Mbowe asema hawamtaki Zitto Kabwe kwenye UKAWA

Mbowe asema hawamtaki Zitto Kabwe kwenye UKAWA

Dkt Kilembwe

Senior Member
Joined
Apr 25, 2015
Posts
154
Reaction score
102
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema hawatamruhusu Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Kauli ya Mbowe imetolewa siku chache baada ya Zitto kutangaza kuwa ACT ipo tayari kujiunga na Ukawa kama wanavyotaka Watanzania wakiwamo baadhi ya viongozi wa umoja huo.

Alitoa kauli hiyo jana wilayani Kyerwa alipozungumza na MTANZANIA.

Mbowe alisema kuwa hawamwamini tena Zitto kwa madai kuwa akiingia Ukawa atakuwa akivujisha siri za umoja huo kwenda Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Hatuwezi kumruhusu Zitto na chama chake kiwe miongoni mwa Ukawa. Tukiruhusu Zitto awepo siri zote zitakuwa zikiwafikia CCM," alisema Mbowe.

Aprili 15 mwaka huu, Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), kilitangaza kuwa kipo tayari kushirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la kuleta mapinduzi ya uchumi na kubomoa mfumo unaowanyonya wananchi.

Zitto alisema hivi sasa taifa limekuwa na shauku ya ACT kushirikiana na vyama vingine kama njia ya kufanikisha malengo ya kukitoa CCM madarakani.

Chanzo: Mtanzania


My take;
Hivi wenye dhamana na UKAWA ni Chadema peke yao,? au Chadema walianzisha UKAWA baada ya anguko lao,sasa wakaona wajifiche chini ya kivuli cha UKAWA? Mbowe anashindwa kuweka hadharani hizo taarifa za siri alizowahi kutoa Zitto.
 
Mkuu dkt kilembwe Zzk si ashasema Ukawa ni wasaka tonge??? Kwa akili ya kawaida tu ulitegemea Nani ampokee??? Wakati fulani kwenye maisha unazi na ufuasi uwekwe pembeni.... Nadhani kwa kuwa yeye Ana nguvu na aliweza kuiangusha serikali mara 2(though sijui ni serikali ipi) basi nadhani nguvu hiyo hiyo inatosha kabisa kuiondoa CCM.....
 
Si atasaliti tena ,yule yuda iskariote
 
Mkuu dkt kilembwe Zzk si ashasema Ukawa ni wasaka tonge??? Kwa akili ya kawaida tu ulitegemea Nani ampokee??? Wakati fulani kwenye maisha unazi na ufuasi uwekwe pembeni.... Nadhani kwa kuwa yeye Ana nguvu na aliweza kuiangusha serikali mara 2(though sijui ni serikali ipi) basi nadhani nguvu hiyo hiyo inatosha kabisa kuiondoa CCM.....

Kwani wewe unaishi kwenye serikali ipi? acha ndoto wakati haupo usingizini
 
Sikio la kufa halisikii dawa. MBOWE hajui kuwa CHADEMA ilishakufa na sasa inatembelea kwenye kivuli cha UKAWA.
 
MBOWE uwezo wake ni mdogo sana,hivi anataka WATU kama akina Lissu ili aendelee kuwaburuza

Teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh teh! Teh teh teh teh teh teh teh! Kumbe thread yako umeileta tu kipropaganda? Ni gazeti gani hilo kwanza tulijue
 
dj hawezi kuunga mkono zitto kuingia ukawa anajua kabisa ikiwa hivyo zitto atakuwa mshindani wake ndani ya ukawa na kama dunia ijuavyo (japo wengi roho inawauma) dj atabwagwa chini kama kiroba!

YUDA anataka kujiunga na wasaka tonge?
 
Si atasaliti tena ,yule yuda iskariote
CHADEMA mmetumia propagqnda ya kijinga sana kwa zitto, kweli elimu ni kitu muhimu sana, hivi kweli MBOWE anafikri kufanya hivgo watamdhoofisha ZITTO kweli? Naiona CCM hiyo ikishinda kwa kishindo tena Mwaka huu. ACT wanaweza kuwa wa pili kwenye uchaguzi mkuu.
 
Hiyo kauli aliyoitoa amewashirikisha CUF na NCCR ama yeye ndo babalao akiamua wengine kimya!!?
 
Kumkaribisha Zito ukawa ni sawa na kumkaribisha Hamad Rashid. Wote hawaaminiwi na vyama walivyofukuzwa. Zito na Hamad wote wana watu nyuma yao na lengo lao kuu ni kudhoofisha chadema and cuf, period. Hakuna upinzani wa kweli hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom