Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

makao makuu ya ccm yaende Dodoma na makao makuu ya chadema yaendelee kuwa Dar,baada ya watu wa Dodoma kuamka na Dodoma itatawaliwa na chadema
 
Yupo sahihi. Ni vizuri kuhamia Dodoma, lakini sii kwa kukurupuka hivi. Wanaokosoa mpango huu wana sababu za msingi, moja ni budget ya Serikali ya mwaka huu haioneshi popote kuhamia dodoma, wanatumia gharama toka budget gani? Iliyoidhinishwa na nani? Pili, Dodoma ninayoifahamu mimi,imejiandaa kwa ujio wa Serikali ndani ya kipindi hiki kifupi?

Kwa maoni yangu, kuna UWEZEKANO MKUBWA WA BUDGET NZIMA YA SERIKALI KUTOTEKELEZEKA KWA ASILIMIA ZAIDI YA 70, hivyo kuja na MKAKATI WA KISINGIZIO CHA KUHAMIA DODOMA. Kama kawaida yetu,tutabaki kulijadili hili suala kwa muda mrefu na hivyo kuwapa mwanya wa kufunika Kombe Mwanaharamu apite. Tukija kushtuka, mwaka wa budget haupo,tunaingia mwaka mwingine. Ni vema tukawa tunafikiri nje ya box
 
Mbowe hapo umezingua

Mpango wa kuhamia Dodoma ni positive kabisa.......kwa maana ya Maono ya mbali

Na change yoyote lazima iwe na resistance..Ili kuweza ku drive change you need to have some sort of madness....Kitu ambacho Bro Magu ana practice now

Sasa Mbowe...sio kila kitu unapinga...sometimes sikusomi kabisaaaaa..Pongeza mara zingine.....kama king of Tz Politics Lowasa

Faida ya Kupongeza ni kupunguza tension na kufungua mwanya wa concessus kwa ajili ya Maendeleo ya Watanzania

CCM wanayo serikali...Huwezi kupambana nao at close ends...Compromise...Compromise

Mbowe be wise meeeeen
Hujasoma bandiko lote,hivyo comment yako ina mapungufu ya kimwendokasi. Hiyo madness unayozungumzia wewe ni ya watu kwenda kuishi uwanja wa jamuhuri? Hivi kwa nini mmekuwa watu wa kupiga makofi kwa kila kitu? Mbowe kashauri ni vema wizara chache zikahamia kwa mwaka huu,mwaka kesho hivyohivyo, hii ni kutokana na hali halisi ya Dodoma. Kama hujawahi kuishi au kufika dodoma kaa kimya!
 
Wanakimbia mamlaka ya kuwa chini ya himaya Mayor wa chadema [emoji111][emoji111][emoji111][emoji111]
 
Mzee mbowe naona ungeshauri namna yakutekeleza mpango wa raisi nasiyo kukosoa moja kwa moja kama siyo jambo jema, tumeshuhudi mipango mingi ya muda mrefu haitekelezeki 100% hii yakukurupuka kwa sasa inatija tushauri namna gani ya kututekeleze japo lazima tukiri changamoto hazikwepeki
Rudi kasome tena hapo juu mwanzo hadi mwisho. Ametoa ushauri mzuri tu, ila kwa akili za mwendokasi naamini kabisa haziwezi ku chew hicho alichokisema!
 
Kuhamia dodoma kuna faida sana kwa uchumi wa nchi
Hebu taja hizo faida za kiuchumi hata tano kama kweli unazijua.

Mie najua zipo faida,hakuna anayekataa, tatizo, serikalivimejiandaa? Kwa miundombinu ipi? Kwa bajeti ipi? Mkutano mkuu wa ccm ukifanyika tu hapo huwa panatokea usumbufu kwa kila kitu, na hapo ni watu wasiofika hata 10,000. Leo uwapeleke familia 100,000 kwa mwendokasi, ni akili au matope? Tunachosisitiza, MAANDALIZI YA ACCOMODATION KWA WAHAMIAJI!
 
Hahahaaaa si ujibu wewe, mimi unanilazimisha ananilisha huyo...mnapenda watu wawe wafata mkumbo...kwangu hiyo neva...
Hapo kwenyewe unafuata mkumbo, akili yako ndogo kuweza kuyachanganua haya na kuyajadili kwa kina.
 
Kaanzishe thread yako kuhusu hilo utajibiwa kama umekosa hoja tulia usome comment wenye akili zao
Watu wenyewe wameshindwa mpaka sasa kujenga ofisi ya saccos yao leo waelewe makao makuu ya nchi kuhamia Dodoma!
 
Hujasoma bandiko lote,hivyo comment yako ina mapungufu ya kimwendokasi. Hiyo madness unayozungumzia wewe ni ya watu kwenda kuishi uwanja wa jamuhuri? Hivi kwa nini mmekuwa watu wa kupiga makofi kwa kila kitu? Mbowe kashauri ni vema wizara chache zikahamia kwa mwaka huu,mwaka kesho hivyohivyo, hii ni kutokana na hali halisi ya Dodoma. Kama hujawahi kuishi au kufika dodoma kaa kimya!
nani amekwambia watu wote wanahamia mwaka huu?
 
Aondoke zake hapa!
ASEEE tunasema wanyakyusa kumdharau mtu
Yy kumleta Lowassa na kumtoa Dr Slaa hakukurupuka?
Lini aliwaomba msamaha watz?
Akili za maiti hizi. Waliomleta Lowassa CHADEMA ni Dr.Silaa na Mbowe. Aliyemwondoa Slaa CHADEMA ni Josephine Mushumbusi baada ya kupiga mpunga wa maana uliowasilishwa na Fisadi la Mafisadi, Dkt. Mwakyembe!
 
Hawa Chadema wanapinga kila kitu wanasahau kuwa walihubiri mabadiliko wakati wa uchaguzi???

Sasa walitaka mabadiliko ya nini wakati kumbe wanapenda mambo yabaki as usual??

Mahakama ya Mafisadi wanapinga

Kuzuia safari za nje wanapinga

Kuhamia Dodoma wanapinga

Kukusanya kodi wanapinga.

Majambazi kukamatwa wanapinga.

Walihubiri mabadiliko kumdanganya nani??

HAWAJAPINGA ILA WANATAKA IFANYIKE KWA UTARATIBU ANGALAU NDANI YA MIAKA MITANO....KWANI NI UWONGO KUWA HATA BAJETI YA MWAKA HUU HAINA FUNGU LA KUHAMIA DODOMA ?
 
Uhamie dodoma uache familia dar maana watoto wanasoma huko mke ana kazi zake huko labda duka kariakoo nae alihamishie dodoma?!kweli mwaka huu watu wataumia sana kisaikolojia.ukiacha mke dar ujue utagongewa tu hakuna namna
 
Magufuli amesema kuhamia Dodoma ni ndani ya miaka 4 iliyobaki ya utawala wake.
Na Mbowe kasema, ni vema basi Wizara chache zikawa zinahamia Dodoma kila Mwaka badala ya hii kasi ya sasa kwa Mawaziri kushindana kukimbilia Dodoma. Rais yuko sahihi, na ushauri wa Mbowe ni sahihi, hakuna aliyepinga kwenda Dodoma!
 
Suala la kuhamia dodoma halikuwepo kwenye Bajeti. Pesa za kuhamia dodoma zinatoka wapi?
 
Hii nchi ni Kama imelaaniwa! Ni kweli JPM kasema Ni mpango wa miaka 4 lakini kuna wapumbavu wanapinga utadhani serikali yote inahamishwa mwaka huu! Na hapo asingeamua kuhama wangekuja Na hoja ya kwa nini serikali haihamii Dodoma![emoji35]
Wewe ni mmoja wa Walaaniwa. Nani kapinga kuhamia dodoma? Kinachopingwa ni hayo Mashindano. PM anaweza kuhamia huko pamoja na TAMISEMI kwa mwaka huu, ila Wizara zinapoamua kufanya mashindano bila kujiandaa hiyo ni kasoro inayopaswa kutolewa tahadhari. Hadi IGP nae anakimbilia Dodoma, ni vema wangejipanga na hili suala lingewekwa kwenye Bajeti kwa mwaka huu w fedha! Muwe mnasoma na kuelewa.
 
Hoja za mbowe hazina mvuto kwa wanyonge kama sisi,hazina hata chembe ya msaada kwa watanzania wa chini.Kama unaona anafaa mwambie magorofa aliojenga Dubai kwa kukwepa kodi za Tanzania azirudishe hapa nchini zisaidie kuwekeza kwenye viwanda watanzania wapate ajira...ndio tutamsaidia kuandamana
Unawafahamu wanyonge wewe? Kaa kimya usisababishe hasira. Acha kabisa kusanifu Wanyonge. Wanyonge ni hawa wanaishindwa kumudu gharama za sukari kutokana na maamuzi ya mwendokasi. Wanyonge ni hawa wanaopunguzwa kwenye viwanda na sehemu nyingine za ajira kwa sababu ya sera mbovu za kiuchumi za serikali hii. Wanyonge walitegemea ajira zaidi, leo hii wanaongezeka mitaani bila ajira. Wanyonge walitegemea kulima na kuuza mazao yao kwenye mahoteli na walaji wengine,leo hii hoteli zinageuzwa hostel kwa kukosa walaji, hivyo matikiti na nyanya za huyu mnyonge vinaozea mashambani. Omba rehema za Mungu kabla hajakuadhibu kwa ku mock wanyonge wa nchi hii!
 
Tuwe wakweli mji wa Dodoma hauwezi ku accomodate watumishi wa wizara zote; kwanza changamoto ya kwanza ni nyumba, wanaobisha hawaijui Dodoma . Unless wakajazane mule kwenye magorofa ya CDA ambayo hayana quality. Poleni watumishi - ndo maana mimi nilijiajiri mapema kukwepa mambo kama haya ya kukurupushana bila maandalizi. Hosp , shule za viwango na hadhi yenu chache ama hazipo, sasa watoto wenu hasa wa primary sijui watasoma wapi
 
Kuna vigezo vinavyotaja ugumu wa kuhama kwa hararaka wala si kuacha kuahamia. Hapo ndipo tunaopinga tuonyeshe jinsi kila kigezo kitawezekana ili kujibu hoja mfano miundombinu itakuwaje.
Humu kumekuwa gulio la ushabiki wa mpira yaani watu kutawaliwa na upenzi na si hali halisi. utadhani watu wanalipwa kwa kutetea upande mmoja dhidi ya mwingine. Tujibu hoja na si kukashifu watu! Tuache kutaja taja majina ya watu kwa kashfa huo ni umbea wa mchana!
 
Back
Top Bottom