Uchaguzi 2020 Mbowe itampa wakati mgumu sana kumnadi Lissu

Ndugu zangu,

Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa siku ya leo.

Katika uchaguzi ambao niliufuatilia kwa karibu kubwa sana tangia nianze kufuatilia siasa na wanasiasa, basi ulikuwa ule wa 2015. Ulikuwa uchaguzi wa kipekee sana kuwahi kutokea hapa nchini, na ulikuwa uchaguzi mgumu sana kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ila CCM walicheza karata kubwa sana ya kumweka Mh. Magufuli. Kwa kutumia rekodi za nyuma za umahili wake wa uchapazi kazi katika kila wizara aliyoteuliwa, ilinifanya kura yangu nimpe huyu ndugu. Na kama CCM wangempitisha Membe, basi kura yangu ingeenda kwa Mh. Lowasa. Na itachukua miaka mingi sana kuwa na uchaguzi kama ule.

Kamari ambayo waliicheza Ukawa, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kumkaribisa Mh. Lowasa (), Mh. Mbowe alikuwa na furaha mno na confidence kubwa sana huku alikuwa anajua kabisa Lowasa anaenda kuingia Ikulu, kulingana na nyota ya siasa amabayo Lowasa alikuwa nayo ambayo ilisababishwa na kuwa na maandalizi ya muda mrefu kwa nafasi hii kubwa kabisa katika kulitumikia taifa. Kama ukisikia mafuriko ya watu kipindi cha Mh. Lowasa, basi yalikuwa mafuriko kwelikweli, Tundulisu hawezi hata kumfikia nusu yake ()

().

Kipindi hiki naona kama Mh. Mbowe hana ile confidence kabisa ambayo aliyokuwa nayo 2015 kipindi cha Mh. Lowasa (). Kwa kutumia uwezo wangu, ambao amenipa mwenyezi Mungu wa kusoma saikolojia ya mtu, yafuatayo yanaweza kuwa ndio sababu ya Mh. Mbowe kuloose confidence kabisa kuelekea uchaguzi mkuu, yaani hajui kinachoenda kutokea. TL alipokuwa Arusha kusaka wadhamini, wananchi walimtaka Mbowe aongee, Mbowe akaja na hakusema chapuo lolote kwa TL, badala yake alitaja kauli mbiu tu (). Kwa jambo hili kwangu linaweza kubeba hoja zifuatazo:

  • Mbowe alikuwa anajua kabisa kuwa watu walikuwa wanamtaka Tundulisu ili aweze kupeperusha bendera ya uraisi Chadema kwa sababu ya lile tukio la mashambulizi dhidi yake ili kulenga kura za huruma ya wananchi, ila bado najiuliza kwa nini aliamua naye kutangaza nia, baadae akaacha?
  • Au Mbowe aliogopa aibu ya kushindwa na Lisu, maana asilimia kubwa ya wajumbe walikuwa wanataka Lisu apeperushe bendera?
  • Kuna uwezekano Mh. Mbowe alikuwa anajua kabisa, Tundulisu hana uwezo wa kupambana na Magufuli, ila kura atakazopata zitakuwa za huruma ya wananchi, ila kwakuwa mkutano mkuu ulikuwa unamtaka TL, basi hakuwa na namna yoyote zaida ya kuunga mkono
Namalizia nakusema, Mh. Mbowe hana confidence kabisa kwenye uchaguzi huu, japokuwa wengine wanaonekana wanayo, ila ni tofauti sana na huyu ndugu, anajua kabisa Lisu hawezi kuifikia level ya Lowasa, hata nusu yake hawezi, ila ataleta upinzani angalau kidogo tu.

Asante,
Nawasilisha
Kejuu

Mkuu, inamaana umeridhika kabisa na hizo elfu saba saba za Lumumba kwaajili ya njaa ya muda mfupi tu? CCM hawafai hata uwasafishe vipi, kuna genge la watu wachache mno huko ambao ndio wanufaika wa kodi zenu na rasilimali za nchi hii. Usiposhiriki kuifurusha CCM madarakani hata watoto na wajukuu zako watashangaa sana juu ya uwezo wako wa kufikiri na kupambanua mambo, tazama namna Bashite anavyojitapa kwa ujinga na upuuzi wenu.
 
Attachments

  • Makonda ajitangaza mla raha namba moja duniani..mp4
    857.8 KB
Hao wazee walishauri sana lakini jamaa hawaelewi wakaamaua kubwaga , sasa wanawachora tuu.. na wagombea wao.
Unajua wazee huwa wana hekima kubwa sana, ndiyo huwa hawataki shari, ndiyo maana wameamua kuwa pembeni kama akina Prof. Safari. Hapo ndiyo utajua namna ya leadership iliyopo pale, maana chama kile ni mali ya mtu, siyo ya watu.
 
Niambie umetumia kipimo gani kwa Lijuakali kusema hataki unafiki??? Mtu ambaye hadi nyie CCM mmempiga spana kuanzia ubunge hadi udiwani????
We hujui tu, kwa analysis zangu inawezekana ikawa hivi:
1. Kumbuka mwaka 2015, Lijua alimgaragaza sana CCM.
2. yawezekana wajumbe walikuwa na hasira sana dhidi yake, wakaamua kulipiza kisasi cha 2015 na kumpa Assenga kura nying.
Nahisi inakutosha.
 
Kajipange upya!!! Wana hasira nae kawanyima nini?? Tatizo mnaona watanzania wote ni wajinga
 
Mkuu, inamaana umeridhika kabisa na hizo elfu saba saba za Lumumba kwaajili ya njaa ya muda mfupi tu? CCM hawafai hata uwasafishe vipi, kuna genge la watu wachache mno huko ambao ndio wanufaika wa kodi zenu na rasilimali za nchi hii. Usiposhiriki kuifurusha CCM madarakani hata watoto na wajukuu zako watashangaa sana juu ya uwezo wako wa kufikiri na kupambanua mambo, tazama namna Bashite anavyojitapa kwa ujinga na upuuzi wenu.
Ilikuwa CCM ile, siyo sasa chini ya Magu. Na laiti Magu angeingia baada ya Nyerere, mbona bongo tungekuwa kama China vile, maana tulikuwa na uchumi sawa na wao. Tatizo tz tuna wapinzani njaa, wanaotageti ruzuku tu. Kwanini wasiunde chama kimoja ili wapambane na CCM. Nyerere alishawahi kuwashauri, ila mnajifanya vichwa maji ().
Check mzee mzalendo hapo, mzee aliyekuwa anatembea katika haki na kipimo cha Kiongozi anatakiwa awe kwenye mizani hii, I think Magu deserve this credit. Na mlivyo waajabu, mnatuletea huyo jamaa awe raisi kweli?
 
Kama mngekuwa mnajua kuwa atapwaya Kwa nini mlimpiga risasi???

hakuna ushahidi wowote unaonyesha ccm wamempiga risasi lissu, basi kwakua hakuna ushahidi sio vizuri kutupia lawama sehem ambapo sio, mfano: juzi mlikua mnalalamika ofisi zenu zmechomwa akaja kiongozi wenu mmoja akaapa kwa biblia kabisa kwamba cdm walishahusika nyuma na kuchoma ofisi zao wenyewe, sasa izi siasa za namna hii haziwpeleki kokote, tunachokiona apa saaahv yawezekana hata hio cdm ikawa mwisho wake mwaka huu
 
Ilikuwa CCM ile, siyo sasa chini ya Magu. Na laiti Magu angeingia baada ya Nyerere, mbona bongo tungekuwa kama China vile, maana tulikuwa na uchumi sawa na wao. Tatizo tz tuna wapinzani njaa, wanaotageti ruzuku tu. Kwanini wasiunde chama kimoja ili wapambane na CCM. Nyerere alishawahi kuwashauri, ila mnajifanya vichwa maji ().
Check mzee mzalendo hapo, mzee aliyekuwa anatembea katika haki na kipimo cha Kiongozi anatakiwa awe kwenye mizani hii, I think Magu deserve this credit. Na mlivyo waajabu, mnatuletea huyo jamaa awe raisi kweli?

Maajabu haya, unajituma kupambania bashite aendelee kula raha? CCM kuna wapuuzi wengi sana.
 
Kajipange upya!!! Wana hasira nae kawanyima nini?? Tatizo mnaona watanzania wote ni wajinga
Unamkumbuka Msigwa aliyekiri mbele za watanzania kuwa alimsingizia Mh. Kinana bungeni, halafu huyo huyo anakuja kutaka kupambana na Mag? Are you really serious guys? Sasa CCM mtaiondoaje madaraka kwa watu wa sampuli hii kama akina msigwa?
 
hakuna ushahidi wowote unaonyesha ccm wamempiga risasi lissu, basi kwakua hakuna ushahidi sio vizuri kutupia lawama sehem ambapo sio, mfano: juzi mlikua mnalalamika ofisi zenu zmechomwa akaja kiongozi wenu mmoja akaapa kwa biblia kabisa kwamba cdm walishahusika nyuma na kuchoma ofisi zao wenyewe, sasa izi siasa za namna hii haziwpeleki kokote, tunachokiona apa saaahv yawezekana hata hio cdm ikawa mwisho wake mwaka huu
Jamaa hawa wanatekana wao kwa wao, halafu wanaisingizia serikali () Siasa za kipopoma kweli yaan.
 
hakuna ushahidi wowote unaonyesha ccm wamempiga risasi lissu, basi kwakua hakuna ushahidi sio vizuri kutupia lawama sehem ambapo sio, mfano: juzi mlikua mnalalamika ofisi zenu zmechomwa akaja kiongozi wenu mmoja akaapa kwa biblia kabisa kwamba cdm walishahusika nyuma na kuchoma ofisi zao wenyewe, sasa izi siasa za namna hii haziwpeleki kokote, tunachokiona apa saaahv yawezekana hata hio cdm ikawa mwisho wake mwaka huu
Alipigwa yale marisasi kwa amri ya Mwenyekiti, mchana kweupe na kwenye makazi ya viongozi huku walinzi wa maeneo hayo wakiwa wameondolewa kupisha "baraka" za jiwe zitimizwe.
 
Mngekuwa hamtaki Chama Chetu kife mngefanya biashara ya kununua madiwani na wabunge wa Chama chetu????? Semeni mnaweweseka tu maana mipango yenu yote imekufa
Hakuna wabuge wala madiwani walionunuliwa, wameondoka kwa matatizo ya chama chenu, na sio hao hata wazee wenu wa ushauri nao walinunuliwa? baregu, safari? Wanaondoka sababu wanaona kua nyie ni pasua kichwa kikundi cha wahuni watu wenye hekima hawawezi kukaa humo, ni bora wakafanye siasa kwenye vyama vingine.
 
Maajabu haya, unajituma kupambania bashite aendelee kula raha? CCM kuna wapuuzi wengi sana.
Unamjua huyu? Ndo siasa zenu, na nina uhakika hata ile ofisi ya kanda ya kusini mmeichoma wenyewe ili kupata kick za kisiasa.
 
Unamjua huyu? Ndo siasa zenu, na nina uhakika hata ile ofisi ya kanda ya kusini mmeichoma wenyewe ili kupata kick za kisiasa.

Propaganda za kijinga sana hizi, inamaana hatuna jeshi la polisi sivyo? Kodi zinatum ika hovyo kabisa.
 
Propaganda za kijinga sana hizi, inamaana hatuna jeshi la polisi sivyo? Kodi zinatum ika hovyo kabisa.
Kwa hiyo bado unaendelea kujitoa ufahamu? Ulikuwa unamsikiliza au ndo ule opopoma wenu? Watu wanatengeneza matukio halafu wanailaumu serikali.
 
Kwa hiyo bado unaendelea kujitoa ufahamu? Ulikuwa unamsikiliza au ndo ule opopoma wenu? Watu wanatengeneza matukio halafu wanailaumu serikali.
Nimekuuliza swali tuna serikali? Kama mtu anaweza kufanya lolote hapa nchini na asichukuliwe hatua yeyote ile basi hatuna serikali, bali ni GENGE TU la wahuni na wahalifu ndio linalotuongoza. Ndio sababu tunataka mabadiliko, Saa ya Ukombozi ni Sasa.
 
Back
Top Bottom