Mbowe awapa ukweli mchungu watu wa kusini, hakuna mtu mwenye uchungu na nyie isipokuwa wenyewe

Utapeli wa siasa tu...Sasa kama umeshawaambia wawe na uchungu wao wenyewe Mwanza kuwekwa Taa kunahusika vipi...nao si waweke hizo taa.

Nadhani afanye utafiti vizuri ajue tatizo ni nini aje na takwimu.
 
Siamini kama haya maneno yametamkwa na Mbowe!

Ninaamini Mbowe ana busara katika masuala ya kisiasa.

Kwa maana nyingine, watu wa kanda ya ziwa hawatakiwi kupata maendeleo au anataka kutuambia watu wa kanda ya kusini watafute Rais wao wa Tanzania.

Haoni kama alikuwa anawaambia kuwa wasitegemee Lowassa kuwasaidia kama atakuwa Rais kwa sababu hatoki Kanda ya kusini.

Siasa za kikanda au udini ni mbaya sana katika nchi zinazoendelea. Siasa za aina hii tuziache kwa sababu hazina maslahi mapana kwa taifa.
 
Huku ni kukwepa majukumu, ukiigawa hii nchi kimajimbo, (kaskazini, kusini, nyanda za juu, ziwa kuu, na mashariki) utakuwa una wanyima watanzania umoja wao walio ujenga kwa miaka mingi. Hii inaweza kufanya upande mmoja wa nchi usiwe na ulazima wa kusaidia upande mwingine. Korosho ya Mtwara, haita nunuwa madawati ya kigoma. Dhahabu ya Mwanza haita nunuwa chanjo ya watoto wa Tanga. Hii inaweza kwenda mpaka kwenye kazi, wa nyanda za juu anaweza kupata mtiani wa kutafuta kazi kanda ya mashariki kutokana na wamashariki wanasema hizi ni kazi zetu rudi ulikotoka. Mifano ipo mingi duniani walio jaribu sera kama hizi, hayakuisha vizuri. Nchi yetu bado haija jitosheleza kwa kila kanda kujitegemea, tusiige mambo kutoka nchi zilizo funguka kiuchumi kwa miaka mingi, tutakuwa tunafanya kinyume cha maendeleo na mshikamano uliokuwepo Tanzania.

Unapenda umoja hata mimi napenda umoja lakini penye ukweli lazima tuseme.Hivi kwenda kujenga uwanja wa ndege CHATO badala ya Lindi na Mtwara unategemea umoja utabaki salama ?.Mwl Nyerere ajenga umoja na kuenzi umoja hakuthubutu kujenga uwanja wa ndege Butiama.
 
Katika yote nakubaliana kwa asilimia miamoja na neno MWENYE UCHUNGU NAA ENEO NI MUHUSIKA. Mfano,mwekezaji wa mgodi wa dhahabu toka eneo A aliyewekeza eneo Z,atakachooangalia ni njia yoyote nafuu ili achukuwe dhahabu aliyokusudia,lakini muwekezaji wa aina hiyo toka eneo A na kuwekeza eneo A,pamoja na kutafuta unafuu lkn atapenda sana eneo A liwe bora. Hapa unafuu nimemaanisha,garama za uchimbaji pamoja na malipo yote kwa mamlaka husika.
 
Kusini wanauza korosho kilo 4000 ,


Alafu nyie chama la kutetea mafisadi chadema mnapeleka porojo zenu za kitoto kabisa.
Walikua wanataka kubomoa ngome za cuf kuiba wafuasi lakini wamechelewa.Lipumba yupo sahihi kabisa anaposema chadema wanauchochea mgogoro wa cuf ili wajinufaishe
 
Unapenda umoja hata mimi napenda umoja lakini penye ukweli lazima tuseme.Hivi kwenda kujenga uwanja wa ndege CHATO badala ya Lindi na Mtwara unategemea umoja utabaki salama ?.Mwl Nyerere ajenga umoja na kuenzi umoja hakuthubutu kujenga uwanja wa ndege Butiama.
Duh, huu uzi nilichangia siku nyingi kidogo kusema sio mimi nileandika, Duh utu uzima.

Anyway watu wanapigia kelele uwanja wa Chato bila kujuwa sababu ya kuwa na uwanja hapo, kwanza mgeuliza huo uwanja ni wa aina gani. Nachoweza kusema, maoneo hayo tuna pakama na nchi nne, na umbali kutoka nchi moja hadi nyingine sio mrefu. Kwa usalama wetu tunahitaji kuwa na uwanja hapo Chato. (Utakuwa umenielewa)
 
Back
Top Bottom