wambagusta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2014
- 2,840
- 2,329
Nilijuwa toka 2005 tanzania Kulikuwa akuna upinzani wakweli. Na mwaka huu ukweli umetimia
Mhe.Mbowe Jiandae Kuwajibika Katika Hili Kwa Watanzania.
Mpasuko Unaoendelea Sasa Katika UKAWA Ni Matunda Ya Maamuzi Yako Mabovu Yaliyokosa Ridhaa Ya Pamoja Ya Viongozi Wenzako.Maamuzi Yako Yaliyokua Na Lengo La Kuwaburuza Viongozi Wenzio Kifikra Na Kimaamuzi.Na Maamuzi Yako Yaliyofishwa Na Tamaa Yako Ya Uroho Wa Madaraka Na Kukubali Kununuliwa.
Kitendo Cha Kumkaribisha Fisadi Papa No.1 Mhe.Lowassa Ndani Ya UKAWA Na Kupewa Nafasi Ya Kuteuliwa Kama Mgombea Uraisi Bila Ya Maridhiano Thabiti Kutoka Kwa Viongozi Wenzio.Kumekufanya Wewe Uwe Fisadi Papa No.11(Haukuwepo Kwenye Listi Ya Awali Ila Sasa Upo).Na Watanzania Wanatakiwa Kukuogopa Kama Ukoma.Kwa Kuweka Maslahi Yako Mbele Kuliko Maslahi Ya Taifa.
Kama Bado Unaamini Kua Kuondoka Kwa Dr.Slaa Na Prof.Lipumba Ndani Ya UKAWA Hakuna Madhara Yeyote kwa UKAWA.Basi Ukae Ukijua Kua Uko Ni Kujidanganya Na Kujilisha Upepo.
Malipo Ya Usaliti Huu Kwa Viongozi Wenzio
Yatakua Ni Kuanguka Kwako Mwezi October Na Kuporomoka Kwako Kisiasa.Na Ujiandae Kwa Aibu Kubwa
Najaribu kutazama jinsi kenyata na ruto walivyoandamwa na kashfa kibao za matukio ya mauaji ya mwaka 2007
baadae namuangalia kenyata na kashfa yake na baba yake kwa kuwanyang'anya wakenya wengi ardhi huko kikuyu highland lakini sasa ndiye raisi
pamoja na kuwa na kashfa kibao namuona kama rais pekee aliyeipeleka puta kenya katika maendeleo zaidi ya marais wote waliotangulia huku uchumi wao ukikua maradufu
kwa mantiki ndogo kama hiyo niko radhi lowasa aingie madarakani hata kama ni fisadi ili
1) kuondoa utawala wa ccm madarakani na kisiwepo chama kinachoamini kuwa kitatawala milele kama ccm wanavyodhani
2) kubadilisha uongozi wa nchi utaifanya hata ukawa itakayoingia madarakani itende mambo kwa umakini huku ikijua baada ya miaka mitano inaweza ondolewa madarakani
nb: Nataka asiwepo mtawala wa milele kama ccm na Lizaibon wanavyoamini kuwa wao hawawezi kuanguka na hilo litafanya kila atakayepewa madaraka kufanya mambo kwa uhakika huku akijua akilegalega miaka mitano inayofata ataondolewa
kura yangu ni ukawa
- bY kalichumbage
kalichumbage
Mpelekeni mahakamani
At least wewe umesema ninayoyafikiria.
Mbowe kauza Chama, hafai kabisa huyu jamaa.
Kura yako ni moja tu mpe unayeona anafaa. Mengine achana nayo.Povu la nini?
Mkuu Slaa si mlikuwa mnamuita padri mzinifu? Vipi leo mnamsifia!!??Sasa wewe una macho ya ubongo kweli wewe? Huyo mwenyekiti wenu na genge lake la walafi unawapa Title gani kama siyo hiyo ya kuganga njaa kali kwa kuhujumu mafanikio ya Upinzani? Kamanda Slaa alikikuta chama hicho cha kifamilia kikiwa hakina mbele wala nyuma. Amejitolea maisha yake kukijenga chama hicho akiamini waliokianzisha ni waadilifu. Sasa huyu mnamwita mganga njaa? Siyo bure mmelogwa.
Lakini na wewe Mzee wetu slaa kwa nini hukufanya background /profile check ya watu walioanzisha CHADEMA? Ujue ukisikia mtu aliwahi kuto aminiwa na Nyerere basi akianzisha jambo usilikurupukie. Usaliti hurithishwa vizazi na vizazi
Mkuu umenena, hii mijambazi ya ccm lazima iondokeAngalau ndoto yangu ya muda mrefu inakaribia kutimia. Sikuwahi kuwa muumini wa vyama kabisa zaidi ya kulazimika.
Ni hivi: kuiondoa CCM madaraka ndiyo objective namba moja, kwa kuwa CCM hawana uzoefu wa kuwa wapinzani wataharibu zaidi huko kwenye upinzani na hivi walishazoea kuendesha mambo yao kwa nguvu na support kubwa ya dola kwao kifo hakitakwepeka.
Wapinzani watakapoingia Ikulu badala ya kuanza kupiga kazi ili kutekeleza majukumu kama walivyojinasibu, wataanza kupingana wao kwa wao na kugombea nyadhifa hivyo kuzorotesha mambo hivyo wataishia kuparanganyika tu. Kufika hapo tutakua tumeshaua utawala , ukuu na utukufu wa vyama na kurudisha mamlaka ya wananchi kutafuta na kujitengenezea viongozi nje ya vyama. Hapo ndipo Tanzania itakua imekombolewa kwa uhakika toka kwenye mikono ya vigenge vya wachachache vijiitavyo vyama.
Hii tabia ya kutuambia mengine itajulikana baadae hatutaki kuisikia kabisa nyie nyumbu.kila kitu kiwekwe hadharani hapa lowassa na genge lake wakishaingia ikulu hatutakuwa na uwezo wa kubadilisha lolote ataitafuna nchi anavyotaka. Hongera kwa uchambuzi makini.
Mbowe ametuuza kwa vipande vya shekeli kwa tamaa ya madaraka. Hafai kabisa kiongozi wa namna hii Kama kuitafuta ikulu kaitafuta kwa fedha akiingia si watamaliza kila kitu hawa.
Wilbroad na Ibrahim ni Mashujaa wa Taifa hili. UKAWA laana ya kuwasliti watanzania imeshaanza kuwatafuna na itawamaliza.