Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

Hivi kwa nini Serikaili inataka kuhamishia makao makuu yake Dodoma????
Naona kama huduma za wahitaji walio wengi zinapelekwa mbali sana..nawaza tu
 
Hata wewe unaunga mkono kila kitu kwani we robot? Huna akili ya kwako mwenyewe ukalitafakari kwa kina swala hilo? Kuhamisha watu kwa malaki ghafla bin vuu, watumishi na mabalozi, familia na wanafuzi, hata kama wewe ni zuzu kwa mfano, hebu linganisha Dar na Dom kwa miundo mbinu, huduma, makazi, nk, wapi na wapi?! Muraa, hebu tumia akili kidogo! Nguo za bure za manjano na kijani na cap zisikufanye ujitoe ufahamu!! Bs

Lini JPM alitamka kuwa serikali yote itahama kwa wakati mmoja? Speech is silver, silence is golden
 
Magufuli amesema kuhamia Dodoma ni ndani ya miaka 4 iliyobaki ya utawala wake.

Hii nchi ni Kama imelaaniwa! Ni kweli JPM kasema Ni mpango wa miaka 4 lakini kuna wapumbavu wanapinga utadhani serikali yote inahamishwa mwaka huu! Na hapo asingeamua kuhama wangekuja Na hoja ya kwa nini serikali haihamii Dodoma![emoji35]
 
Hawa wanasiasa wakiwa wanaongea kama kweli wanataka kufikia wananchi wafanye hivyo mbele ya camera,
tena camera za watu maarufu mitandaoni kama akina Millard Ayo maana haya maandishi watu hawasomi, hii thread tu ni uthibitisho tosha sana, watu hawajasumbuka kusoma wameanza kujibu hata bila kujua kama kaongea point au la.
 
O


Miaka zaidi ya 40 serikali ya kuhamia Dodoma from Dar ,imekuwa kama safari ya wana Israel from Egypt to Canaan (Palestine acient land)
Is it a joke?Maamuzi ya kuhamisha capital yalipita kwa ngazi za chama na serikali ya wakati huo iliokuwa madarakani tokea Uhuru na ndio hiyo hiyo imezinduka usingizi wa pono kufanya wajibu wake. Kwa mantiki hiyo sio jambo au swala la kukurupukuka,ila yaonyesha umetanguliza uoga wa maamuzi tulioamua kisheria miaka zaidi ya 40.Stay focus on big picture.
Huo uamuzi ulikuwepo na ulikuwa ni mpango wa miaka kumi. Sasa naona unataka kutekelezwa kwa muda mfupi ndio wasíwasi ilipo. Hata katika ilani ya CCM imesema mpango huo uanze kwa awamu, kujengwe miundo mbinu kwanza na fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi na wizara zitumike kujenga majengo hayo Dodoma.
Mpaka sasa kuna ndugu yangu wao wamehamishwa wiki mbili zilizopita lakini hawajalipwa stahiki zao mpaka leo hii, wanalala kwenye chumba kimoja watu wengi kama wanafunzi wa shule za bweni. Nyumba zenyewe shida kuzipata. Barabara nyingi ni mbovu. Hadi wafanyakazi wengine wanatishia kurudi Dar kwa sababu ya hali ngumu ya maisha. Hali itakuwaje wafanyakazi wengi watakaphamishwa?
 
Hawa wanasiasa wakiwa wanaongea kama kweli wanataka kufikia wananchi wafanye hivyo mbele ya camera,
tena camera za watu maarufu mitandaoni kama akina Millard Ayo maana haya maandishi watu hawasomi, hii thread tu ni uthibitisho tosha sana, watu hawajasumbuka kusoma wameanza kujibu hata bila kujua kama kaongea point au la.
Ndivyo watanzania wangi tulivyo, hatusomi kazi ni kuchangia kwa ushabiki, kwa mtindo huu hii tutaendelea kuwa nyuma sana
 
Hawa Chadema wanapinga kila kitu wanasahau kuwa walihubiri mabadiliko wakati wa uchaguzi???

Sasa walitaka mabadiliko ya nini wakati kumbe wanapenda mambo yabaki as usual??

Mahakama ya Mafisadi wanapinga

Kuzuia safari za nje wanapinga

Kuhamia Dodoma wanapinga

Kukusanya kodi wanapinga.

Majambazi kukamatwa wanapinga.

Walihubiri mabadiliko kumdanganya nani??
Usiwe bwege wewe.Chadema wao ni vichaa wapinge tu bila hoja? Nia ya Mh.rais ni nzuri sana katika utekelezaji ndio shida.sasa wewe unaagiza Polisi akimuona jambazi amuue au traffic police akikamata gari lipo wrong site akamate atoe matairi auze achukue hela hiyo ni akili? Unawaambia watu wahamie Dodoma hukuwandaa kwa chochote na huku unasema watakaobaki dar unawafukuza na majengo ya serikali unauza hiyo ndo akili? Huko ndo kukurupuka wanakosema chadema. Sifa za nini twende kwa mpango mambo yatanyooka. Mwambie apunguze masifa ataumbuka mbele ya safari.
 
Lini JPM alitamka kuwa serikali yote itahama kwa wakati mmoja? Speech is silver, silence is golden
Kama hakusema why all the panic and hoolabaloo to the extent RC wa Ddm anatoa katazo for 14 day, the akafuatia Jennister kwamba the plan is on hold! Ni matamko na kauli ambazo sio well thought thru kabla ya kuropoka; na hiyo ndio sababu kubwa ya distress na mkanganyiko ambao utasababisha mkwamo of gigantic proportions!
 
Huo uamuzi ulikuwepo na ulikuwa ni mpango wa miaka kumi. Sasa naona unataka kutekelezwa kwa muda mfupi ndio wasíwasi ilipo. Hata katika ilani ya CCM imesema mpango huo uanze kwa awamu, kujengwe miundo mbinu kwanza na fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi na wizara zitumike kujenga majengo hayo Dodoma.
Mpaka sasa kuna ndugu yangu wao wamehamishwa wiki mbili zilizopita lakini hawajalipwa stahiki zao mpaka leo hii, wanalala kwenye chumba kimoja watu wengi kama wanafunzi wa shule za bweni. Nyumba zenyewe shida kuzipata. Barabara nyingi ni mbovu. Hadi wafanyakazi wengine wanatishia kurudi Dar kwa sababu ya hali ngumu ya maisha. Hali itakuwaje wafanyakazi wengi watakaphamishwa?

Mkuu nimekusoma,ni namna gani ya kufanikisha uhamiaji wa wafanya kazi toka Dar kuja Capital Dodoma.Kama wizara yenye watendaji wakumwaga hazionyeshi kuwa na smart move sababu muulize waziri wa Elimu.Kilicho wazi ni woga usiokuwa na mipaka kwa sababu zilizo wazi.
 
Yaani nyie wafuasi wa CCM mmeshalishwa limbwata.... MTU anaekosoa sio mpingaji ...MTU anaekosoa anamapenzi mema kuliko anaepinga koz anaepinga hataki MTU asonge mbele!!! Ila mbowe sio mpingaji kwa sababu anasaidia JPM kuona mapungufu yake!!!
 
Mbowe using'ang'anie Dar! Pia kumbuka tokea enzi za mwalimu mipango na mikakati ya kuhamia Dom ilikuwepo na ilikuwa inapangwa kama mipango imekamilika mnasubili nin kuhama. Dar?
 
Mh.Raisi Hajasema Wizara zihame siku moja ila wanachofanya ni Wizara na Taasisi zilizoonyesha Nia ya Kweli kuna kuhama
 
Yaani awashangaa wanaoshobokea kwenda Dodoma, utafikiri hawana ubongo. Kwani DSm inawaka moto hadi tukurupuke kiasi hiki? Aibu gani hii jamani?
Yote hayo yanafanyika kutimiza ndoto za mwalimu ..............!!
 
Back
Top Bottom