Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,519
- 41,030
Tungekuwa tunachukia ubaguzi, wa kwanza tuliyetakiwa kumtupia mawe ni Magufuli.Kitendo cha hayati Magufuli kufanya diversication of ecomic development kilimkwaza sana Mbowe na sasa ameanza kufunguka yake ya moyoni.
Kiongozi anayeona kanda walikotoka wazazi wake na ukoo wake kuwa ina umuhimu kuliko kanda zingine hafai hata kiduchu
Kiongozi anyefikilia masuala ya kuleta maendeleo kwa kuzingatia kanda na ukabila huyu ni kiongozi mbaya sana
Taifa la Tanzania naturally halina ukabila na Ukanda na kiongozi anayepandikiza chuki na za namna hii hafai hata kidogo.
Taifa hili halijawahi kuwa na kiongozi aliyebagua watu ili kuwapelekea maendeleo.
Huu ndio wakati wa kumchambua Mbowe na Chadema yake kuwa hafai kabisa.
Watu wapate maendeleo kwa jitihada zao na siyo kwa upendeleo. Hata upendelee namna gani, kama watu hawana elimu inayowapa mwamko wa kutafuta maendeleo ni kazi bure.
Magufuli aliipendelea sana Chato, je Chato imekuwa bora kuliko Mwanza, Moshi, Arusha, Iringa au Njombe?
Kilishikamanisha Taifa baada ya uharibifu alioufanya Magufuli, ni lazima uovu wote kama ule alioufanya wazi na kwa kificho, ni usemwe.
"Kipindi hiki wenzetu wa Kaskazini wasubiri kwanza" - Magufuli.
"Sitapeleka maendeleo majimbo yanayoongozwa na wapinzani. Hata mzazi huwezi kumpa chakula mtoto wa jirani kabla ya wa kwako" - Magufuli. Cha ajabu, kodi alichukua kote, lakini anasema maeneo mengine hatapeleka huduma za maendeleo.
Magufuli alikuwa kiongozi mbaguzi aliyejaa uovu wa aina mbalimbali. Tunamshukuru Mungu, kwa kulipa Taifa letu nafasi ya wananchi wake kuwa huru tena. Leo hakuna hofu ya kutekwa, kuuawa, kupotezwa wala kubambikiwa kesi. Tunamshukuru Mungu, siyo kwa kifo cha Magufuli, bali kwa kuliondia Taifa kutoka kwenye mateso.
Fikiria haya ni maneno ya Rais. Ni vigumu kuamini kama tulikuwa na Rais ambaye alikuwa mzima. Kauli ya Dialo kuwa marehemu alikuwa na tatizo la afya ya akili, inapata nguvu sana, ukikumbuka kauli kama hizi.