Mbowe apata mpinzani uenyekiti CHADEMA, ni Kansa Mbarouk

Mbowe apata mpinzani uenyekiti CHADEMA, ni Kansa Mbarouk

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Tabora Kansa Mbarouk amejiuzulu nafasi zake zote ndani ya CHADEMA na kutangaza kuwa sasa anaenda kuchukua fomu ya kugombea Uenyekiti wa Taifa.... Hatua hiyo ya kushtukiza imemtia kiwewe mh Mbowe pamoja na kundi lake ambao hivi sasa wanahaha kumchafua kansa... wanatumia mitandao ya kijamii, nafasi zao za uongozi ndani ya chama na marafiki zao mbalimbali lakini mbaruk kwa jinsi anavyokubalika atashinda...

Twende na Mbaruk

mkuu tarifa zake tulishazipata
 
Kama alishindwa kuongoza Tabora Chadema iungwe mkono ataweza kuongoza Chadema iungwe mkono kitaifa?
 
Duh!cdm shikamoni, Duh!mara hii tayari mmeshamuundia zengwe!Yan kila anaetaka kumpinga Mbowe lazima aundiwe zengwe.Nyie mwisho wenu utakuwa m'baya sana na Dhambi ya udini,Ukabila na Ukanda lazima iwatafune

Mmechelewa sana kuanzisha hii thread yenu. Leo tena mtagombezwa na mabwana zenu CCM kama walivyowagombeza mlivyozembea kwenye mkakati ule wa madiwani wa Shinyanga ambao mlilenga wakae CCM kwa muda...
 
Ruttashobolwa, unasemaje kuhusu coincidence iliyokwisha zungumzwa juu ya huyu jamaa, pale inapokuja kutokea bila hat ya chembe ndogo ya mabadililko? Mtu mzima, ningekuwa mimi ningeyeyuka kwa haya. Lakini pia ningeogopa kukanushana na intellingencia ya CHADEMA kwa sababu inaumbua. Soma hapa uburudike kidogo.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/714187-kuelekea-uchaguzi-mkuu-chadema-mkakati-wa-adui-ni-huu-hapa.html

Mkuu kweli huyu ni msaliti na waraka alio andaa soon waandishi wa habari wataitwa na utaoneshwa live.
Huyu amepata wapi ujasiri wa kumpinga mtu aliyechukuliwa fomu na wazee?
 
Msome Makene utagundua kuwa ni kosa la jinai kwa mwanachadema kuchukua fomu ya kugombea uenyekiti na huyu ameshaitwa msaliti na katumwa na bila shaka tunasubiri press conference kuoneshwa mkakati wake.......

Mbowe hatakiwi kupingwa kwa namna yoyote ile.. Huyu Mbaruku wameshamuita msaliti ametumwa na ACT
 
Ruttashobolwa, unasemaje kuhusu coincidence iliyokwisha zungumzwa juu ya huyu jamaa, pale inapokuja kutokea bila hat ya chembe ndogo ya mabadililko? Mtu mzima, ningekuwa mimi ningeyeyuka kwa haya. Lakini pia ningeogopa kukanushana na intellingencia ya CHADEMA kwa sababu inaumbua. Soma hapa uburudike kidogo.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/714187-kuelekea-uchaguzi-mkuu-chadema-mkakati-wa-adui-ni-huu-hapa.html

Huo ni uongo uliotungwa na chadema kwa sababu amegusa maslahi ya wenye chadema yao
 
Zito alipotaka kugombea uenyekiti aliitwa msaliti, mbaruku anataka kugombea uenyekiti kashaitwa msaliti.. hiyo ndio chadema,
 
Muulize huyo Mwenyekiti wako jana alienda Nzega na gari ya Mwigamba kama nani na juzi Igunga alikuwa na gari ya Mwigamba walilala hoteli moja , ni Mwenyekiti wa Chadema huyo ama ACT ? Muulize kikao chake na viongozi wa Bukene kilikua na malengo gani?

Mkuu sasa kama ushahidi mnao kwanini msishughulikie ndani ya chama apate adhabu kuliko kuripoti JF? Tumaini makene kama afisa habari wa chama ana mamlaka gani kumsema kiongozi mwenzie nje kama ni mamluki pasipo kuwa offically approved kwa vikao vya chama? Hamuoni kuwa hili swala linakipaka chama matope?
 

Mmechelewa sana kuanzisha hii thread yenu. Leo tena mtagombezwa na mabwana zenu CCM kama walivyowagombeza mlivyozembea kwenye mkakati ule wa madiwani wa Shinyanga ambao mlilenga wakae CCM kwa muda wakielekea Alliance with CCM Tanzania.


kwa hiyo Makenee na wewe Machadema ni mabwana zakoeeeeee?!
 
Mkuu kweli huyu ni msaliti na waraka alio andaa soon waandishi wa habari wataitwa na utaoneshwa live.
Huyu amepata wapi ujasiri wa kumpinga mtu aliyechukuliwa fomu na wazee?

Mkuu hawa akina Mbowe na Slaa wanawachezea waumini wao cheusi chekundu!
 
Twende taratibu Laki si pesa. Uongo upi unaotungwa na kusemwa kabla haujatokea halafu ndipo utokee? Mbona hiyo makala ilisemwa kabla hata huyo mlengwa hajatangaza nia na imetokea kama tetesi zilivyosikika? Ninaomba unchanganue kwanza hii ko insindensi.


Huo ni uongo uliotungwa na chadema kwa sababu amegusa maslahi ya wenye chadema yao
 
MSIBA MZITO CHADEMA
TAARIFA ZILIZO TUFIKIA HIVI PUNDE NI KWAMBA MWENYEKITI WA CHADEMA WA MKOA WA TABORA NDUGU KANSAS MBAROUK AMEJIUZUlU LEO, SABABU ZA KUJIUZULU KWAKE NI KUTOKANA NA UONGOZI WA JUU KUTO KUSHUGHULIKIA MIGOGORO ILIYO NDANI YA CHAMA NA KUKIACHA CHAMA NA WANACHAMA WAKE KUFARAKANA.
SAMBAMBA NA MWENYEKITI HUYO PIA KADA MAARUFU KUTOKA MKOANI TABORA BWANA M. KWITIME NAE PIA AMEJIUZULU KWA SABABU HIZO HIZO.
 
Mbarouk amewekewa zengwe baada ya kutaka kugombea uenyekiti wa chadema taifa.. alitaka kugusa maslahi ya wenye chama.
 
Chadema kama wewe siyo mchaga halafu ukawa tishio huwezi kudumu hata kidogo lazima watakuondoa tu waachieni chama chao wenyewe.
 
Back
Top Bottom