndiye chaguo la wengi," alisema Mtei.

Mtei alisema yeye anasimamia msimamo wa Mbowe na kamati kuu ya chama hicho kuhusu kumpendekeza Dk Slaa kuwania nafasi hiyo.

Alisema kila mmoja ndani ya chama amekuwa na hisia na mawazo tofauti lakini msimamo wake kwa sasa ni kumtaka Dk Slaa awanie nafasi hiyo ya urais na si Zitto. "Kila mmoja na hisia na maoni yake, Dk Slaa ana yake, Freeman na yake hata mimi nina hisia zangu na Slaa ndiye pendekezo langu nataka atupeperushie bendera," alisema Mtei. ( MWANANCHI JAN 3,2013)
 
Mbowe amejingáta tena ulimi! Mtei amemwagia petroli kwenye moto. Sasa sijui na Mtei nae ameteleza kwa mara nyingine tena? CHADOMO!
 
Back
Top Bottom