Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpaka Kieleweke, Jun 21, 2011.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  soma tamko lililotolewa muda huu bungeni.


  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  KUHUSU BAJETI YA SERIKALI YA MWAKA 2011/2012


  Utangulizi
  Mnamo tarehe 21/06/2011 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2011/2012.

  Pamoja na Bajeti ya Serikali kukubali na kuzingatia baadhi ya hoja zilizotolewa na wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani CHADEMA kama vile ;
  a) Kupunguza kodi na tozo mbalimbali kwenye mafuta ya petrol na dizeli.

  b) Kupunguza kiwango cha faini za makosa ya barabarani kutoka shilingi 300,000/50,000 hadi kufikia ukomo wa shilingi 30,000.

  c) Kufuta leseni za biashara kwenye Majiji,Halimashauri za Wilaya na Vijiji.

  d) Kufuta misamaha ya kodi kwenye makampuni yanayotafuta mafuta na gesi Nchini.
  e) Kuongeza pesa kwenye bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa kodi ya skills development levy 2/3 inapelekwa kwenye bodi kwa ajili ya Mikopo.

  Katika kupitisha bajeti hiyo wabunge wa Kambi ya Upinzani na hususani wa CHADEMA tuliamua kupiga kura za HAPANA kwenye mapendekezo hayo ya Serikali kutokana na sababu mbalimbali na haswa hizi zifuatazo;
  1. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuondoa posho za vikao (sitting allowances) kwenye mfumo wa malipo ndani ya serikali.

  2. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa magari yote aina ya "Mashangingi" yanayotumiwa na viongozi na watumishi wa umma yauzwe kwa mnada ndani ya miezi sita na viongozi hao wakopeshwe magari kwa ajili ya kufanya majukumu yao mbalimbali.

  3. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kufuta/kupunguza misamaha mikubwa ya kodi ambayo Makampuni ya Madini yanapata ili kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

  4. Serikali imekataa kuingiza pensheni kwa ajili ya wazee wote nchini ya shilingi 20,000 kila mwezi ili kuweza kuwapunguzia ukali wa maisha wazee wetu .

  5. Serikali imekataa Kufuta/kuondoa misamaha ya kodi kwa kipindi cha miaka 10 kwenye maeneo maalum ya uwekezaji (EPZ).

  6. Serikali haikukubaliana na hoja yetu ya kuhakikisha kuwa tunapunguza gharama za safari na haswa kuhakikisha kuwa ni viongozi wakuu na wenzi wao tuu ndio waruhusiwe kusafiri kwa kutumia daraja la kwanza (first class) ambao ni ;

  • Rais
  • Makamu wa Rais
  • Waziri Mkuu
  • Spika
  • Jaji Mkuu
  Mawaziri wasafiri kwa kutumia daraja la pili (bussines class) na viongozi wengine wote wa umma na watumishi wa umma wakiwemo wabunge wasafiri kwa kutumia daraja la kawaida (economy class).

  Pia misafara ya viongozi wakuu ipunguzwe ili kupunguza gharama za kuhudumia misafara hiyo pindi wanaposafiri nje ya Nchi.

  Hitimisho.

  1. Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
  2. Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya "Shangingi" alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.
  Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

  Imetolewa na ;
  ………………………
  Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),

  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni

  21 Juni 2011
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Safii sana,

  Kuongoza ni kutoa mfano hata ikibidi kufa na tai shingoni. Ipo siku mawe yatawasikia na watawala watageuka manyani!!

  Aluta continua!!
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Safi sana Chadema 2015 CCM wanaumia kwani hawajui kusoma nyakati.
   
 4. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hana lolote anatafuta cheap popularity ili agombee urais 2015
   
 5. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  safi sana kamanda Mbowe, aluta continua.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  GOD BLESS yoU
   
 7. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Mbowe, wewe ni mfano wa kuigwa kwa nchi yetu! Umefika wakati wa Serikali kuwajali wananchi wake!
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  CRAP Crap
   
 9. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Safi sana mbowe,umeongoza kwa mfano
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Hongera Mbowe kuonyesha kwa vitendo
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Du...!Bravo!
  Nchini Burundi huu ndiyo utaratibu uliotumika!
  Ilianza kama mzaha, lakini baadaye kweli kabisa viongozi wote waandamizi serikalini walilazimika kurudisha mashangingi, chini ya usimamizi wa Kamanda Kagame!
  ****** uko wapi?...wanaume washakuanzishia kutafuna, meza sasa!
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Si unyamaze kama huna la kusema
  Popularity anayo tayari hana shida ya kuitafuta
   
 13. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  hapa wamemshika mtu pabaya....wananchi mpooooooo? mnataka nini tena?
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  wanatenda wanayosema, wanaishi kulingana na hali halisi ya maisha , hawana tamaa, hawataki kuwa wapiga porojo kama yule Mbabu wa Sumbawanga, anaejiita mtoto wa mkulima, wako kuwatetea wananchi, na kuwahudumia kwa kadri ya uwezo wao woote.
   
 15. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Yangu macho mwaka huu, sijui atafuata nani na atakataa kitu gani. Viva CHADEMA
   
 16. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  safi sana ubarikiwe
   
 17. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Excellent! CCM mpo?
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,471
  Likes Received: 19,862
  Trophy Points: 280
  yuko malesyia huko
   
 19. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wewe ulitaka afanye nini ili aoneshe kuwa anawajali wananchi?
   
 20. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Anatafuta uraisi 2015 kwa kila njia! Ameona Zitto kamzidi kete kwa kukataa posho! Anata na yeye aonekane bora
   
Loading...