Mbowe, na sisi pia tumekuchoka pumzika acha udikteta ndani ya chama

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Messages
8,673
Points
2,000

technically

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2016
8,673 2,000
Mimi ni mfuasi wa mageuzi ndani ya nchi hii ila niseme ukweli wa principle ya dictetor yeyote, watu wanaomzunguka huwa hawamwambii ukweli na uwa wanamkimbia pale maji yakiwa shingoni hivyo natoa ushauri sio tu kwa Mbowe.

Watu wote wenye mamlaka ya kiuongozi jaribuni kuwa mnatoka na kwenda kusikiliza Umma unataka nini juu ya uongozi wenu.

Ndicho kinachofanyika kwa Mbowe watu walio karibu yako wanakupaka mafuta kwa mgongo wa chupa ila ukweli wanaujua wewe umechoka hauna tena jipya ndani ya chama wao wanakushauri upuuzi ili waendelee kula ruzuku sasa subiri 2020 ruzuku ikipungua jinsi watakavyokubadilikia.

Mbowe Jiangalie ondoka kwa heshima kama kweli CHADEMA ni taasisi toka nenda mtaani sikiliza watu halisi wapenda mabadiliko ya kweli sio wapambe.
 

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
1,405
Points
2,000

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
1,405 2,000
Mimi ni mfuasi wa mageuzi ndani ya nchi hii ila niseme ukweli wa princple ya dictetor yeyeto watu wanao mzunguka uwa hawamwambii ukweli na uwa wanamkimbia pale maji yakiwa shingoni ivyo natoa ushauri sio tu kwa Mbowe, Watu wote wenye mamlaka ya kiuongozi jaribuni kuwa mnatoka na kwenda kusikiliza Umma unataka nini juu ya uongozi wenu.
Mkuu,ungesubili kwanza mning'inio uishe ndipo ufikilie unachoandika
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,538
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,538 2,000
Bora umenisaidia kusema. Ni kweli Mbowe kafanya mazuri na kakifikisha chama pazuri. Pia amekaa madarakani muda mrefu wa kutosha, ni vyema akipisha wengine wasogeze chama mbele. Uzoefu unaonyesha kiongozi mzuri huwa ni miaka 10 mwisho, ikizidi sana 15. Ikipita hapo, hata yale mazuri yake huanza kuyaharibu.

Tujenge utamaduni wa kupokezana vijiti ili kuleta mawazo na hamasa mpya kila wakati. Msimamo wangu huu ni dhabiti na ninaweza kuutetea bila kumhofia mtu yoyote. Huu sio muda wa Mbowe kuendelea tena kuwa mwenyekiti wa cdm kwa Utetezi wowote ule.
 

sacred wall

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Messages
368
Points
1,000

sacred wall

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2017
368 1,000
eti muumini wa mageuzi kama ungekuwa muumini wa mageuzi ungejua umuhimu wa Mboe ndani ya upinzani
technically ni upinzani, sema amepotea leo. Mkicheza mchezo wa kitoto CDM linakuwa tawi la CCM. Technically, muache mbowe awavushe katika janga la Jiwe! Anahitajika mwamba ambaye yuko tayari kufa! siyo mimi au wewe tunaoogopa kufa na kufilisiwa!
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,538
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,538 2,000
Kwenye udikiteita wa Jiwe Mbowe akiondoka, CDM imekufa! labda kama unataka ife!
Ni kipi ambacho Mbowe anazuia sasa hivi akiwa mwenyekiti? Kama ni uhanga yeye ni muhanga namba moja wa udictator wa Magufuli. Miradi yake mingi imehujumiwa tena kwa sababu zilizo wazi za kisiasa. Kesi anazo za kubambikiwa na huenda akafungwa, alikaa ndani siku 90 tena kwa amri toka juu na hakuna chochote alichofanya.

Kama ni haiba ya chama inazidi kuharibiwa huku yeye akiwa mwenyekiti, viongozi mbalimbali wanahongwa na kuhamia ccm, mikutano na kazi za kisiasa zilizopo kisheria Magufuli kazizuia na Mbowe katii bila hata kwenda mahakamani kupata uamuzi wa kisheria. Kampokea Lowassa na kumpa cheo adhimu cha kugombea urais, hivi leo karudi ccm baada ya kuitumia cdm kama kondomu, mwenyekiti madhubuti hawezi kuokoteza mgombea urais kwa njia ya mwendo kasi. Sasa kwa mazingira hayo na muda aliokaa madarakani aendelee kuwa mwenyekiti ili iwe nini kwa mfano?
 
Joined
Nov 5, 2019
Messages
19
Points
45
Joined Nov 5, 2019
19 45
Nikwel huu ni mda mzuri wa Mbowe kuachia uenyekiti kwa huo mda ametufikaisha pazuri , John heche ,ana faa kupokezana kijiti na Mbowe, pia kama akipitishwa tena kuwa mwenyekiti namshauri awe mkali kama mwenzake( jiwe) akimwaga mboga Mbowe achukue ugali akatafute mboga kwa jirani asiendelee kuzira wakati wa kula.
 

tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,538
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,538 2,000
technically ni upinzani, sema amepotea leo. Mkicheza mchezo wa kitoto CDM linakuwa tawi la CCM. Technically, muache mbowe awavushe katika janga la Jiwe! Anahitajika mwamba ambaye yuko tayari kufa! siyo mimi au wewe tunaoogopa kufa na kufilisiwa!
Hakuna cha kuivusha cdm, siungi mkono kiongozi yoyote anayeutaka uenyekita wa cdm aliyetokea ccm, kama Cecil Mwambe au Sumaye, ila kuna watu madhubuti kama John Heche nk. ambao ucdm wao hatuna shaka nao.
 

Forum statistics

Threads 1,388,907
Members 527,828
Posts 34,014,205
Top