sokowelehk
Senior Member
- Sep 16, 2018
- 161
- 126
Ukweli toka moyoni mwangu, Wewe ni mfiasi wa upinzani mwenye uelewa wa juu saana, nimekua nikikufuatilia tangu muda kidogo, mfano ujio wa lowasa ndani ya chadema, uliupinga hadi pale aliporudi alikotoka. Wapinzani wengi wa Tanzania wanaweza wasikuelewe ila ukweli utasimama na mbowe anatakiwa kupumzika.Kwani ni yeye tu anaweza kupitia hayo? Ni lazima anayekuja na yeye apitie mazingira yake? Mbona wako wapinzani wengi tu wanapitia hayo, au yeye ni special? Kaondoka Slaa na cdm bado ni hai, tujenge cdm imara kama taasisi, na sio viongozi ving'an'ganizi wa madaraka eti ni watu imara. Kama amekuwa mwenyekiti kwa miaka 15 bila kujenga taasisi imara bali kujigeuza yeye ndio imara, basi hicho sio chama bali kundi la marafiki walioko kwenye siasa. Cdm tujitahidi kuepuka siasa za mtu bali tujenge chama imara, kwani Mbowe anaweza kufa hata leo, je ikitokea hivyo ndio chama kitakufa, acheni mambo ya utetezi wa aibu.