Mbowe hakupaswa kusema vile, kisiasa aliteleza

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,173
25,446
Nimebahatika kusikiliza kipande cha hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe aliyoitoa huko Mtwara. Ni katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Reli mkoani humo. Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alizungumza mambo mengi yakiwemo ya kivyama, kimaisha na kadhalika. Niseme wazi kuwa Mbowe alitoa hotuba nzuri na ya kuvutia.

Naipongeza hotuba ya Mbowe kwakuwa ilitumia lugha ya tahadhari na staha. Pia, Mbowe alikuwa akizungumza kwa hoja na kwa kutaka kutoa somo kwa wapigakura-hatua kwa hatua. Binafsi, naiona sehemu kubwa ya hotuba ya Mbowe kama bora, yenye ukomavu wa kisiasa, umahiri na ujuzi wa mambo mengi yakiwemo ya kimaisha kwa watanzania.

Lakini, kuna kitu kimoja Mhe. Mbowe hakupaswa kukisema kadiri alivyokisema. Alikuwa akijenga hoja kuwa katika vyama vya siasa vya upinzani kuna juhudi za kuvidhoofisha au hata kuvisambaratisha. Akawa anatolea mfano mtifuano unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi almaarufu kama CUF.

Mhe. Mbowe akasema, pamoja na mambo mengine, kuwa CHADEMA 'itauwawa' siku akifa yeye na si akiwepo. Hapo ndipo penye tatizo. Pamoja na kuwa yeye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na kiongozi wa juu kabisa wa chama chake, anapaswa kujua kuwa chama si mtu, chama ni mfumo. Kauli yake hiyo inaonyesha wazi kuwa yeye ndiye CHADEMA na CHADEMA ndiye yeye.

Hilo si jambo jema. Akiwa ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini anapaswa kujenga chama kimfumo zaidi kuliko watu. Asikijenge chama chake katika kuwategemea watu ambao 'wakifa' na chama kinakufa. Ingawa mimi si mwanasiasa, naamini kuwa chama si watu pekee. Ni itikadi. Hata chama chenye wanachama wachache chaweza kushinda uchaguzi kwa itikadi.

Najua, Mhe. Mbowe alikuwa kwenye jukwaa la kisiasa. Kwa kusema vile, hakika, aliteleza. Hakupaswa kusema vile. Kauli ya kuonyesha kuwa 'akifa' yeye ndipo chama chake kitaanza kudhoofishwa au kuuwawa si kauli njema kisiasa. Kwa ukomavu, umahiri na ubobezi wake katika ulingo wa kisiasa, naamini atakuwa makini zaidi!
 
Hilo li chama lilishakufa mara nyingi anataka life mara ngapi???
 
Aliyoyasema Mbowe huko Mtwara ndio hali halisi ya CHADEMA na ndio ukweli......wenyewe ambao watu wengi CDM WANAFUMBA MACHO ILI KUTOUONA UKWELI......

Mbowe ni CHADEMA na CHADEMA ni yeye.....akiondoka yeye maana yake CHADEMA ITAKUFA....na ndio maana akafuta kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye katiba ya CHADEMA ILI YEYE AENDELEE KUWA MWENYEKITI MPAKA SIKU MUNGU ATAKAPOMCHUKUA.....

MBOWE HAAMINI KAMA KUTAKUJA KUWA NA KIONGOZI MAHIRI CHADEMA KULIKO YEYE..........
 
Mbowe yy kwa sasa ndo mwenyekiti so chama kikifa yy ndo wakulaumiwa so amejarbu kuonesha msisitizo katka uongoz wake chama hakitomfia

Hiii ni sawa na mpira mess ndo kapten wa agentina kila wanavofungwa fainali yy ndo analaumiwa coz ndo kiongoz,,au ronaldo kupewa sifa zote za ushnd wa ureno japo hakumaliza hata kipind cha kwanza

So ndo hvohvo kwa mbowe baya lolote yy ndo atalaumiwa na zuri yyte yy ndo atasifiwa
 
Upo sahihi. Hilo hakupaswa kuliongea, maana linajenga picha ya kwamba Chama hicho ni one man show
kwa chadema ni sawa mkuu,kifupi Mbowe karithi chama,nafasi na madeni yote ya chama,so ngumu kwa cdm kupata mtu atakaye beba dhamana hizo,( mtazamo wangu)
 
Mara ngapi tunasikia kauli Kama Hizi kutoka kwa viongozi.

Nyerere alisemaje kuhusu kuwapa nchi Wapinzani

Mkapa alisema nini vile pale Jangwani

CCM wanasemaje kuhusu kuwapa nchi wapinzani
 
Aliyoyasema Mbowe huko Mtwara ndio hali halisi ya CHADEMA na ndio ukweli......wenyewe ambao watu wengi CDM WANAFUMBA MACHO ILI KUTOUONA UKWELI......

Mbowe ni CHADEMA na CHADEMA ni yeye.....akiondoka yeye maana yake CHADEMA ITAKUFA....na ndio maana akafuta kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye katiba ya CHADEMA ILI YEYE AENDELEE KUWA MWENYEKITI MPAKA SIKU MUNGU ATAKAPOMCHUKUA.....

MBOWE HAAMINI KAMA KUTAKUJA KUWA NA KIONGOZI MAHIRI CHADEMA KULIKO YEYE..........
Mkuu na yule aliyesema bora CCM haikumfia pale Dodoma pia alikuwa anamaanisha yeye ndiye CCM na CCM ni yeye?. Hizo ni kauli tu za kisiasa zinazoonesha commitment ya mtu kwa taasisi Fulani. Ni kama kusema chini ya uongozi wangu makanikia hayatasafirishwa nje.
 
Nimebahatika kusikiliza kipande cha hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe aliyoitoa huko Mtwara. Ni katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Reli mkoani humo. Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alizungumza mambo mengi yakiwemo ya kivyama, kimaisha na kadhalika. Niseme wazi kuwa Mbowe alitoa hotuba nzuri na ya kuvutia.

Naipongeza hotuba ya Mbowe kwakuwa ilitumia lugha ya tahadhari na staha. Pia, Mbowe alikuwa akizungumza kwa hoja na kwa kutaka kutoa somo kwa wapigakura-hatua kwa hatua. Binafsi, naiona sehemu kubwa ya hotuba ya Mbowe kama bora, yenye ukomavu wa kisiasa, umahiri na ujuzi wa mambo mengi yakiwemo ya kimaisha kwa watanzania.

Umesikiliza Hotuba nzima ama Kipande?, maelezo yako ya awali inaonyesha kana kwamba umesikiliza Kipande, lakini maelezo yako yote unaisifia hotuba na pia umepata cha Kukosoa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni msisitizo wa kua tayari kufaa kwajiri ya chama sio kwamba amijimilikisha chama hizo ni aina za public speech kuvuta hinsia za wasikilizaji
 
Mkuu Ile speech ya Mbowe kiukweli ni nzuri sana na ina hoja nzito kweli-kweli..

Mbowe kuisema kauli ile sidhani kama alikuwa na maana hiyo unayoisema rather ni kuonyesha uongozi wake ulivyo MADHUBUTI kuweza kutoruhusu Chama kufa..

Pili ni kuonyesha jinsi alivyo serious na Siasa za upinzani na kwamba haiwezekani hata siku moja akawa MSALITI.
 
Unataka kumlisha maneno, yeye amesema kufa Chadema labda yeye auwawe....

Kwa maana hiyo hawezi kuachia Uenyekiti mpaka afe au auwawe...

Kifupi ni mwenyekiti wa kudumu.!

Wewe ndiyo uliyemlisha maneno.Pole sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom