Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,516
Nimebahatika kusikiliza kipande cha hotuba ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Mhe. Freeman Mbowe aliyoitoa huko Mtwara. Ni katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Reli mkoani humo. Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alizungumza mambo mengi yakiwemo ya kivyama, kimaisha na kadhalika. Niseme wazi kuwa Mbowe alitoa hotuba nzuri na ya kuvutia.
Naipongeza hotuba ya Mbowe kwakuwa ilitumia lugha ya tahadhari na staha. Pia, Mbowe alikuwa akizungumza kwa hoja na kwa kutaka kutoa somo kwa wapigakura-hatua kwa hatua. Binafsi, naiona sehemu kubwa ya hotuba ya Mbowe kama bora, yenye ukomavu wa kisiasa, umahiri na ujuzi wa mambo mengi yakiwemo ya kimaisha kwa watanzania.
Lakini, kuna kitu kimoja Mhe. Mbowe hakupaswa kukisema kadiri alivyokisema. Alikuwa akijenga hoja kuwa katika vyama vya siasa vya upinzani kuna juhudi za kuvidhoofisha au hata kuvisambaratisha. Akawa anatolea mfano mtifuano unaoendelea ndani ya Chama cha Wananchi almaarufu kama CUF.
Mhe. Mbowe akasema, pamoja na mambo mengine, kuwa CHADEMA 'itauwawa' siku akifa yeye na si akiwepo. Hapo ndipo penye tatizo. Pamoja na kuwa yeye ni Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na kiongozi wa juu kabisa wa chama chake, anapaswa kujua kuwa chama si mtu, chama ni mfumo. Kauli yake hiyo inaonyesha wazi kuwa yeye ndiye CHADEMA na CHADEMA ndiye yeye.
Hilo si jambo jema. Akiwa ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini anapaswa kujenga chama kimfumo zaidi kuliko watu. Asikijenge chama chake katika kuwategemea watu ambao 'wakifa' na chama kinakufa. Ingawa mimi si mwanasiasa, naamini kuwa chama si watu pekee. Ni itikadi. Hata chama chenye wanachama wachache chaweza kushinda uchaguzi kwa itikadi.
Najua, Mhe. Mbowe alikuwa kwenye jukwaa la kisiasa. Kwa kusema vile, hakika, aliteleza. Hakupaswa kusema vile. Kauli ya kuonyesha kuwa 'akifa' yeye ndipo chama chake kitaanza kudhoofishwa au kuuwawa si kauli njema kisiasa. Kwa ukomavu, umahiri na ubobezi wake katika ulingo wa kisiasa, naamini atakuwa makini zaidi!