Mbowe arejesha Shangingi la Kiongozi wa Upinzani Bungeni

Imenipendezea. Hii ya kutenganisha fomu ya mahudhurio ni very trick kwa Spika. Kitakachotokea hatatenganisha. Then, what next? Hawatasaini. Then, tuone kama watafukuzwa ubunge. BTW aabunge wengine wa Chadema nao watarejesha mashangingi yao au ni Mbowe tuu?
Kwanini warejeshe mashangingi yao? Hujui la Mbowe lilikuwa mali ya serikali kama kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani? Pia hujui wabunge yale mashangingi ni mali yao? Ukielewa hayo utapata majibu ya maswali yanayokusumbua na pia utaelewa ni mashangingi yapi cdm wanapendekeza yapigwe mnada
 
"Hitimisho.
  1. Tumeamua kumwandikia katibu wa Bunge barua ili aweze kutenganisha fomu kwa ajili ya mahudhurio na kwa ajili ya posho na wabunge wa CHADEMA hawatasaini fomu za posho.
  2. Kuhusu magari, kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB) Mhe. Freeman Mbowe ameamua kurejesha gari yake aina ya "Shangingi" alilopewa na Bunge ili liwe la kwanza kupigwa mnada.
Tunawataka wabunge wengine waunge mkono hoja hizi kwa masilahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Imetolewa na ;………………………Mhe. Freeman A. Mbowe (Mb),Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni
21 Juni 2011"


Mi nataka kujua hilo "Shangingi" la KUB litapigwa mnada wapi na lini? Na ili kuweka uwazi, lazima lipigwe mnada wa hadhara. Isije kuwa ni kiini macho tu...




 
Kama kushindana huko kuna wasaidia watanzania kuondokana na matumizi mabaya ya fedha za umma, na waendelee tu tena ni safi sanaa, wewe rejao kalaghabaho !
 
Mbowe we ni shujaa! Jaman lile sha'ngingi lililoandikwa KUB unalirudishwa kweli? Jaman,nlilitaman juzi pale askari monument,yan full tinted alaf plate no.KUB. Inahitaji uzarendo wa hali ya juu!
 
Du...!Bravo!Nchini Burundi huu ndiyo utaratibu uliotumika!Ilianza kama mzaha, lakini baadaye kweli kabisa viongozi wote waandamizi serikalini walilazimika kurudisha mashangingi, chini ya usimamizi wa Kamanda Kagame!****** uko wapi?...wanaume washakuanzishia kutafuna, meza sasa!
kijana kagame ni rais wa rwanda
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbuka brazamen). Huyu brazame ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analotumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka waliomuuzia. Sijui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.

Join Date : 9th May 2011
Posts : 1,402
Thanks 285
Thanked 121 Times in 105 Posts
Rep Power : 23

Hapo kwenye red na muda uliojiunga inaonekana ulikuwepo zamani lakini ukaamua kujivua gamba.
 
Ni bao la nguvu la kiuchumi lakini zaidi la kisiasa. kama serikali inataka kumpiku wafanye haraka kutangaza kuyanyang'anya mashangingi yote na kuyapiga mnada kama alivyofanya Kagame. Viongozi waanze kutumia magari binafsi
Kweli kipindi hiki jamaa aka magamba wamekamatwa pabaya na bado kuna maeneo mengine mengi tu ya kuwakamata, sasa ngoja mtasikia Mkama, Nape nk wakija na hoja dhaifu ku-crash hii ya CDM
 
Du...!Bravo!
Nchini Burundi huu ndiyo utaratibu uliotumika!
Ilianza kama mzaha, lakini baadaye kweli kabisa viongozi wote waandamizi serikalini walilazimika kurudisha mashangingi, chini ya usimamizi wa Kamanda Kagame!
****** uko wapi?...wanaume washakuanzishia kutafuna, meza sasa!

Mkuu hiyo ni Rwanda!
 
CHADEMA...
Mnaanza kuonyesha namna viongozi wa Afrika wanavyotakiwa kuishi. Hongereni sana sana! God bless you all!!
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbuka brazamen). Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analotumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka waliomuuzia. Sijui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.

Nadhani hapa hoja ni kwamba amerejesha au hajarejesha? na ujipime na moyo wa kimaskini uliokuwa nao wewe je ata kama ingekuwa bajaj ungethubutu kurudisha?
Hapa ndipo ninapoona angalau vibusara vya Nape aliesema si kila hoja inayotoka upande wa upinzani basi ya kupingwa tu, huo ni ujuha a.k.a msukule.
 
Wewe kama ulikuwepo utakumbuka na kama hukuwepo kuna watu waliokuwepo toka hii Forum ilipokuwa Jambo kabla ya Jamii, wao watakumbusha. Au Brazameni anaweza kufufka akamwaga vitu hapa. Unanchekeshaa!

Uharo huu hey give us a break!
 
hongera mbowe huo ndiyo uongozi kwa vitendo
Inasikitisha viongozi kuishi kama peponi kwa kutumia kodi zetu huku wakihubiri tz ni maskini wakati umaskini huo hauwagusi mpk wastaafu .
inasikitisha zaidi wanatumia magari kwa shughuli binafsi siku za wkend na usiku stk unaikuta salon bar club usiku hii inatia hasira kwa wote wenye kujali na wanaojua kufuatilia matumizi ya kodi yetu . Posho , magari na kufanya kazi chini ya kiwango ni kansa kwa taifa
 
avatar25709_2.gif

hili ikirudishwa nalinunaaaaaa kwa mkopo
 
Du...!Bravo!
Nchini Burundi huu ndiyo utaratibu uliotumika!
Ilianza kama mzaha, lakini baadaye kweli kabisa viongozi wote waandamizi serikalini walilazimika kurudisha mashangingi, chini ya usimamizi wa Kamanda Kagame!
****** uko wapi?...wanaume washakuanzishia kutafuna, meza sasa!
Kwani Kagame ni raisi wa Burundi tangu lini?
 
vivaa KAMANDA WA ANGA...chadema tunaonyesha njia kwa vitendo..wananchi mnataka nini? Kuanzia sasa tuwazomee magamba wakitumia ovyo raslimali za nchi yetu..
 
Safii sana,

Kuongoza ni kutoa mfano hata ikibidi kufa na tai shingoni. Ipo siku mawe yatawasikia na watawala watageuka manyani!!

Aluta continua!!

Sahihisho dogo tu "Kuongoza ni kuonyesha njia hata ikibidi kufa na tai shingoni. Ipo siku mawe yatawasikia na watawala watageuka manyani!!"
 
Kwanza angerudisha fedha alizokopa NSSF zilizomfanya anunulie Vogue (namkumbuka brazamen). Huyu brazamen ni katika wana JF wa zamani na kuna siku aliweka nyuzi humu JF iliyoonesha kuwa jigari analotumia Mbowe ni la wizi huko Uingereza, akataja mpaka waliomuuzia. Sijui brazamen yuko wapi siku hizi? Atupe ma data ya uhakika.
Hivi nyie mapashkuna wengine mna ID's NGAPI NGAPI?
Kumbukumbu zinaonyesha umejiunga juzi 9 May 2011, halafu hapohapo unaongelea habari za Brazameni wa zamani!...
Unaidhalilisha hiyo buibui uliyovaa!
 
Back
Top Bottom