Mbowe: Lowassa ni dhaifu, ni bubu

Mbowe: Lowassa ni dhaifu, ni bubu

Status
Not open for further replies.
.
Yani umejuaje Kababu....tuliwaandikia thread humu mwanzo kabisa..tukifikilia watakuwa SMART kungamua kusudio la MCHEZA SINDIMBA WA CCM, wao wakaganda kusubilia uenda akaja kwao.Na CCM kwa kung'amua hilo wakawa wana nunua muda ili wasije Wakatengeneza mpasuko kwa gharama ya huyo Mwanaccm wao.

CDM walikuwa na nafasi njema sana ya KUMKANA mtajwa KABLA ye yeye kuja na DONGO la ATOHAMA CCM...wakati macho ya WATANZANIA nzima walikuwa wanajua CCM watamfukuza MWANACHAMA WAKE huyo na KUNDI lake.Yani ata kama PLAN hiyo ilikuwepo UKIMYA wa CDM/UKAWA kupangua KUTOKUWA TAYARI kumpokea MWANACCM huyo na kundi lake unaweza kuwa ULIVULUGA PLAN yote ya CCM na hivyo uenda ikajikuta INATAFUTA PLAN B.

Yani sipati picha kama CDM/UKaWA haya anayosema Kamanda wao MBOWE angeyamwaga mapema Kabisa kabla LOWASA ajasema leo hii CDM wangekuwa vifua mbele.Matokeo yake yakawa ya FISI kutembea nyuma ya mtu kusubilia MKONO wa binadamu UDONDOKE.Wamekosa POINTI nyingi sana tena sana ...manake kwenye SWALA la UFISADI wangekuwa MBELE ya CCM kwa kuonyesha kuwa ATA pale RUMORS zilipokuwa ZINAIBUKA kuwa Kuna WANACCM kindakindaki wanataka kufukuzwa na hivyo wanategemewa kupokewa na CDM/UKAWA wao wangekuwa MBELE kuwa WALIKWISHA kataa hawapokei MAFISADI na makapi ya CCM.

Tuliwaonya sana mwanzoni semeni mapema ...wakakaa kimya UKICHEKA NA KIMA UTAVUNA MABUA.Nilitoa thread hii hapa Tetesi za CHADEMA/UKAWA kupokea Watakaotemwa Na Kaango La CCM Hakika Ni Kweli.
List of shame ilitangazwa September 2007 huyo unayemtaja yumo au hayumo?

1. Dr. Daudi T.S. Balali - sasa marehemu ?
2. Andrew J. Chenge - mgombea Ubunge kupitia CCM, Bariadi.
3. Basil P. Mramba - mgombea ubunge kupitia CCM, Rombo.
4. Gray S. Mgonja - Kaibu Mkuu mstaafu, Hazina.
5. Patrick P. R. Rutabanzibwa - Katibu Mkuu mstaafu ?
6. Nazir Karamagi - Waziri mstaafu.
7. Nimrod Mkono - mgombea ubunge kupitia CCM, Musoma vijijini
8. Rostamu Azizi - mgombea ubunge kupitia CCM, Igunga.
9. Edward Lowassa - mgombea ubunge kupitia CCM, Monduli.
10. Benjamin W. Mkapa - Raisi mstaafu, CCM.
11. Jakaya Mrisho Kikwete - mgombea Uraisi kupitia CCM
 
Lowasa anaitwa fisadi ,mimi sikatai ila shida ni wale wanaomwita fisadi ,wao ni akina nani kama yeye ni fisadi.
Naomba mtu mmoja mwenye kumbukumbu nzuri aorodheshe matukio ya ufisadi ya kutisha baada ya Lowasa kujiuzulu na tuone ni nani hakuwa ndani ya serikali au bunge anaegombea uraisi.
Na kama alikuepo alifanya nini kuonyesha jamii kuwa hakupendezwa na hayo.
 
Nani alijitoa kwenye serikali na kwenda kwenye media na kusema mimi najiuzulu nafasi yangu ndani ya serikali hii kwani siwezi kuwa sehemu yake kwa ufisad huu.
Aidha wa escrow au wowote ili sasa aje nasi tujue huyu si sehemu ya uchafu
 
Kama nimemwelewa Mbowe vizuri haimaanishi anataka achaguliwe yeye badala ya EL.
 
Dj Clay F akiwa katika ubora wake. Dj asidanganye watu, Lowassa ilikuwa tumaini la UKAWA, baada ya kutoa msimamo kuwa hawezi kuhama CCM, ndipo Dj Clay F anakuja na huu utumbo.
 
Lowasa anaitwa fisadi ,mimi sikatai ila shida ni wale wanaomwita fisadi ,wao ni akina nani kama yeye ni fisadi.
Naomba mtu mmoja mwenye kumbukumbu nzuri aorodheshe matukio ya ufisadi ya kutisha baada ya Lowasa kujiuzulu na tuone ni nani hakuwa ndani ya serikali au bunge anaegombea uraisi.
Na kama alikuepo alifanya nini kuonyesha jamii kuwa hakupendezwa na hayo.

Ndio maana wenye Akili tunasema mwisho wa ccm ni october
 
Chama cha mapinduzi kimejaa wahuni,mwaka 2005 ni Lowassa na jk walitembea nchi nzima wakisema " Maisha bora kwa kila mtanzania"
Mwaka 2010 wakaja na Ari mpya,nguvu,mpya na kasi mpya walimu waliokuwa hawana nyumba za kukaa hafi leo shida ni ileilel
Uhuni uleule wa watu walewale,wanaanza nangojera za " safari ya matumaini"


Watanzania hatuhitaji kutiwa matumaini,kwani nchi inakila kitu,

Wakati watoto walikuwa wanashinda njaa shuleni Lowassa alikuwa waziri,

Wakati watoto wa shule wakikosa vitabu,madarasa na madawati Lowassa alikuwepo,

Wakati umeme wa mgawo na wakutegemea mvua Lowassa aliluwa waziri,

Wakati ajira za watanzania zikizamishwa kwa kuuzwa viwanda vyetu vya nguo,viatu,ngozi,sukari Lowassa alikuwepo,

Wakati nchi ikiendelea kukumbwa na rushwa,Lowassa alikuwepo,

Wakati Azimio la Arusha likivunjwa zanzibar ambalo ndilo liliwadhibiti wezi wa ccm Lowassa alikuwepo,

Wakati ccm ikishindwa kukusanya kodi,na kuendelea kukopa,Lowassa alikuwepo na kwa kujua mwelekeo wa Lowassa,juzi amesema" tunaweza kutumia geai kukopa fedha ulaya"


Huyu anaanza kuwaza kukopa,watanzania tutegemee nini,kwa rais aliyemiongoni mwa waovu na anaunga mkono kukopa huku deni la Taufa likiongezeka?
 
Marafiki zake ni hao akina MSABAHA ,KARAMAI ,ROSTAM, CHENGE,sasa unategemea nin hapo ,KARAMAI mfano si yule jamaa alienda kuingia mikataba wa BUZWAGI kule uingereza,ilyo mpelekea ZITTO kufukuzwa bungeni pia nasikia ni mwanahisa wa BARIC , hao ndo marafiki wa LOWASA, inasikitisha kweli

Mkuu hapo si nchi itauzwa kwa matajiri na wahindi.
 
"Ikulu ya watanzania inahitaji maskini mwemzao,si mtu anayetaka kuwa rais ili aongeze utajiri kutoka ng'ombe 1000 hadi 10,000!


Akiwa anajua kuwa magonjwa ni chanzo kikubwa cha umaskini,akiwa waziri wa maji,yako wapi mahi Lindi,mtwara,Dar es salaam,morogoro,Tanga,kigoma,Tabora,Mwanza,Mbeya,Magu,shinyanga Lowassa yako wapi majisafi na salama? Au visima ambavyo kila mtu anachimba ndio maji uliyoleta?


Magu tu na Bunda iliyokaribu na ziwa viktoria ilikushinda sembuse Ikulu?

Hatuhitaji dalali wa ikulu
 
Mh.Mbowe amenukuliwa na Tanzania Daima akimchana Mh.Lowasa kuwa ni mgombea dhaifu na bubu wa kukemea ufisadi.

Amesema UKAWA hawawezi kuwa nae,hivyo asiwatishe CCM kuwa ana nafasi UKAWA.

Source:Tanzania Daima page no.5

Eti chanzo cha habari ni gazeti la Tanzania daima....!! Kwi kwi kwi kwi kwi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom