Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

Mbowe: Mpango wa kuhamia Dodoma ni wa kukurupuka

Mbowe hapo umezingua

Mpango wa kuhamia Dodoma ni positive kabisa.......kwa maana ya Maono ya mbali

Na change yoyote lazima iwe na resistance..Ili kuweza ku drive change you need to have some sort of madness....Kitu ambacho Bro Magu ana practice now

Sasa Mbowe...sio kila kitu unapinga...sometimes sikusomi kabisaaaaa..Pongeza mara zingine.....kama king of Tz Politics Lowasa

Faida ya Kupongeza ni kupunguza tension na kufungua mwanya wa concessus kwa ajili ya Maendeleo ya Watanzania

CCM wanayo serikali...Huwezi kupambana nao at close ends...Compromise...Compromise

Mbowe be wise meeeeen

Kabla hujamwambia Mbowe amezingua ilibidi utuambie kuwa kivipi mpango wa kuhamia Dodoma ni positive? Njoo na supporting arguments ambazo zitatufanya tuamini kuwa Mbowe amezingua kama yeye alivyoainisha sababu zake.
 
Mzee mbowe naona ungeshauri namna yakutekeleza mpango wa raisi nasiyo kukosoa moja kwa moja kama siyo jambo jema, tumeshuhudi mipango mingi ya muda mrefu haitekelezeki 100% hii yakukurupuka kwa sasa inatija tushauri namna gani ya kututekeleze japo lazima tukiri changamoto hazikwepeki
 
mwendo kasi wa kuamia dodoma, waangalie sana wasije wakaja vunjika miguu
 
Kwani "Kukurupuka" maana yake nini? kuna watu mnaweza kumbishia mbowe bila kuelewa maana ya kukurupuka. Yule anayepingana na kauli ya mbowe, aweke maana ya kukurupuka hapa ili tuone kama ilichofanya serikali ni kukurupuka au la.
 
Mbowe ameongea kwa mifano na hoja, wewe unajibu kwa ngonjera. Hebu onesha jinsi huo mpango ulivyo positive huku ukimrejea Mbowe kwa yale aliyoyasema kuhusu BAJETI, USUMBUFU, FAMILIA NA MIFUMO YA KIUCHUNGUZI YA POLISI

hayo aliyoyataja mbowe hayafai ku dis credit idea nzima ya kuhamia Dodoma...ni vitu vidogo ...changamoto zinazoweza kufanyiwa kazi with time....

Mh Rais amesema muda wa kuhamia ni sasa hadi 2020....Mh Rais yuko sahihi katika hili na ninampongeza

Inabidi ifike wakati tubadili aina ya siasa tunzaofanya...There are good things ambazo hatuhitaji kuzipinga tu....tunajiweka mahala pabaya...Better to kunyamaza
 
Kwani "Kukurupuka" maana yake nini? kuna watu mnaweza kumbishia mbowe bila kuelewa maana ya kukurupuka. Yule anayepingana na kauli ya mbowe, aweke maana ya kukurupuka hapa ili tuone kama ilichofanya serikali ni kukurupuka au la.

kukurupuka ni kufanya kitu kwa mhemko pasipo kuwa na plan hapo mwanzoni

suala la Dodoma liko kwenye plan ya nchi yetu Tangu Enzi za nyerere..Ndio maana CDA iliundwa........

Ilani ya CCM ya 2015 imeliongelea hili pia

why tumlaumu Mh Rais

Tusiwe this kind of people.......Ili wananchi watuelewe inapaswa sometimes tuongee Lugha yao...we need to change

Mbowe amechoka.....he keeps doing the same thing..same way...expecting different results
 
hayo aliyoyataja mbowe hayafai ku dis credit idea nzima ya kuhamia Dodoma...ni vitu vidogo ...changamoto zinazoweza kufanyiwa kazi with time....

Mh Rais amesema muda wa kuhamia ni sasa hadi 2020....Mh Rais yuko sahihi katika hili na ninampongeza

Inabidi ifike wakati tubadili aina ya siasa tunzaofanya...There are good things ambazo hatuhitaji kuzipinga tu....tunajiweka mahala pabaya...Better to kunyamaza
Umetoka mfano kwamba Dodoma haijajipanga ku - accommodate idadi ya watu wanaoelekea huko. Familia zitahitaji kuhamisha watoto, miundombinu ya kazi na kadhalika. Rais sawa kasema 2020, lakini kuna ambao wameshaadhimia kwenda mwezi ujao, hayo kwako ni mambo madogo madogo?

Well then, hiyo IDEA NZIMA ya kuhamia Dodoma bila bajeti maalum, imelenga kuleta positive impact gani kiasi iwe ghafla hivi?
 
Hata wewe unaunga mkono kila kitu kwani we robot? Huna akili ya kwako mwenyewe ukalitafakari kwa kina swala hilo? Kuhamisha watu kwa malaki ghafla bin vuu, watumishi na mabalozi, familia na wanafuzi, hata kama wewe ni zuzu kwa mfano, hebu linganisha Dar na Dom kwa miundo mbinu, huduma, makazi, nk, wapi na wapi?! Muraa, hebu tumia akili kidogo! Nguo za bure za manjano na kijani na cap zisikufanye ujitoe ufahamu!! Bs
MTK acha kuongea aibu,Lazima tujipambanue ,tujifunue,kuhamia dodoma ,itakuza uchumi wa nchi kwa asilimia kubwa.Maendeleo kwenye secta ya usafilishaji yatakuwa makubwa,Dodoma itachangia pato la Taifa kwenye sector zote kama vile kilimo,ufugaji,maendeleo ya ardhi na Makazi.Asietaka kuhamia Dodoma yeye abaki tu.
 
yeah...kuna uwezekano kukatokea adha na usumbufu mkubwa zaidi ya ule wa maamuzi ya sukari.

usumbufu kama huo ni hatari sana kwa mustakabali wa nchi kubakia a cohesive unit.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitotekeleza mpango wa kuhamia Dodoma kwani ni wa kukurupuka.

Msimamo huo umetolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alipozungumza na gazeti hili wakati wa kutoa heshima za mwisho za aliyekuwa mpigapicha mwandamizi wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga ambaye anatarajiwa kuzikwa leo huko Kwimba, Mwanza.

“Serikali inaendeshwa kwa kukurupuka. Ni mpango usiotekelezeka,” alisema Mbowe.

Alisema uhamaji unaotekelezwa sasa haukuwa na maandalizi wala mkakati kwenye ilani ya chama tawala wala Bajeti ya Serikali hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kukwama huko mbele.

Miongoni mwa vitu vinavyoufanya mpango huo usitekelezeke kwa ufanisi, kwa maoni yake, alisema miundombinu ya kutosheleza watendaji wote na wadau wengine muhimu ambao watalazimika kufuata huduma muhimu za wizara na idara za Serikali.

“Huku ni kuwaumiza wananchi. Watumishi wa Serikali, wanahabari na wadau wengine wakihama wote watapata wapi malazi katika mji ule?”

Muda mfupi baada ya kukabidhiwa majukumu ya kuiongoza CCM, Julai 23, Rais John Magufuli alieleza nia yake ya kutekeleza uhamisho wa makao ya Serikali kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma na kwamba atahakikisha, ndani ya miaka minne anatimiza ndoto hiyo ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya tangu mwaka 1973.

Siku moja baadaye, akihutubia kwenye hafla ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitangaza kuhamia mjini humo Septemba na kusema kuwa wizara nyingine zitamfuata.

Tangu kutolewa kwa matamko hayo ya viongozi waandamizi wa Serikali; wizara, taasisi, mashirika ya umma, idara na baadhi ya ofisi binafsi, mabalozi na wanadiplomasia zimeanza kuandaa mazingira ya utekelezaji huo.

Lakini, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alionyesha wasiwasi wake juu ya umakini wa Serikali kutekeleza azma hiyo akisema kutakuwa na usumbufu mkubwa kwa watumishi na familia zao suala linaloweza kupunguza morali yao ya kazi. “Watu wana familia zao. Watoto wanasoma... Dodoma hakuna shule za kutosha watoto watakaohama na wazazi wao.”

Alisema wakati wazo hilo linatolewa na kuungwa mkono enzi za Mwalimu Nyerere kulikuwa na sababu za msingi lakini hivi sasa kuna mabadiliko makubwa yaliyochagizwa na maendeleo ya sayansi na teknolojia. Alisema wakati huo mindombinu ya mawasiliano haikuwa rafiki tofauti na iliyopo sasa inayowezesha watu walioko New York, Marekani kufanya mkutano na wenzao waliopo popote duniani kwa kutumia miutano kwa njia ya masafa. “Sababu zimepitwa na wakati,” alisisitiza.

Alishauri, mpango huo ungetekelezwa kwa utaratibu maalumu, akitoa mfano kwa wizara moja au mbili kuhama kwa kila mwaka mpaka zitakapokamilika ili kupunguza gharama zisizo na ulazima.

Alisema kuhamisha wizara siyo waziri au katibu mkuu pekee, bali ni watumishi wote na miundombinu yote iliyopo ambayo ni muhimu kwa utekelezaji wa majukumu yake: “Kwa mfano, Wizara ya Kilimo ina watumishi 2,000 na maelfu ya mafaili yenye taarifa za kiutendaji… unawahamishaje watu wote hawa na mindombinu iliyopo unaifanyaje? Namshangaa IGP anaposema anahama wakati mifumo yote ya uchunguzi na taarifa imejengwa hapa kwa kutumia mabilioni ya fedha za wananchi.”

Wiki iliyopita, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Polisi, Nsato Marijani alisema jeshi hilo litahamia Dodoma mwezi huu na watakaohusika ni Inspekta Jenerali na baadhi ya makamishna.
 
Cha ajabu ni kwmaba mda si mrefu nimesoma HABARILEO likiandika Lowasa ampongeza raisi Magufulu kwa kazi yake, na pia amechukulia hilo hamisho kua ni jambo zuri, na pia akatoa ushauri kwamba Magufuli afanye taratibu kwa huo hamisho. Angalao leo ndio nieona maneno mazuri ya upinzani hasa kutoka kwa Lowasa, akitoa pongezi pia pia akitoa ushauri
 
Nampongeza sana Mzee Mbowe kwa kuwa na uelewa mkubwa pongezi zangu za dhati zikufikie, wanaosema mbowe amekosea nadhani ni wasela hawana familia endapo kama wangekuwa na familia wangekubaliana na mawazo ya Mbowe , binafsi sipingi suala la kuhamia Dom isipokuwa kuna haja ya kuwashilikisha wataaram ili wasaidie katika kushauri juu ya jambo hili. Kuhamia Dodoma kutawaumiza watumishi wa umma kwani watumishi wengi wamesettle na kwakweli wengi wapo kwenye mikopo ambayo kwa namna moja au nyingine walikopa ili kujistili wao na watoto wao na wake/waume zao sasa gafla unasema kesho ameni tena bila ufafanuzi mzuri kwakweli watumishi wa serikali wanalia machozi ya damu wewe unayesema mpango huu utekelezwe haraka nadhani ni mtu wa kijiweni na pengine hauna upendo na familia yako.
pili jambo hili halipo kwenye bajeti pia tunavyo vipaumbele vingi kwa sasa kama vile shule, hospitali, maji nk hivyo sizani kama kuhamisha watumishi wote kwa sasa ni jambo ambalo limezingatia tahaluma ya uchumi. swali: mshauri wa uchumi wa mheshimiwa yuko wapi?

Hongera mzee mbowe pia nakushauri msajili kituo cha televisheni hii itawasaidia katika kuelimisha wananchi kupitia televisheni yenu maana kwa sasa mtakosa pa kusemea
 
Huu mpango wa kuhamia Dodoma kwa gafla hivi unaweza kuzalisha matatizo kuliko faida..kwa wanaokumbuka suala la sukari yalitolewa maagizo mengi ikiwemo ya kugawa sukari bure ila mwisho wa siku bei iliongezeka kuliko kabla ya yale matukio..
 
Nampongeza sana Mzee Mbowe kwa kuwa na uelewa mkubwa pongezi zangu za dhati zikufikie, wanaosema mbowe amekosea nadhani ni wasela hawana familia endapo kama wangekuwa na familia wangekubaliana na mawazo ya Mbowe , binafsi sipingi suala la kuhamia Dom isipokuwa kuna haja ya kuwashilikisha wataaram ili wasaidie katika kushauri juu ya jambo hili. Kuhamia Dodoma kutawaumiza watumishi wa umma kwani watumishi wengi wamesettle na kwakweli wengi wapo kwenye mikopo ambayo kwa namna moja au nyingine walikopa ili kujistili wao na watoto wao na wake/waume zao sasa gafla unasema kesho ameni tena bila ufafanuzi mzuri kwakweli watumishi wa serikali wanalia machozi ya damu wewe unayesema mpango huu utekelezwe haraka nadhani ni mtu wa kijiweni na pengine hauna upendo na familia yako.
pili jambo hili halipo kwenye bajeti pia tunavyo vipaumbele vingi kwa sasa kama vile shule, hospitali, maji nk hivyo sizani kama kuhamisha watumishi wote kwa sasa ni jambo ambalo limezingatia tahaluma ya uchumi. swali: mshauri wa uchumi wa mheshimiwa yuko wapi?

Hongera mzee mbowe pia nakushauri msajili kituo cha televisheni hii itawasaidia katika kuelimisha wananchi kupitia televisheni yenu maana kwa sasa mtakosa pa kusemea
Awamu hii imekua sio rafiki kwa watumishi wa umma..ila matokeo ya uonevu kwa watumishi wa umma yataonekana 2020
 
Hawa Chadema wanapinga kila kitu wanasahau kuwa walihubiri mabadiliko wakati wa uchaguzi???

Sasa walitaka mabadiliko ya nini wakati kumbe wanapenda mambo yabaki as usual??

Mahakama ya Mafisadi wanapinga

Kuzuia safari za nje wanapinga

Kuhamia Dodoma wanapinga

Kukusanya kodi wanapinga.

Majambazi kukamatwa wanapinga.

Walihubiri mabadiliko kumdanganya nani??
Tatizo ni kuwa HUELEWI KITU,IT'S BETTER TO BE QUITE
 
Back
Top Bottom