Vema,
Binafsi sipendi kuegamia upande wowote, nadhani ni wengi wapo hivi. Inakuwa ajabu pale mtu anapoingia kwenye forum akaona mawazo ya watu kama wanne akaanza kudai kuwa ina maana ninyi ni CUF au CHADEMA au CCM?
Sipendi hata kuitwa mmojawapo wa vyama hv. Ninachopenda ni mawazo mbadala ya kuweza kulitoa taifa letu kwenye upupu wa umasikini uliowatanza watanzania wenzetu. Najiona masikini lakini nikienda kijijini huwa najiona Mengi mdogo.
Barabara mzozo, umeme mzozo, maji balaa, mawasiliano ya simu ndo kabisaa hadi wapande miembe, nyumba za kulala basi hata usipende kuoneshwa, mavazi wengine bado wanavaa magome, chakula hata uhakika wa kupata mlo mmoja ni issue.
Nani atatukomboa? Siilaumu CCM, lakini wanataka nimlaumu nani? Upinzani? Wana nafasi ya kufanya hivyo? Serikali iliyo madarakani daima ndo hutwishwa mzigo. Ndo maana binafsi nikiilaumu CCM simaanishi kuwa SIIPENDI, hapana. Naipenda CCM kama ikitekeleza ahadi zake kwa watanzania.
Haya yote huahidiwa kila chaguzi. Wana bahati watanzania ni wasahaulifu hivyo kuwapa tena kura kwenye chaguzi zinazofuatia. Tena wengine wanajisifu vitu vingine ambavyo ilikuwa ni kutekeleza wajibu wao kama viongozi.
Sipendi hii tabia ya mtu kusifiwa sifa kem kem kwa kutekeleza wajibu. Mpinzani pia akipiga kelele bila kuhakikisha zinafika mbali na kuhakikisha umma unapata kile anachokipigia kelele basi namwona nae ni sawa na chura tu.
Tanzania yenye neema inawezekana! Na naamini mabadiliko mazuri yanaweza kuanzia kwetu hapa! Trust me, we can!