Mbowe ni mti wenye matunda mazuri na matamu kwa sasa hapa Tanzania

So funny indeed... Wote wanaomcheka na kumdhihaki Mbowe ni kapuku chokambaya wenye majina bandia wasio na uwezo hata wa kuongoza familia

Jr
 
MBOWE NI MTI WENYE MATUNDA

WANAOHAMA Chadema kwenda CCM walishagundua kwamba, ili upate Mapokezi ya Wana-CCM yenye Shangwe na Ndelemo kama hayo anayoyashangaa Lijuakali huko Jimboni kwao Kilombelo ni sharti umtukane na kumdhalilisha Mwenyekiti Mbowe.

Matusi na Udhalilishaji unaofanywa dhidi ya Mwenyekiti Freeman Mbowe unahusu kula Fedha za Chama na zaidi kwamba anang'ang'ania Uenyekiti wa Chama.

Utadhani Mbowe ndiye Kiongozi pekee anayehusika na taratibu za Matumizi ya Fedha za Chama hiki ama anaupata huu Uenyekiti kwa kujipachika ama kujiteua mwenyewe kwa lazima.

Hata wahusika (Custodians) wa Mali za Chama ikiwemo hizo Fedha za Chama ambao ni Makatibu Wakuu wa Chama kuanzia kwa Dr Slaa, Dr Mashinji mpaka wa sasa Mhe.Mnyika, hayupo anayewaza kama na wao wanaweza kuwa wahusika kwenye ulaji huu, ila Mbowe peke yake ndiye anayekula Fedha za Chama.

Ukiwaachilia mbali hawa Custodians, wapo pia Maafisa wa Chama wengi tu wanaohusika na masuala ya Fedha kwenye Chama kama ilivyo kwenye Taasisi nyingine yoyote ile, lakini hawa wanaohama Chama wanamuona Mwenyekiti Mbowe pekee kama mlaji wa Fedha za Chama.

Aidha, kabla hujafika kwa Maafisa wa Chama wanaofanya Kazi kwenye Idara ya Fedha, yupo Mtaalam wa Fedha anayeitwa Mhasibu. Huyu naye hajawahi kuonekana popote Machoni pa Wahamaji kama Mhusika wa kula Fedha za Chama, ila Mbowe peke yake ndiye mlaji wa Fedha za Chadema.

Lakini, jambo kubwa zaidi linaloishangaza Dunia nzima na Viumbe vilivyomo, ni jinsi gani Mkaguzi wa Serikali ya Magufuli (CAG Kichele) ameshindwa kuona jinsi Mbowe alivyokula Fedha za Chadema hata akafikia uamuzi wa kuipa Chadema Hati Safi baada ya Ukaguzi wake.

Kwamba, hawa wanaoshupaza shingo kuwa Mbowe amekula Fedha za Chama, wanataka kutuambia kwamba, CAG wa Serikali ya Magufuli siku hizi anampenda sana Mbowe na hata Mbowe akionekana amekula Fedha za Chadema inayoisumbua CCM anamuacha tu bila kumchukulia hatua na anatoa Hati Safi kwa Chadema.

Vijana wengi ambao tunaonekana leo hii Kisiasa, tumelelewa kwenye Mikono ya Uongozi wa huyu Freeman Mbowe tunayemtukana na kumdhalilisha pale tunapopata Mlango wa pili wa kutokea pale tulipoingilia.

Wahamaji wa Chama hiki karibia wote, wamekubali kuhama kwa kulishwa maneno ya Udhalilishaji kwa Maslahi ya CCM na Watu wao badala ya kuusema ukweli wa nafsi zao juu ya kwa nini wanahama kutoka Chadema.

Mwenyekiti Mbowe akubali apigwe Mawe ili tusonge mbele kama Chama, maana yeye ndiye tumemkabidhi jukumu hili la kutukanwa na kudhalilishwa kwa niaba yetu.

Msiogope!

Mapambano yanaendelea!

Watashindana na Chadema lakini kamwe hawatashinda.


In God we Trust
Mbowe ni Mbabe wa Mababe, hongera zake.

Je, unajua maana ya kaulimbiu ya CHAMA CHAKE "Peoples - Power". Politicians use people to get political power. Once in power they use them again to stay in power. That is Peoples - Power

Wakati Mbowe akitafuna mpunga, yeye na familia yake, ambao hakuupanda, nyie mnamshangilia, kumpamba na kumsujudu kama mazuzu. Angalau angejenga ofisi za chama, kuwalipa viongozi wa chama hata posho, kuwasaidia wapiga kura wa jimbo lake, nk.

Wahenga walinena Wajinga ndio waliwao, kama wewe Mnawia
 
Kawaulize lumumba wenzako na Tot
Kwa akili za mleta maada, Mbowe kuambiwa anang'ang'ania madaraka ni kutukanwa! Pia kuulizwa pesa kwa ajili ya uchaguzi ujao ziko wapi ni matusi! Kuna wakati ni ngumu kukubali kuwa chadema imefikia hapa. Tuwaache muendelee kupeana hayo matunda na mwenyekiti wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app

In God we Trust
 
Hawa wanao ondoka chadema ni sawa na kukataa kupanda daladala ya mshikaji wakonkwa sababu tuu unakwonea wivu, kumbe hujui daladala halikosagi abiria.
 
Mbowe ni Mbabe wa Mababe, hongera zake.

Je, unajua maana ya kaulimbiu ya CHAMA CHAKE "Peoples - Power". Politicians use people to get political power. Once in power they use them again to stay in power. That is Peoples - Power

Wakati Mbowe akitafuna mpunga, yeye na familia yake, ambao hakuupanda, nyie mnamshangilia, kumpamba na kumsujudu kama mazuzu. Angalau angejenga ofisi za chama, kuwalipa viongozi wa chama hata posho, kuwasaidia wapiga kura wa jimbo lake, nk.

Wahenga walinena Wajinga ndio waliwao, kama wewe Mnawia
Hongera sana mkuu wa mazuzu

In God we Trust
 
Back
Top Bottom