Wana CHADEMA, naomba kuwashauri Kama ifuatavyo:
1. Matamshi yenu Mara huyu kambi ya Zitto na huyu ya Slaa! Yanakera wasomaji Kama Mimi na wengine naamini.
2. Badala ya kujenga Chama chenu mnakiua kila kukicha,
3. Kwa staili hii hamtafika 2015, hata wale mliowapata mtawapoteza, pia wanaotaka kujiunga mnawazuia maana kutwa ni ooooo! Zitooooo oooooooo! Silaaaa? Hamna kazi za kufanya?
4 badala ya kumjenga mdogo wangu Zito mnambomoa bila kujua. Your promoting strategy is too cheap!!!!!!
5. Mara nyingi nimekuwa nikimsikiliza Zitto, huwa Ana hoja nzuri sana sana, tatizo huzianzisha Kama mtu binafsi na sio Chama. Fuatilia hoja zote za Zitto tangu ameanza, kutwa ni media tuu (one man show), itawezekana hapewi ushirikiano au la sijui.
6. CCM inajiimaisha, CDM inajibomoa, hata pale mlipojenga mnabomoa wenyewe, tena kwa mikono yenu, so sad
7. CHADEMA watu waliwapenda/ wanawapenda only kwa sababu mumeweza kusaidia kuongoza nchi mkiwa pembeni na hii ni dhana nzima na maana ya upinzani. Pale mnapokosa dira na kuanza viroja ninyi kwa ninyi Hakika mtaangamia.
8. Mjitathmini upya muangalie Kama bado mko kwenye njia sahihi au la. Jirekisheni mapema msipoangalia aliyosema mhe Wasira yatatimia.
9. TUNAPENDA MUENDELEE KUWEPO ILI MUIKOSOE SEREKALI KWA FAIDA YA WATANZANIA
Naomba kuwasilisha
Queen Esther