Eric Ongara
Senior Member
- Sep 19, 2006
- 165
- 8
Tumegeuka taifa la vipofu
Freeman Mbowe
KWA wengi, nimekuwa kimya. Kimya kina tafsiri nyingi. Kila mtu kwa uelewa wake na pengine matamanio yake. Leo nimeamua kuandika tena. Na nitaendelea kuandika "mpaka kieleweke." Nakiri ni muda mrefu sijaandika. Sababu ni nyingi. Naamini katika subira.
Naandika kwa mara ya kwanza kupitia vyombo vya habari - baada ya Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2005. Nilishiriki kama mgombea urais. Nilipigana, niliumia lakini jumla ya kura haikuniwezesha kuongoza nchi.
Sijutii ushiriki wangu. Naushangilia na kuuona kama mchango wangu wa ‘damu' kwa Watanzania wenzangu wa leo na kesho. Nimekomazwa na kuimarishwa katika dira, dhamira na hata mbinu za harakati.
Kwa wenye dhamira safi, uchaguzi una malengo mawili ya msingi. Yote ni sehemu ya mchakato wa harakati. La kwanza ni nia ya kupewa ridhaa ya kuongoza na la pili ni fursa ya kufikisha mawazo na fikra mbadala kwa wale wanaoombwa ridhaa husika. Naamini ujumbe ulifika japo haujatosha.
Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kushiriki uchaguzi ule. Nawashukuru wale wa chama changu walioniamini na kunitwisha msalaba ule. Watanzania wengi walinisikiliza – kwenye mikutano na kwenye vyombo vya habari – nawashukuru kwa subira yao!
Wako walioniombea usiku na mchana! Wako walionisaidia kwa hali na mali zao! Wako walionipa kura zao (zilizohesabiwa na zilizoyeyuka). Nawapa asante sana na nawaombea sana kwa Mwenyezi Mungu kwani sina uwezo wa kulipa fadhila na upendo wao kwangu.
Wako niliowakwaza ama kwa kauli au kwa vitendo katika mchakato ule! Nawaomba wanielewe! Naam, wako walioninyima kwa sababu mbalimbali za haki na zisizo. Hawa nao nawatakia heri! Wako walioniibia kura zangu! Hawa …..!
Nilishiriki kupokea matokeo yaliyomtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi. Nilimpongeza Kikwete kwa kumkumbatia. Niliwachanganya wengi, hasa wale wengi jasiri walioumia na walioshuhudia uhuni wa kutisha kutoka kwa mamlaka zilizopewa wajibu wa kusimamia haki, amani na usalama kwenye chaguzi na hata maisha yetu ya kawaida. Ni kweli rafu ilichezwa sana – hata Kikwete na timu yake wanajua uchaguzi haukuwa huru na wa haki. Si Kikwete wala wenzake wenye ujasiri wa kulikiri hili.
Nilipata moyo huo kwa sababu moja tu: Naipenda nchi yangu! Naamini katika mabadiliko ya mbinu na mazoea. Naamini katika subira. Utamaduni wa kukubali matokeo ni mojawapo ya mbinu za mapambano.
Kuna msemo wa Kiingereza unaosema "to retreat is not to surrender but rather, a war strategy", yaani "kurudisha majeshi nyuma si ishara ya kujisalimisha bali ni mkakati wa kivita." Niliamini kuwa mabadiliko ni mchakato, na mchakato ni tunda la muda!
Sawa, tuliibiwa, lakini tuna sababu ya kukiri pia kuwa tulikuwa na udhaifu wetu uliosababisha tukaibiwa! Hili nitalijadili siku za usoni!
Siku ya kupokea matokeo pale Diamond Jubilee, kundi kubwa la wanahabari lilinivaa na kunihoji: "Mheshimiwa Mbowe, kwa matokeo haya huoni kuwa wapinzani mmeshindwa sana?" Nilifadhaishwa na swali hili na nakumbuka kujibu: "Kwanza mimi si mheshimiwa ila ni kamanda…. Wa kujuta kwa matokeo haya siyo wagombea na viongozi wa vyama vya upinzani pekee, bali ni Watanzania wote…… Wana CCM wengine wanashangilia bila kujua msiba huu unawahusu ….. pengine wenye sababu ya kushangilia ni kundi dogo la viongozi wa CCM, serikali yake iliyopita na inayokuja na washirika wao ambao wana hakika ya hifadhi ya uchafu wao na mwendelezo wa ufisadi wao wakitumia mgongo wa mfumo wa vyama vingi."
Baada ya kauli ile, wanahabari wengi walitawanyika kwani wengi wao nao walikuwa katika mkumbo wa ulevi wa ushindi wa Kikwete na CCM. Wengi hawakujua kuwa, baadhi yao wameibaka taaluma na hivyo nchi. Walikuwa wamemaliza kazi ‘waliyotumwa' na hivyo wana sababu ya kukaa mkao wa kula! Wengi walijiona na wengine bado wanajiona sehemu ya utawala!
Leo zaidi ya mwaka umepita baada ya uchaguzi – wengine wanasema haukuwa uchaguzi bali ‘mnada wa kura.' Hukumu ya kama neema imeonekana nawaachia Watanzania. Mengi yanasemwa lakini moja linaendelea kunisononesha. Watanzania wengi wanauliza "Wapinzani wako wapi? Mbona kina Mbowe na wenzake hatuwasikii?
Maovu mengi yanafanyika mbona wao wamekaa kimya?"
Ukweli ni kuwa hawajakaa kimya. Wapinzani wamesema na wanasema sana, ila watawala, na baya zaidi Watanzania walio wengi bado wanawasaliti!
Watanzania wenzangu! Hata wapinzani ni binadamu wenye kupata maumivu na mfadhaiko. Kuna makundi mengi ya wanaharakati yanayopigania haki na ustawi katika nchi yetu. Najipa ujasiri kusema katika makundi yote haya, kundi la vyama vya upinzani (pamoja na kuwapo ‘waganga njaa' miongoni mwao) limejitoa mhanga kuliko makundi mengine yote!
Wengine wanadai kufanya siasa za upinzani Tanzania ni lazima uwe na ‘uendawazimu' kidogo. Hii ni kutokana na mazingira magumu ya maisha ya kiuchumi na kijamii kwa wengi yanayoambatana na harakati hizi.
Pamoja na upungufu wake, viongozi wa upinzani ni watu wenye kuhitaji kuungwa mkono na kusaidiwa mzigo huu na jamii. Jamii ina wajibu wa kututia moyo na siyo kubeza! Maisha yetu na familia zetu tumeyaweka rehani na kila siku kukicha salama tunamshukuru Mungu!
Kosa letu nini? Kutetea haki na ustawi katika nchi yetu na watu wake wakiwamo hao waliogeuzwa mawakala wa kutudhalilisha! Ninawaheshimu wote wenye mamlaka ya uongozi wa taifa letu. Kamwe sitasita kuwapongeza wafanyapo mema.
Hata hivyo, nakataa kufanywa kondoo. Nakataa kuwa mnafiki. Nakataa kubariki dhuluma, wizi, ufisadi na unafiki unaofanywa na wengi tuliowapa dhamana ya kuongoza maisha yetu ya leo na hata vizazi vijavyo.
Mbali na wajibu tuliopeana kikatiba, kwa kuwa katika nchi moja, yaani jamii moja tuna mkataba wa asili ambao wanafalsafa wanauita ‘social contract.' Kwa social contract hii, sisi kama Watanzania tumekubali kuachia baadhi ya uhuru wetu asilia na kukubali kutii mamlaka (na hivyo sheria) tukitegemea kuwa kwa kufanya hivyo, mamlaka itatuwezesha kupata uhuru zaidi unaoambatana na haki na ustawi.
Uchaguzi leo umekwisha lakini maisha yetu hayajakoma. Lazima tuendelee kujiuliza kama wale tuliowapa dhamana ya kutuongoza wanatekeleza wajibu wao kama sehemu ya ‘social contract' hii.
Mimi kama Mtanzania na zaidi kama kiongozi ninayeongoza kundi kubwa la Watanzania ni wajibu wangu kuendelea kuhoji utekelezaji wa ‘social contract' baina ya wananchi na viongozi. Naelewa hautakuwa ujumbe mzuri kwa wale wenye madaraka! Harakati ni zoezi la kudumu hasa pale haki inapokuwa inahubiriwa kinafiki kwa maneno lakini inabezwa kwa matendo na watawala.
Najua wengi wataingiwa hofu na maneno haya! Lakini sihitaji kujikomba kwa yeyote. Ndiyo, mimi si malaika au mtakatifu. Kama binadamu wengine, nami nina udhaifu wangu, lakini hauondoi ukweli na umuhimu wa kuhoji utendaji na dhamira ya wale wanaotuongoza. Kufanya hivyo ndiyo kuendeleza unafiki uliotufikisha Watanzania tulipo! Najua wengine watasema Mbowe anafanya kazi ya uchochezi! Ni kweli, sina sababu ya kukataa ukweli huu.
Sioni sababu ya kutochochea Watanzania waamke, wajijengee ujasiri kudai haki badala ya kuendelea kuiomba na kuona kuwa ni fadhila! Tuna sababu gani ya kutii mamlaka kama haitelelezi sehemu yake ya mkataba?
Utawala uliopatikana kwa njia chafu utatawala hivyo hivyo. Waliojitwalia madaraka kwa kutumia vibaya sheria (safi na chafu); vyombo vya dola yakiwamo majeshi ya ulinzi na usalama na hata usalama wa taifa; tume isiyo huru na isiyo ya haki; fedha za ufisadi; utajitakasa vipi kutenda yaliyo mema bila kukiri uharamia uliotumika kwenye uchaguzi?
Hivi kweli kiongozi mwadilifu anaweza kujisifu kwenye ushindi mchafu? Nina hakika viongozi wetu nao wanapenda kusifiwa. Sina hakika ni wangapi wanaambiwa ukweli kavu kavu kama huu! Mimi nitawaambia na maisha yangu nayakabidhi kwa Mungu!
Nchi inafadhaisha. Viongozi wanashangilia umaskini wetu na ujinga unaotujengea woga na hofu! Watanzania tunajengwa kuwa tegemezi kwa serikali kifikra na kiuchumi. Tumefungwa mnyororo wa fikra! Bado tuna usingizi wa kudhani Kikwete na Lowassa ndio wana ufunguo wa suluhisho la matatizo yetu! Ndiyo sababu kila kukicha utasikia "serikali itusaidie lile, Kikwete tukomboe, Lowassa tupia jicho lile!' Eti wanaombwa wakati ni wajibu wao kujua.
Tabia ya kutukuza viongozi na serikali imeendelezwa hata bungeni. Utasikia wabunge "tunaiomba serikali…., tunamwomba waziri n.k.'' Tumejikabidhi jumla kama makinda! Kikwete anapeta Ulaya sisi tunamngojea! Siku akirejea, mawaziri kazi hawafanyi – wote wakiongozwa na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, mawaziri, mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya, meya na wengine kibao lazima waache kazi, wachome mafuta ya misafara ya magari wakajipange uwanja wa ndege kumpokea ‘messiah' mwenye muarobaini wa matatizo ya Watanzania!
Huu ndiyo unafiki na ukondoo na si itifaki wala nidhamu! Ni udhaifu unaoukuta nchi za Afrika tu! Leo kuna watu wazima tena wasomi wanaamini bila CCM hawawezi kuishi! Nani kasema bila CCM hakuna maisha? CCM ya nini kama imeshindwa kutekeleza wajibu wake katika ‘social contract?'
Tupende tusipende, katika jamii yoyote kuna matabaka ya watu. Daraja la juu, la kati na la chini. Mara nyingi Tanzania tunajidanganya, hatuna matabaka haya! Pengine liliwezekana kidogo enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
Daraja la juu leo lina viongozi wa juu serikalini, washirika wao ambao ni wafanyabiashara wakubwa na hasa wawekezaji wa nje. Katika nchi yetu, kundi hili ni dogo sana na nina diriki kusema halifiki watu 250! Katika nchi yoyote, kundi hili ndilo hufaidi nchi na lenye neema. Halipendi mabadiliko kwani tayari uzuri au ubora uliopo kwao ni neema!
Daraja la kati (working class) ndiyo mara nyingi huleta mabadiliko katika nchi. Kundi hili hujumuisha viongozi wa dini, wasomi – yaani wanataaluma mbalimbali, watumishi wa serikali (civil servants), viongozi wa kijamii wakiwamo waandishi wa habari - (civil society), viongozi wa kisiasa (political leaders) na wafanyabiashara wa kati.