Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Ni bao la nguvu la kiuchumi lakini zaidi la kisiasa. kama serikali inataka kumpiku wafanye haraka kutangaza kuyanyang'anya mashangingi yote na kuyapiga mnada kama alivyofanya Kagame. Viongozi waanze kutumia magari binafsi
 


Hitimisho.
  1. Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
  2. Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya "Shangingi" alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.
Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na ;………………………Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.21 Juni 2011.

Imenipendezea. Hii ya kutenganisha fomu ya mahudhurio ni very trick kwa Spika. Kitakachotokea hatatenganisha. Then, what next? Hawatasaini. Then, tuone kama watafukuzwa ubunge. BTW aabunge wengine wa Chadema nao watarejesha mashangingi yao au ni Mbowe tuu?
 
Anatafuta uraisi 2015 kwa kila njia! Ameona Zitto kamzidi kete kwa kukataa posho! Anata na yeye aonekane bora

Zitto akikataa posho, Mbowe akikataa shangingi vyote sawa kwani tunachotaka ni unafuu wa mtanzania na sio kuelemewa mzigo wa kodi kuwalipia wakubwa wachache. Na nimesahau wote ni Chadema. Mengineyo jaza mwenyewe.
 
hana lolote anatafuta cheap popularity ili agombee urais 2015
Hana lolote nani na cheap popularity ipi au upo ndotoni? Lakini sishangai magamba wameshindwa kabisa kusoma alama za nyakati kama enzi za mfalme Belshaza wa Babel alipoona kiganja cha mkono kikiandika ukutani na Daniel kumpa tafsiri bado hakuelewa matokeo yake wana historia mnajua..
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbuka brazamen). Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analotumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka waliomuuzia. Sijui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.
 
Mh.Mwenyekiti nashukuru kunipatia nafsi ya kwanza kutoa machache juu ya hatua hii.

Kwanza hongera wewe mwenyewe kwa kuwa mfano ili wenzako wafuate maana kweli kuongoza si maneno tu bali ni pamoja na kuonyesha njia,ni matendo.

pili hongera wabunge wetu wa CDM kwa kazi mnayoifanya,ni ngumu lakini binafsi naona mnaimudu vilivyo,kwa hili naamini nyote spirit ni ileile moja,fateni njia ya ukombozi

tatu nakipongeza chama changu cha CDM kwa hitimisho lenye kila dalili ya ushindi,kwa hili tayari ni rekodi na naamini sasa ndege yetu iko anga ya juu kabisa baada ya kutake off,hizi ndo bakora nzuri kwa CCM na naamini kabisa 2015 is for us

YES WE CAN......CDM forever & backward never!!
 
Du...!Bravo!
Nchini Burundi huu ndiyo utaratibu uliotumika!
Ilianza kama mzaha, lakini baadaye kweli kabisa viongozi wote waandamizi serikalini walilazimika kurudisha mashangingi, chini ya usimamizi wa Kamanda Kagame!
****** uko wapi?...wanaume washakuanzishia kutafuna, meza sasa!
Mkuu hapo pekundu navyojua mimi Kagame ni Raisi wa Rwanda sio Burundi.
 
Anatafuta uraisi 2015 kwa kila njia! Ameona Zitto kamzidi kete kwa kukataa posho! Anata na yeye aonekane bora

Kwani Prime Minister wa UK, Cameron, alipataje u prime minister? Hivi hivi. Kiutani utani, watu wakachukulia kama mzaha vile mara ghafla.
 
Safii sana,

Kuongoza ni kutoa mfano hata ikibidi kufa na tai shingoni. Ipo siku mawe yatawasikia na watawala watageuka manyani!!

Aluta continua!!

Gen DC

Kuna baadhi ya watanzania wana nia njema sana na nchi yetu! Shida Magamba wao ni matumbo tu hawana kingine, kuna waziri Mwandamizi mmoja husafiri na mkewe kwa gharama za serikali. Hawa watu hawaangalii kama kuna watoto wanazaliwa mazingira magumu hakuna hata huduma za msingi kwa wakunga. Madarasa ya shule za msingi ni aibu hakuna hata dawati karne hii. Sekondary za kata ni aibu zaidi. Kila sehemu ni hovyo hovyo magamba wana taka waendelee kutufanya sisi tuwe masikini zaidi na zaidi.

Ipo siku miti itatusikiliza.
 
Mbowe bwana anaponda mashangingi wakati kachukuwa milioni 90 kwa ajili ya gari, kachakuwa tena mkopo wa milioni 200 benki mdhamini wake ni ofisi ya katibu mkuu wa bunge, acha usanii bwana
 
soma tamko lililotolewa muda huu bungeni.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:KUHUSU BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2011/2012:
Utangulizi.Mnamo tarehe 21/06/2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 .Pamoja na Bajeti ya Serikali kukubali na kuzingatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani CHADEMA kama vile ;a) Kupunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta ya petrol na dizeli.b) Kupunguza kiwango cha faini za makosa ya barabarani kutoka shilingi 300,000/50,000 hadi kufikia ukomo wa shilingi 30,000.c) Kufuta leseni za biashara kwenye Majiji,Halimashauri za Wilaya na Vijiji.d) Kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni yanayotafuta mafuta na gesi Nchini.e) Kuongeza pesa kwenye bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa kodi ya skills development levy 2/3 inapelekwa kwenye bodi kwa ajili ya Mikopo. Katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani wa CHADEMA tuliamua kupiga kura za HAPANA kwenye mapendekezo hayo ya Serikali kutokana na sababu mbalimbali na haswa hizi zifuatazo;
1. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuondoa posho za vikao (sitting allowances) kwenye mfumo wa malipo ndani ya serikali.2. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa magari yote aina ya Mashangingi yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.3. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.4. Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu .5. Serikali imekataa Kufuta/kuondoa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ). 6. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa tunapunguza gharama za safari na haswa kuhakikisha kuwa ni viongozi wakuu na wenzi wao tuu ndio waruhusiwe kusafiri kwa kutumia daraja la kwanza (first class) ambao ni ;· Rais· Makamu wa Rais· Waziri Mkuu· Spika· Jaji MkuuMawaziri wasafiri kwa kutumia daraja la pili (bussines class) na viongozi wengine wote wa umma na watumishi wa umma wakiwemo wabunge wasafiri kwa kutumia daraja la kawaida (economy class) .Pia misafara ya viongozi wakuu ipunguzwe ili kupunguza gharama za kuhudumia misafara hiyo pindi wanaposafiri nje ya Nchi. Hitimisho.
  1. Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
  2. Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya Shangingi alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.
Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na ;Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.21 Juni 2011.
Uongozi ni kuonyesha njia!Safi sana kwa kutembea katika maneno yako!
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbu brazamen).

Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analoumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka walimuuzia. Sojui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.

Uharo huu!
 
hana lolote anatafuta cheap popularity ili agombee urais 2015

Kama cheap popularity itapunguza matumizi yasiyo ya lazima then let it be. Siangalii sana tendo alilofanya bali outcome ya hicho kitendo. Kwakweli tupende tusipende huu ni uzalendo. Tusiwakatishe watu tamaa yakufanya mazuri kwaku-argue eti wanatafuta popularity. Let us assume your right. Sasa kwani wakitafuta popularity at this way does it cost you? At the end of the day we(the people) end up gaining. Let us not complain on everything even when it cost us nothing! Let us focus on what is important i.e. control spending.
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbu brazamen).

Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analoumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka walimuuzia. Sojui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.
kweli wewe Kichaa, mpaka leo unashangaa habari ya kukopa, pumbav*****, unafikiri kwa makali***
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom