Mbowe, Rais Samia atakugombanisha wewe na Wanachama, Wafuasi na viongozi wenzako wa CHADEMA

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Mwenyekiti Mbowe, kwa yanayoendelea nchi hii na kwa reaction ya wana-CHADEMA kufuatia maamuzi ya Spika kuwalinda Mdee na Wenzake, naiona hatari ya Rais Samia kukugombanisha na viongozi wenzako wa CHADEMA pamoja na wafuasi na mashabiki wa chama hiki.

Hizi ni tweets za Martin Maranja Masese aliyejitoa kuripoti kesi yake ile ya mchongo.

By Martin kupitia twitter:

Mwenyekiti, Freeman Mbowe aachane na mpango wa kupeleka ujumbe wa CHADEMA ikulu katika mazungumzo. Ni dhihaka mtu mzima kudharauliwa hadharani. Wao wanapenda picha zetu tukiwa Ikulu na wanazitumia kwa maslahi yao lakini hawaheshimu makubaliano ya pande mbili. Ni watu wabaya.

Mwenyekiti @freemanmbowetz SSH ni kiongozi wa CCM, hawajawahi kuwa na dhamira njema na sisi, hili la leo bungeni kuwakumbatia COVID-19 nadhani linapaswa kuwa taa nyekundu kwako. Tunaweza kuachana sasa na siasa zao za ulaghai mezani kwa kichaka cha maridhiano. Shtuka mwenyekiti!
 
Hili nilianza kuliona mapema.

Mbowe akirudi ikulu nitaanza kupoteza imani nae, hekima yake iliyopitiliza sasa inatumiwa vibaya na CCM na serikali yake.

Ameshaonesha nia nzuri alikuwa nayo, na utayari wa mazungumzo alikuwa nao, bahati mbaya wenzake ikulu hawako tayari, sasa aachane nao.

Wasituzuge na sauti laini na vilemba, awaachie watanzania sio wajinga wataamua, ukweli wanauona.
 
Anayekihujumu chama CHADEMA ni Freema Aikael Mbowe.
Hakika,anaye hujumu CHADEMA ni Mbowe..Anacheza mchezo wa kitoto sana..nina hakika hayo yote anayajua na walikubaliana na samia kwa maslahi yake.
 
Vijana wa ufipa wananifurahisha Sana. Mtu anatoa ushauri akiwa nyuma ya utambulisho(ID) feki na hapo hapo anataka Mbowe ndio awe mpambanaji akiwa na ID orijino. Kama mnaona njia aliyotumia Mbowe kutafuta suluhisho kwa mazungumzo haifai vueni ID zenu feki mpambane pamoja naye .

Hata yatakaposhindana Mbowe kwa hatua ya kutafuta majadiliano mezani ni ushujaa uliowashinda 'mafisi' wengi CHADEMA
 
Ndo maana wale covid walikua na kiburi sana mbele ya baraza.. Walishaambiwa watalindwa
 
covid 19 wanahitajika kwa sababu mbili..ule msaada wa european union WA EUROS ZA KUTOSHA BUNGENI unaohitaji idadi fulani ya wapinzani kwenye kamati zabunge wakati huo kuna watu waliiiba kura kupitiliza na kukosesha idadi

Pili inadhaniwa kwamba hii situation italeta mgawanyiko chadema kumbe IMEWAGEUZA WATU WENYE"HESHIMA ZAO" KUWA VITUKO
 
Mwenyekiti Mbowe, kwa yanayoendelea nchi hii na kwa reaction ya wana-CHADEMA kufuatia maamuzi ya Spika kuwalinda Mdee na Wenzake, naiona hatari ya Rais Samia kukugombanisha na viongozi wenzako wa CHADEMA pamoja na wafuasi na mashabiki wa chama hiki.

Hizi ni tweets za Martin Maranja Masese aliyejitoa kuripoti kesi yake ile ya mchongo.
Kweli asee
 
Kwan mbowe na mama dagama waliongea nn ? Ulikuwa mwaliko personal na sio masuala ya wabunge, hata yey mbowe anashangaa I

Maswala personal kisha akaambiwa aje awakanye wafuasi wake kuinanga serikali huku mitandaoni? Mimi ni mmoja kati ya watu wasio na imani tena na Mbowe hususani kwenye hizi safari zake za ikulu. Mbowe ashauriwe kuachia uenyekiti wa CDM ASAP.
 
Mwenyekiti Mbowe, kwa yanayoendelea nchi hii na kwa reaction ya wana-CHADEMA kufuatia maamuzi ya Spika kuwalinda Mdee na Wenzake, naiona hatari ya Rais Samia kukugombanisha na viongozi wenzako wa CHADEMA pamoja na wafuasi na mashabiki wa chama hiki.

Hizi ni tweets za Martin Maranja Masese aliyejitoa kuripoti kesi yake ile ya mchongo.
Naiona hatari hii mbele ya Mbowe , anapaswa kuamua kuwavna Samia au kuwa na Chadema
 
Back
Top Bottom