Mbowe aunda Baraza la Mawaziri Vivuli - ni la CHADEMA

Du sawa km hajawahi kuchukua fomu kupitia Chama chake kwa kuomba ateuliwe kugombea Urais na akakwama NEC basi nimekosea ila ataomba sasa kupitia Chama alichopo haogopi k2

mbona unarudia rudia makosa .... sasa ubongo wako umechakachuka ... National Electoral Commission (NEC) haihusiki na uchaguzi wa ndani wa chama chochote ..... sijui una maana gani ..... au hujui kujieleza kwa maelezo yanayojitosheleza .... unacharuka kupost haraka haraka
 
The problem ni kwamba HAELEWEKI.

Shibuda anaeleweka, huwa anajipambanua kama ni mwana CCM damu damu, hana uchungu na nchi bali anauchungu na CCM. Ndo maana huwa anatoa ushauri kama CCM inataka ibaki madarakani ifanye ABC!

Kuingia CDM ni njia ya kwenda Bungeni tu, hana lolote la dhati ndani ya upinzani. Wamemuweza na kumtosa uwaziri kivuli. Jamaa lina domo chafu hilo, sijapata kuona! Linapeleka mambo ya mipasho bungeni!
 
Kwa ujumla, ni baraza makini. Ila nadhani Mbowe amenoa kwenye uteuzi huu:

John Mnyika - Nishati na Madini?!

Tundu Lissu - Sheria na Katiba


Sawa, Tundu Lissu ni mwanasheria aliyebobea. Lakini wizara ingemfaa zaidi ni Nishati na Madini kuliko wizara ya sheria. Huku ana uzoefu mkubwa wa tafiti nyingi alizofanya akiwa LEAT na pia angetumia vyema utaalamu wake wa sheria kufumua mikataba ya wizi ya kwenye madini na umeme.

Mnyika hana uzoefu wa mambo ya nishati na madini ingawa ni mwanasiasa makini. Lissu angetoa mchango mkubwa zaidi kwenye hii wizara nyeti.

Kikwete amekuwa hajui umuhimu na unyeti wa wizara hii ndiyo maana siku zote anateuwa mawaziri wasio na uwezo unaotakiwa kwenye wizara ya madini, kama William Ngeleja, wa sasa.

Inasikitisha kuona Mbowe naye amenoa kwenye wizara hii kama Kikwete.


Baraza hufanya kazi kwa kusaidiana,lakini pia usiwe na shaka na Mnyika kwani anaimudi vema.
 
Asenteni sana wanajamii kwa kunipambazua juu ya shibuda na uwepo wake chadema! Kama ni hivyo ni hatari sana kwa cdm waspokua care
 
Bora alivyoachwa maana watu wengi walishaanza kuwa na wasiwasi nae kutokana na mchango wake wa wiki iliyopita. Hivi mawaziri vivuli nao wana packages za maana kama kiongozi wa kambi ya upinzani au wajumbe wa kamati za bunge???

Wenye majibu please??????? Tujue Waheshimiwa Kafulila na Hamad Rashid walikuwa wanapigania nini.
 
Hakuna manaibu! Wako wasaidizi. Baraza hilo ndilo ambalo CDM inaamini linaweza kutekeleza kazi ya wananchi. Ukubwa wa baraza kwa nchi masikini kama ya kwetu ni mzigo!!
 
MSemaji ofisi ya Raisi: Freeman Mbowe, Msaidizi: Silinde David
Uwekezaji na Uwezeshaji: Matiko
Ofisi ya Waziri Mkuu: Vicent Kiboko
Ofisi ya Raisi: Said
Ofisi ya Raisi & Utawala Bora: Mch Nakse wa Karatu
Ofisi ya Makamu wa Raisi: Gekulu
Ofisi ya Raisi & Mazingira: Leticia Nyerere
OFisi ya Fedha: Zitto Kabwe Msaidizi: Christina Lissu
Mambo ya Ndani: Lema
Katiba ya Sheria: Tindu Lissu
Kimataifa: Wenje
Jeshi la Ulinzi: Seladhini
Mawasiliano: prof Kayili
Makazi: Mdee
Maliasili: Mch Peter Msigwa
Nishat na Madini: Mnyika
Ujenzi: Machemli
Uchukuzi: Mhonga Said
Viwanda: Olenywa
Elimu na Mfunzo: Mtinda
Afya: Dr Gilbert Mbasa
Maendeleo ya Jamii: Naomi Kaiula
Vijana na michezo: Mbilinyi Mr Two
Kilimo: Meshack Obulugwa
Maji: Haines Kiwia

Hawa ndio MAWAZIRI KIVULI WA UPINZANI

Mbona Baraza kubwa?
 
Hii safi ila wachape kazi sasa na kubuni mbinu mbadala za kuinua uchumi na kumkomboa mwananchi wa kawaida.
 
daaah nimecheka haswa ..Wenje mambo ya kimataifa kazi ipo..wangempa msaidizi awe Lema
 
Fareed said:
Kwa ujumla, ni baraza makini. Ila nadhani Mbowe amenoa kwenye uteuzi huu:

John Mnyika - Nishati na Madini?!

Tundu Lissu - Sheria na Katiba

Sawa, Tundu Lissu ni mwanasheria aliyebobea. Lakini wizara ingemfaa zaidi ni Nishati na Madini kuliko wizara ya sheria. Huku ana uzoefu mkubwa wa tafiti nyingi alizofanya akiwa LEAT na pia angetumia vyema utaalamu wake wa sheria kufumua mikataba ya wizi ya kwenye madini na umeme.

Mnyika hana uzoefu wa mambo ya nishati na madini ingawa ni mwanasiasa makini. Lissu angetoa mchango mkubwa zaidi kwenye hii wizara nyeti.

Kikwete amekuwa hajui umuhimu na unyeti wa wizara hii ndiyo maana siku zote anateuwa mawaziri wasio na uwezo unaotakiwa kwenye wizara ya madini, kama William Ngeleja, wa sasa.

Inasikitisha kuona Mbowe naye amenoa kwenye wizara hii kama Kikwete.

Fareed,

..hata mimi nilikuwa na mawazo kama yako.

..lakini nimekumbuka kwamba Lissu yuko kwenye kamati ya Sheria na Katiba ya Bunge.

..uteuzi wa kamati za bunge umetangulia uteuzi wa baraza la mawaziri kivuli.

..nadhani suala hilo ndilo lililo-influence uteuzi wa Mnyika na Lissu ktk wizara hizo.

NB:

..sina uhakika, lakini nadhani Mnyika yuko kwenye kamati ya nishati na madini.
 
MSemaji ofisi ya Raisi: Freeman Mbowe, Msaidizi: Silinde David
Uwekezaji na Uwezeshaji: Matiko
Ofisi ya Waziri Mkuu: Vicent Kiboko
Ofisi ya Raisi: Said
Ofisi ya Raisi & Utawala Bora: Mch Nakse wa Karatu
Ofisi ya Makamu wa Raisi: Gekulu
Ofisi ya Raisi & Mazingira: Leticia Nyerere
OFisi ya Fedha: Zitto Kabwe Msaidizi: Christina Lissu
Mambo ya Ndani: Lema
Katiba ya Sheria: Tindu Lissu
Kimataifa: Wenje
Jeshi la Ulinzi: Seladhini
Mawasiliano: prof Kayili
Makazi: Mdee
Maliasili: Mch Peter Msigwa
Nishat na Madini: Mnyika
Ujenzi: Machemli
Uchukuzi: Mhonga Said
Viwanda: Olenywa
Elimu na Mfunzo: Mtinda
Afya: Dr Gilbert Mbasa
Maendeleo ya Jamii: Naomi Kaiula
Vijana na michezo: Mbilinyi Mr Two
Kilimo: Meshack Obulugwa
Maji: Haines Kiwia

Hawa ndio MAWAZIRI KIVULI WA UPINZANI

Good start!Mkuu Mbowe na imani umepata shida sana kupanga safu hii maake wachezaji ndio hawa waliopata usajiri kupitia dirisha dogo.Any way i hope watasukuma gurudumu japo kwa sasa no comments!
 
Kwa wasiojua Arusha, pazuri na Geneva of Africa ,ila Usalama ni mdogo,Leo askari kapigwa risasi,wanaopigwa visu,bisibisi ndo usiseme,waziri aliangalie hili na siasa ziwekwe kando kwani nihatari.kilakukicha afadhali ya Jana ....Jana polisi kwenye masako wamemkuta mtoto wa sekondari amehifadhi shotgun mobili zimekatwa na zilishaua na kupora vyakutosha,mikes na non do zaukweli..hao hao ndo walimpiaga nakumuua askari wa kampuni moja inaitwa intelligence nakufa nakumwacha njane njamzito....tunakwenda wap?waziri mwenye dhamana na kivuli wake lemma pigen kaz tukae kwa usalama tuzalishe japo hakuna umeme.Hali ni mbaya sana
 
Back
Top Bottom