Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

Hawa Chadema wanapinga kila kitu wanasahau kuwa walihubiri mabadiliko wakati wa uchaguzi???

Sasa walitaka mabadiliko ya nini wakati kumbe wanapenda mambo yabaki as usual??

Mahakama ya Mafisadi wanapinga

Kuzuia safari za nje wanapinga

Kuhamia Dodoma wanapinga

Kukusanya kodi wanapinga.

Majambazi kukamatwa wanapinga.

Walihubiri mabadiliko kumdanganya nani??
Unadhani mabadiliko ni kuendesha nchi kwa matamko
 
Binafsi napongeza uamuzi wa kutekeleza kwa vitendo azma ya kuhamishia serikali Dodoma.

Pamoja na maendeleo ya teknolojia lakini hakuna haja ya makao makuu ya serikali kuongeza msongamano kwenye mji ambao location yake inaufanya uwe na msongamano mkubwa wa shughuli za kibiashara.

Japo siishi Dar es Salaam lakini naweza kusema hilo jiji limesheheni kupita kiasi, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wenyeji na wageni.

Kuhama Dar ina maana wanasaidia wananchi wanaoenda kutafuta huduma kwenye ofisi za serikali kuepuka adha ya msongamano na watu wa biashara hapo Dar.

Lakini kama alivyosema Mbowe umakini unahitajika ili kitoathiri sana wafanyakazi na shughuli za serikali. Hata hivyo ni vigumu kukadiria kwa uhakika athari zinazoweza kutokea.

Wengi wa hao wanaohama ndio watekelezaji wa mipango ya uhamaji na "ukiwabembeleza" watakwamisha kwa namna moja au nyingine huo mpango ili tu waendelee kubaki pale walipopazoea...

Kutokana na hilo naunga mkono moja kwa moja mipango ya haraka inayoendelea kufanyika kuhamishia serikali Dodoma...
 
Hakuna sehemu niliokutukana

Kaka hakuna nilikokutukana hata kama naishi kama ndege lakini hutanishawishi kuhusu malalamiko yako dhidi ya kuhamia Dodoma.Kwa watu wenye kufikilia ulitakiwa kutoa hoja kwa nini unapinga kuhamia lete hoja hapa. unaweza kutukana lakini ukaumbuka mwenyewe.watanzania lazima tubadilike kama SABODO anavyobadilika.UKWELI UBAKI KUWA UKWELI.
Unasema Mbowe hana uwezo wa kuchangia spare parts kwani hujui kuwa analipa kodi na ni haki yake kuhoji matumizi ya kodi yake? Wewe hulipi kodi ndio maana unaishi kwa ndio mzee
 
Pole sana kwa sababu ili unishinde njoo na point kama technically sio kudaka vya wenzako hapa hutapita
 
Watu wengi hawajui kwa nini wazungu huwa wanasema *"LIFE BEGINS AT 40".*
Yaani maisha yako ya kweli yataanza ukifika umri wa Miaka 40. Wakati ambapo unatakiwa uwe na elimu uliyoihitaji.. Uwe na familia yako tayari.. Uwe na kwako tayari siyo umepanga bado.. Uwe na usafiri binafsi.. Uwe na kitu chako cha kukuingizia pesa na si kutegemea ajira peke yake. *At 40!!*

*At 40* inabidi uwe unaishi. Siyo ndio unaanza kujaribu hiki na kile.
*At 40* inabidi uwe unasomesha zaidi kuliko kusoma wewe japo kuongeza maarifa ni vizuri.
*At 40* unatakiwa uwe umeshapata exposure kusafiri huku na kule dunia hii kujua wengine walioendelea zaidi wanaishi vipi na wewe ufanyeje?
*At 40* utakuwa unaomba nauli kwa baba na mama kwani?

Sasa hivi vitu haviji ukiwa upoupo tu hutafuti fursa za kukusaidia kuwa na maisha tofauti upo tu una LIKE kila kitu facebook na Instagram unatuma tu picha za ajali za mabasi zikikosekana unatuma za migomo ya madereva mgomo ukiisha unatuma za mafuriko kama mvua zimeisha unatuma picha za Lowassa yaani umekuwa mtumwa wa simu. Ikikosa network unalalamikia kampuni ya simu utafikiri hiyo network unafanyia kitu cha maana. Gallery yako imejaa vitu vya ajabuajabu tu. Havikufikishi popote na umri unazidi kwenda unazidi kusogea miaka 40 hivi hivi. Maisha ya kweli yataanza ukiwa na miaka 40. Wakati ambapo watoto wako hawatakula LIKES zako za instagram bali wanahitaji chakula. Wanahitaji ada. Wanahitaji maisha bora. Wewe unasubiri maisha bora CCM ndio wakupe. Wasipokupa unataka UKAWA waje wakupe ukiwa umekaa Instagram una LIKE picha za Wema Sepetu. Umeshajua wema akifika miaka 40 atakuwaje? Ulishajiuliza wanamuziki waliovuma miaka 15 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 25 hivi au 30 wakati huo wana miaka mingapi na wako wapi sasa hivi. You see? Unayemfuatilia kila siku kavaaje kaamkaje katembea na nani hakusaidii kuwa na maisha mazuri. Maisha bora hayaji ukiwa unafatilia nyimbo gani zimetoka udownload. Maisha bora hayaji kwa KU-ENTERTAIN brain yako bali kwa kuifikirisha akili na kufanya mambo ambayo wachache tu ndo wanafanya.

Kwani wanasoka wangapi wako kama Beckham
Wanamuziki wangapi wako kama Kirk Franklin
Wacheza Tennis wangapu wako kama Roger Federer? Unadhani amekuwa champion akiwa amekaa na TECNO chumbani ana comment kuhusu migomo? No. Alikuwa ana-hussle wakati wengine wanachat.

Seriously. Diamond unaye mfollow anafanya kazi hivyo. Anatoka studio saa saba usiku wewe uko kwenye page yake una LIKE. Huwezi kuona kuwa uko tofauti. Anaandaa maisha akifika miaka 40 awe na kila kitu wewe utakuwa unalalamikia network ya tigo na kutuma picha za sijui gari limegonga treni. Kwa hiyo wewe ndo NIPASHE sasa hivi?

Anyway. Kuwa serious na maisha yako angalau basi kwa ajili ya watoto wako na wajukuu zako.
Aisee huyu mzazi wetu alifanya jambo la maana . Au unadhani watazikuta hizo comments na LIKES zako? No. Wanapaswa wakute nyumba, viwanja, account za benki zinazopumua. Siyo account inaingiaga mshahara tu halafu by tarehe 10 iko empty ushakomba kila kitu!!!! Wanatakiwa wakute assets za maana angalau . Siyo rundo la CD za bongo movie ambazo hazikusaidii wewe wala wao.

Siku zilizobaki kumaliza mwaka huu 2016 una mikakati gani kuweka msingi wa maisha tofauti sana na kuhakikisha ufikapo umri wa miaka 40?
Au bado unategemea mshahara wa laki 6 (tena hapo kabla ya makato) uje ubadili maisha yako.
Kwa waajiriwa, Microsoft ya Bill Gates inapunguza wafanyakazi 800. Kama ulikuwa hujui. Unadhani kampuni yako ndo utakaa hapo milele???
Be carefully ndugu.

" KUZALIWA MASIKINI SI KOSA BUT KUFA MASIKINI NI DHAMBI"
 
Mbowe siku hizi anavutia bangi uvungu wa kitanda na anashushia kiroba chenye radha ya pasheni ndio maana haish kubwabwaja utumbo.
Hoja hupingwa kwa hoja siyo porojo Mbowe ameeleza sababu za msingi uamuzi wa serikali kuhamia dodoma ulikuwa wa kukurupuka
 
Binafsi hawa waUPINZANI washanichosha sasa,nakubali kupinga au kukosoa jambo ni jambo jema na la msingi sana,TATIZO la hawa wao wanapinga/kukosoa tu bila kutoa ushahuri au way through.sasa manake nini!!!!kosoa/pinga kisha lete suluhu.....tunahitaji kusonga mbele na sio kubaki tuliko au kurudi nyuma.
 
Binafsi hawa waUPINZANI washanichosha sasa,nakubali kupinga au kukosoa jambo ni jambo jema na la msingi sana,TATIZO la hawa wao wanapinga/kukosoa tu bila kutoa ushahuri au way through.sasa manake nini!!!!kosoa/pinga kisha lete suluhu.....tunahitaji kusonga mbele na sio kubaki tuliko au kurudi nyuma.

Jibu maswali mawili kuhusu uamuzi wa serikali kuhamia dodoma kama siyo wa kukurupuka.
1=gharama za kuhamisha wizara hizo pesa zinatoka wapi?
2==Hizo pesa zilipitishwa bunge lipi na lini?
 
Jibu maswali mawili kuhusu uamuzi wa serikali kuhamia dodoma kama siyo wa kukurupuka.
1=gharama za kuhamisha wizara hizo pesa zinatoka wapi?
2==Hizo pesa zilipitishwa bunge lipi na lini?
Sawa kwa mtazamo wako,sema basi nini kifanyike kuhusu kuhamia huko Dom na wahamie lini.
 
Sawa kwa mtazamo wako,sema basi nini kifanyike kuhusu kuhamia huko Dom na wahamie lini.
Ambacho kinatakiwa kufanya serikali inatakiwa kuwasilisha muswada bungeni pamoja bajeti ya kuhamia dodoma na kuanza maandalizi taratibu mpaka zoezi litapokamilika siyo kama inavyofanyika kila waziri anatoa kauli za kukurupuka kuhusu kuhamia dodoma
 
Mbowe hapo umezingua

Mpango wa kuhamia Dodoma ni positive kabisa.......kwa maana ya Maono ya mbali

Na change yoyote lazima iwe na resistance..Ili kuweza ku drive change you need to have some sort of madness....Kitu ambacho Bro Magu ana practice now

Sasa Mbowe...sio kila kitu unapinga...sometimes sikusomi kabisaaaaa..Pongeza mara zingine.....kama king of Tz Politics Lowasa

Faida ya Kupongeza ni kupunguza tension na kufungua mwanya wa concessus kwa ajili ya Maendeleo ya Watanzania

CCM wanayo serikali...Huwezi kupambana nao at close ends...Compromise...Compromise

Mbowe be wise meeeeen

Sidhani kama amepinga serikali kuhamia Dodoma

Nilivyomuelewa mimi ni kuwa, mpango wa kibajeti na kimiundombinu haukuandaliwa bali ni mtu tu limemjia kichwani na kulisema!!

Theoretically kwa kusema tu yaweza kuwa na ndivyo imekuwa miaka yote ktk awamu zote, lakini practically kwa muda wa miaka mitatu HAIWEZEKANI!!

Unajua Nigeria iliwachukua muda gani kuhamisha makao ya serikali toka Lagos kwenda Abuja?

Na unafikiri ilifanyika kwa matamko ya barabarani tu?

No, it was through specific strategies and scientific laid down plans!!

Ndiyo, ni mpango ulioasisiwa na baba wa taifa hayati Mwl J.K Nyerere miaka zaidi ya 40 iliyopita

Lakini umebaki kuwa wa kinadharia zaidi kuliko matendo!!

Huyu naye, from no where anatupa miaka mitatu lakini huku akiwa hana mpango maalumu unaosomeka na kueleweka na kila mwananchi.

The ONE MAN SHOW inaendelea na atachoka si muda na kurudi kwenye bussiness as usual kwa sbb CCM ni ile ile, haijabadilika!!

Ushahidi wa kuthibitisha hili ni bajeti ya mwaka huu wa fedha wa 2016/2017, ni wapi tumeambiwa labda wizara hii na hii na pengine idara flani flani zitahamia Dodoma pamoja na mafungu yake ya fedha??

Jibu ni HAKUNA na kama hiyo kitu ipo, basi ndugu yangu Freeland hebu tuwekee hapa.

Na kama hakuna, hili limetokea wapi ghafla tu from nowhere??
 
Hawa Chadema wanapinga kila kitu wanasahau kuwa walihubiri mabadiliko wakati wa uchaguzi???

Sasa walitaka mabadiliko ya nini wakati kumbe wanapenda mambo yabaki as usual??

Mahakama ya Mafisadi wanapinga

Kuzuia safari za nje wanapinga

Kuhamia Dodoma wanapinga

Kukusanya kodi wanapinga.

Majambazi kukamatwa wanapinga.

Walihubiri mabadiliko kumdanganya nani??
 
Back
Top Bottom