Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Hilo li chama lilishakufa mara nyingi anataka life mara ngapi???Nimebahatika kusikiliza kipande cha hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe aliyoitoa huko Mtwara. Ni katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Reli mkoani humo. Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alizungumza mambo mengi yakiwemo ya kivyama, kimaisha na kadhalika. Niseme wazi kuwa Mbowe alitoa hotuba nzuri na ya kuvutia.
Naipongeza hotuba ya Mbowe kwakuwa ilitumia lugha ya tahadhari na staha. Pia, Mbowe alikuwa akizungumza kwa hoja na kwa kutaka kutoa somo kwa wapigakura-hatua kwa hatua. Binafsi, naiona sehemu kubwa ya hotuba ya Mbowe kama bora, yenye ukomavu wa kisiasa, umahiri na ujuzi wa mambo mengi yakiwemo ya kimaisha kwa watanzania.
Lakini, kuna kitu kimoja Mhe. Mbowe hakupaswa kukisema kadiri alivyokisema. Alikuwa akijenga hoja kuwa katika vyama vya siasa vya upinzani kuna juhudi za kuvidhoofisha au hata kuvisambaratisha. Akawa anatolea mfano mtifuano unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi almaarufu kama CUF.
Mhe. Mbowe akasema, pamoja na mambo mengine, kuwa CHADEMA 'itauwawa' siku akifa yeye na si akiwepo. Hapo ndipo penye tatizo. Pamoja na kuwa yeye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na kiongozi wa juu kabisa wa chama chake, anapaswa kujua kuwa chama si mtu, chama ni mfumo. Kauli yake hiyo inaonyesha wazi kuwa yeye ndiye CHADEMA na CHADEMA ndiye yeye.
Hilo si jambo jema. Akiwa ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini anapaswa kujenga chama kimfumo zaidi kuliko watu. Asikijenge chama chake katika kuwategemea watu ambao 'wakifa' na chama kinakufa. Ingawa mimi si mwanasiasa, naamini kuwa chama si watu pekee. Ni itikadi. Hata chama chenye wanachama wachache chaweza kushinda uchaguzi kwa itikadi.
Najua, Mhe. Mbowe alikuwa kwenye jukwaa la kisiasa. Kwa kusema vile, hakika, aliteleza. Hakupaswa kusema vile. Kauli ya kuonyesha kuwa 'akifa' yeye ndipo chama chake kitaanza kudhoofishwa au kuuwawa si kauli njema kisiasa. Kwa ukomavu, umahiri na ubobezi wake katika ulingo wa kisiasa, naamini atakuwa makini zaidi!
kwa chadema ni sawa mkuu,kifupi Mbowe karithi chama,nafasi na madeni yote ya chama,so ngumu kwa cdm kupata mtu atakaye beba dhamana hizo,( mtazamo wangu)Upo sahihi. Hilo hakupaswa kuliongea, maana linajenga picha ya kwamba Chama hicho ni one man show
Unataka kumlisha maneno, yeye amesema kufa Chadema labda yeye auwawe....Petro E Mselewa,nadhani alikuwa zaidi anaweka msisitizo wa jambo husika.Ila nadhani ilichanganyika na kahasira kidogo.
Mkuu na yule aliyesema bora CCM haikumfia pale Dodoma pia alikuwa anamaanisha yeye ndiye CCM na CCM ni yeye?. Hizo ni kauli tu za kisiasa zinazoonesha commitment ya mtu kwa taasisi Fulani. Ni kama kusema chini ya uongozi wangu makanikia hayatasafirishwa nje.Aliyoyasema Mbowe huko Mtwara ndio hali halisi ya CHADEMA na ndio ukweli......wenyewe ambao watu wengi CDM WANAFUMBA MACHO ILI KUTOUONA UKWELI......
Mbowe ni CHADEMA na CHADEMA ni yeye.....akiondoka yeye maana yake CHADEMA ITAKUFA....na ndio maana akafuta kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye katiba ya CHADEMA ILI YEYE AENDELEE KUWA MWENYEKITI MPAKA SIKU MUNGU ATAKAPOMCHUKUA.....
MBOWE HAAMINI KAMA KUTAKUJA KUWA NA KIONGOZI MAHIRI CHADEMA KULIKO YEYE..........
Nimebahatika kusikiliza kipande cha hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe aliyoitoa huko Mtwara. Ni katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Reli mkoani humo. Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alizungumza mambo mengi yakiwemo ya kivyama, kimaisha na kadhalika. Niseme wazi kuwa Mbowe alitoa hotuba nzuri na ya kuvutia.
Naipongeza hotuba ya Mbowe kwakuwa ilitumia lugha ya tahadhari na staha. Pia, Mbowe alikuwa akizungumza kwa hoja na kwa kutaka kutoa somo kwa wapigakura-hatua kwa hatua. Binafsi, naiona sehemu kubwa ya hotuba ya Mbowe kama bora, yenye ukomavu wa kisiasa, umahiri na ujuzi wa mambo mengi yakiwemo ya kimaisha kwa watanzania.
Acha kujidhalilisha..Hilo li chama lilishakufa mara nyingi anataka life mara ngapi???
Khaa! Na bado mnajiita "learned" brothers.Came on learned brother your so bold than this bwana!
Unataka kumlisha maneno, yeye amesema kufa Chadema labda yeye auwawe....
Kwa maana hiyo hawezi kuachia Uenyekiti mpaka afe au auwawe...
Kifupi ni mwenyekiti wa kudumu.!