KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Binafsi, kwa mtazamo wangu ukiachana na gharama kubwa za uendeshaji wa Serikali za majimbo kwa maana ya kwamba mpaka Serikali inaitwa serikali inakuwa ni mamlaka kamili yenye kujitegemea kwa kila kitu. Na kama tutaamua kufuata utaratibu unaotumiwa na Marekani wa kila "state" Ina serikali yake hii itakuwa ni hasara kubwa kwa maana ya ukubwa wa serikali.
Mtazamo wangu unaotofautiana na wa CHADEMA. Kama CHADEMA wanaona Serikali ya majimbo iwe ni serikali kwenye majimbo ya uchaguzi au ngazi ya wilaya au ngazi ya mkoa sitakubaliana nao kabisa kwa sababu zifuatazo:
Ya kwanza, ngazi hizo zitafanya kuwe na Serikali nyingi sana hata ambazo zitapelekea gharama za utendeshaji kuwa kubwa. Ebu tuchukulie hili Kama mfano, Serikali zinazoanzia ngazi za mkoa kwa idadi ya mikoa iliyopo tutakuwa na Serikali 30. Hii itapelekea hasara kubwa mbeleni.
La pili, kwa kuwa kuna maeneo yaliyo bora kiuchumi kulingana na makusanyo hivyo serikali za majimbo zitafanya yawe bora zaidi na yale maeneo yasiyo na mzunguko mkubwa wa pesa yataendelea kudumaa.
Kwa sababu, tutakuwa tumerasimisha Cha sehemu Fulani ni Cha pale tu hakitakiwi kutoka nje ya pale na hivyo kufanya maeneo yasiyo na rasilimali kushindwa kujiendesha.
Moja ya faida kubwa ya muundo wa sasa wa serikali yetu ni mgawanyo bora wa rasilimali za eneo na zinatumika kusaidia uchumi wa taifa zima. Na mfumo huu unaharakisha maendeleo ya maeneo kwa haraka.
La tatu, kutakuwa na hatihati ya kuwepo kwa ukabila na ujimbo. Kwa Mazingira ya sasa ya serikali yetu ukabila si rahisi kuwepo kutokana na muingiliano mkubwa wa watu wa makabila au majimbo mbalimbali.
Sasa tufikiri kwa umbali mrefu zaidi juu ya suala hili kutakapokuwa na Serikali ya majimbo lazima kutakuwa na chokochoko tu kwamba kilichopo hapa ni kwa ajili ya wa hapa na kabila la hapa. Hivyo inaweza kuzorotesha umoja wa kitaifa tulionao.
Serikali kamili ya majimbo inaweza kuwa ni chanzo Cha matatizo mengi baadae hivyo wazo la kuwa na Serikali ya majimbo lina ugumu kiasi chake.
Licha ya hivyo bado nasimama na CHADEMA juu ya faida ya Serikali za majimbo kwa sababu zifuatazo:Kwanza, Serikali za majimbo zinaweza kuchochea maendeleo kwa haraka kwa sababu kila serikali itajitahidi kuhakikisha inaleta maendeleo. Pili, itasaidia huduma muhimu kuwafikia Wananchi wa haraka zaidi.
Hivyo badala ya kuwa na mfumo wa serikali wenye serikali za majimbo nyingi na kupelekea gharama kwa serikali kubw kubwa, Haya ndio maoni yangu kwenye Sera hiyo:
Kwanza, Sera ya Serikali ya majimbo ijikite kwenye eneo lenye ukubwa wa Kanda. Kwa maana ya kwamba kila Kanda iwe na Serikali yake hapa tutapunguza ukubwa wa serikali na gharama kwa kuihudumia.
Pili, ili kuwe na usawa kwenye mgawanyo wa rasilimali zilizopo serikali ya Kanda inaweza kuwa ni muafaka. Badala ya rasilimali kutumika eneo dogo kama Jimbo basi zitumike kwenye Jimbo.
Tatu, ili kusaidia maendeleo sawa kwa kila Kanda ,Serikali kuu iratibu mchakato wa maendeleo kwa Kanda zote. Makusanyo yanayokusanywa kwenye Kanda , asilimia fulani iende serikali kuu ambayo itatumia kuboost Kanda zilizo nyuma kimaendeleo.
Hitimisho, nakubaliana na CHADEMA juu ya Serikali ya majimbo ikiwa tu nao Wana mtazamo kama wangu na pia nakubaliana na wote wenye kutazama kwa jicho la gharama za uendeshaji wa Sera hii.