Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Km huyu jamaa wanaemwita DJ ambae IQ yake inatiliwa shaka kakiuza chama kwa EL, Akipewa nchi ataiuza pia. Tuweni makini na viongozi kama hawa.

Nawaza hivi huyu jk na safari za nje haijauza nchi kweli? Mikataba 17 ya china nchi aijauzwa tuu bado?mboye auze nchi gani?
 
Imebainika kuwa katika harakati za kumpokea Lowassa ndani ya Chadema,ni Dk. Slaa pekee ambaye amekana Rushwa kutokana na uadilifu wake wa mafunzo ya dini alopata tangu mtoto. Ikumbukwe kuwa Lowass pia alishindwa k umrubuni Mangula akiwa anawania urais kupitia ccm,hali ya ugumu wa Mangula kukataa Rushwa el amekumbana nayo pia alipokuja kuhamia huku kwa Slaa. Ungozi wa pesa hautotufikisha mahali.
 
Imebainika kuwa katika harakati za kumpokea Lowassa ndani ya Chadema,ni Dk. Slaa pekee ambaye amekana Rushwa kutokana na uadilifu wake wa mafunzo ya dini alopata tangu mtoto. Ikumbukwe kuwa Lowass pia alishindwa k umrubuni Mangula akiwa anawania urais kupitia ccm,hali ya ugumu wa Mangula kukataa Rushwa el amekumbana nayo pia alipokuja kuhamia huku kwa Slaa. Ungozi wa pesa hautotufikisha mahali.


Historia inaonesha kuwa vipindi fulani katika mstakhabali wa nchi unalazimisha kupima nini ni janga zaidi ya jingine. Marehemu Samora Machel na Frelimo walikubali kutia saini Mkataba wa Nkomati wa ushirikiano na Makaburu kama mkakati wa kujinusuru na kutoa nafasi kukabiri janga kubwa kuliko zote wakati huo la kuondolewa serikali ya Frelimo na Renamo ikisaidiwa na Makaburu. Wakomunisti wa Afrika ya Kusini waliingia ubia na ANC ya mabwanyenye weusi ili kutokomeza kwanza ukaburu na mapambano na ubepari yaje baadaye. Katika Vita Kuu ya Dunia ya Pili wakomunisti walishirikiana na mabwenyenye wa mrengo wa kulia na kati kutokomeza janga kubwa zaidi wakati huo la ufashisti, yaani ubepari wa mrengo wa wa kulia kupitiliza. Hivyo hivyo mapambano ya kuleta uhuru wa Tanganyika yalivyo unganisha nguvu za mabwenyenye wazungu na waasia pamoja na zile za wakulima na wafanyakazi wa rangi zote kwa azimio lile la mkutano mkuu wa Tanu wa 1958 pale Tabora. Hivyo hivyo Mandela na ANC waliingia "urafiki wa mashaka" na De Clerk kiongozi wa Makaburu ili kuondolewa ukaburu kuwe kwa amani ya "kula matapishi" ya kuwalaani huko nyuma kuwa ni wabaya wa Mwaafrika!!

Mabadiliko ya haraka haraka yanayoendelea hapa Tanzania yenye lengo la kuondoa CCM madarakani kama chama dola kinachodumaza na kudhoofisha ushindani wa kisiasa miongoni mwa mabwenyenye wa tabaka tawala Tanzania ni mabadiliko yatakayoleta neema kwa Watanzania wote. Ile tu CCM kudhoofishwa na kujiunga UKAWA kwa Lowassa ni kuvuja kwa pakacha ambayo ni nafuu ya mchukuzi.....Nikuondoa kizingiti kikuu cha kushamiri kwa demokrasia pana na maendeleo endelevu Tanzania ambacho ni kuhodhiwa na ukiritimba wa chama dola cha CCM kinachojinadi kama chama cha mrengo wa kushoto wakati ni chama cha mrengo wa kulia kama vyama vyote vya siasa Tanzania kwa sasa.

Kumeguka kwa CCM-Mambo Leo kama taasisi ya kakundi ka wana mtandao ulioingiza serikali ya sasa ya Tanzania madarakani mwaka 2005, ni faraja kwa wote wenye kuitakia mema nchi hii na ni kiashiria cha kukomaa kwa vuguvugu la ukombozi wa pili wa Tanzania utakaochukua sura ya demokrasia zaidi ili kuwa na maendeleo endelevu zaidi yapatikane kupitia kupatikana nafasi chanya zaidi ya kupitishwa kwa Katiba Mpya kama ilivyopendekezwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Kwa mara ya kwanza vyama vy siasa vya upinzani kiuhalisia (tofauti na vile ambavyo vimebebwa na watawala wa sasa kwa lengo la kuua upinzani wa kisiasa kijanja kijanja kama ACT- Wazalendo), sasa vimeunganishwa na kupigania Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Jaji Warioba ( UKAWA) badala ya kuunganishwa na kutaka kuondoa CCM madarakani pekee.

Ghafla mwanasiasa mwenye nguvu nyingi ndani ya chama cha kifisadi cha CCM, mwanasiasa ambaye umaaarufu wake umetokana na kuongoza mtandao uliouweka utawala wa sasa wa CCM madarakani, Ndugu Edward Lowassa, amekasirishwa na kukatwa jina lake na aliodhani ni rafiki zake ndani ya CCM na kuamua kusema basi na lolote liwe kwa kujiunga na vuguvugu la kupigania katiba mpya!! Naye sasa kang'amua kuwa Katiba ya sasa na ile Pendekezwa ni za ovyo maana haziruhusu kuwepo mgombea huru bila mizengwe. Hasira za Lowassa zimezaa tunda zuri la kug'amua kuwa Watanzania wanahitaji mabadiliko kupitia Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba. Hasira hizi za mkizi ni furaha ya kunguru na ni busara kwa viongozi wa CHADEMA na UKAWA kwa ujumla kutoongopa "kula matapishi yao" kwa kumkaribisha Ndugu Lowassa...huyu huyu waliomwita fisadi... kujiunga na UKAWA na kugombea urais. Nafasi ya kihistoria imejitokeza ya kukiondoa CCM madarakani kwa amani!!

Sishangai wasaliti wa vuguvugu la kukiondoa CCM madarakani wanatushauri sisi Watanzania wenye shauku ya kuutumia upenyo huu wa mpasuko ndani ya CCM kukiondoa CCM madaraka!!! Eti tuombe radhi kwa" kula matapishi yetu" wote tulio wahi kumwita Lowassa fisadi! Wao wanataka tuendelee kuvumilia kutawaliwa na CCM labda kwa miaka mitano au zaidi hivi mpaka chama kipya cha watakatifu kiitwacho ACT-Wazalendo kitakapo kuwa tayari kututawala badala ya CCM!! Sishangai kusikia ushauri huu kutoka kwa wasaliti hawa ambao kazi yao hata huko nyuma imekuwa ni kuudhoofisha upinzani dhidi ya CCM na kukisaidia CCM kiendeleee kuwa madarakani!! Hawa jamaa ni wasomi sana na ni wajanja sana, ilo lazima kulikiri!!!

Sitashanga kama haya ninayoyasema yatapigwa madongo na wasaliti hawa!! Historia itakapoandikwa baada ya UKAWA kupata viti vingi zaidi Bunge lijalo au hata kuutwaa urais na kupata Katiba Mpya iliyobebwa ndani ya Rasimu ya Pili ya Tume ya Rais iliyoongozwa na Jaji Warioba, itawapa hukumu yao stahiki, wajanja na welevu hawa! Bila shaka wanaoomba UKAWA ishindwe kupata viti vingi Bunge lijalo na iukose urais na hivyo tuendelee kutawaliwa na CCM na wao wapate viti vya kutosha kuwa viongozi wakuu wa eti upinzani muruwa wenye maadili ya Azimio la Arusha Tanzania!! Ni haki yao ya binadamu kuendelea na matumaini haya kama na sisi tulivyo na haki ya kuendelea na matumani yetu ya uwezakano wa ushindi mnono chini ya UKAWA dhidi ya ukiritimba wa chama kimoja chama dola cha CCM!

By Mwl. Lwaitama
 
Aisee bado watanzania tununuliwe sasa. Lowassa katumia bil.10 kumnunua MBOWE kuingia CHADEMA, sasa kuna taarifa kuwa DUNI HAJI amenunuliwa kwa mil.550 ili akubali kujiunga na CHADEMA ili ateuliwe kuwa mgombea mwenza wa LOWASSA. Hiyo haitoshi inasemeka mgogoro unaoendelea kule CUF unatokana na CHADEMA kumnunua Maalim Seif Sharif Hamad kwa ahadi ya kugaramia Kampeni za Uchaguzi kule Zanzibar, pesa zitakazotolewa na LOWASSA ili kukubali mgombea mwenza atoke CUF.

 
Wakati mwingne tuwe wakweli hizo 10 bilion ukiambiwa uto ushahidi utaweza au umeamua kuchafua hali ya hewa kwa faida ya chama chako.
 
Ccm wako kazini kudanganya watanzania kama walivyozoea miaka ya ujama,watanzania sasa ni wasomi bana labda hapo Lumumba
 
Lowasa anatumia fedha za kifisadi alizotuibia wananchi. Ndo maana hazionei huruma
 
Hivi watanzania wamelogwa na nani? You take a lot of your time to write foolish articles!!!!

Wewe umechanganikiwa kweli ni dhahiri kwamba elimu yako ni finyu mno ndo maana unaishi kwa hisia ambazo zinaweza kuharibu nchi.
 
Thread unayoleta tayari Mhafidhina mwenzio Lizaboni ameshaiandika lete propaganda mpya mkuu
 
Bora kujua bilioni kumi za Lowasa kuliko kutojua wanazotumia CCM
 
Hii chorus ya billion kumi imeshachuja vijana wa lumumba embu jipangeni na nepi wenu tafadhali at least mje na ingine, hii haiuziki tena.
 
Aisee bado watanzania tununuliwe sasa. Lowassa katumia bil.10 kumnunua MBOWE kuingia CHADEMA, sasa kuna taarifa kuwa DUNI HAJI amenunuliwa kwa mil.550 ili akubali kujiunga na CHADEMA ili ateuliwe kuwa mgombea mwenza wa LOWASSA. Hiyo haitoshi inasemeka mgogoro unaoendelea kule CUF unatokana na CHADEMA kumnunua Maalim Seif Sharif Hamad kwa ahadi ya kugaramia Kampeni za Uchaguzi kule Zanzibar, pesa zitakazotolewa na LOWASSA ili kukubali mgombea mwenza atoke CUF.


Only fools will understand you not 2015
 
Lowasa anatumia fedha za kifisadi alizotuibia wananchi. Ndo maana hazionei huruma
hahahaha!! kama 'mama wa mboga', 'joka la makengeza' na wengine wafanyavyo. yani hawa watu hawana huruma kabisa!
 
Back
Top Bottom