Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Si mlikuwa mnawatangazia kuwa ni fisadi sasa mmemsafisha kwa sabuni gani ? Si mnaona mnavyotuchanganya Watanzania
 
Siasa ni dynamic zinaenda zinabadilika.Adui wa jana ni rafiki wa leo na pengine rafiki wa jana leo ni adui.CUF leo ni rafiiki wa chadema ingawa alikuwa adui wa chadema huko nyuma.Vivyo hivyo kwa NCCR na chadema.Hivyo ndivyo siasa zinavyoenda kutegemea mabadiliko ya kifikra ya wakati husika.

Dr.Slaa alijiunga chadema baada ya kukatwa kwenye kura za maoni ccm mwaka 1995.Leo hii ni mhimili wa chadema hasa unapozungumzia nafasi ya uraisi.Kwa hiyo staili aliyojia Dr.Slaa ya kukatwa jina kinyume na taratibu ndiyo hiyo iliyomkuta Lowassa (kama akija chadema).Litakuwa sio jambo jipya.....

Lengo namba moja la chama chochote cha siasa ni kushika dola.Bila kushika dola(ama sehemu yake) chama kitaendelea kuwa cha mapendekezo tu kwa chama kinachotawala.Ni hiari ya serikali ya chama hicho kukubali au kuyakataa mapendekezo hayo.Tumeona mapendekezo mengi sana yamekataliwa kwenye bunge la jamhuri na lile la katiba.Ni kwakuwa tu watoa mapendekezo sio chama dola wala sehemu yake.Hapa unaona umuhimu wa kutocheza na nafasi ambayo inaweza kukifanya chama ama kiwe chama dola au sehemu yake.

Tatizo la nchi yetu ni mfumo wa uendeshaji wa nchi kuanzua serikali za mitaa mpaka serikali kuu.Na huu mfumo uliotokana na ccm hauwezi kubadilika bila kwanza kuitoa ccm yenyewe.

Kama Lowassa atahamia chadema pamoja na kampani yake hasa ya wabunge na madiwani basi tunaweza kama sio kuitoa ccm madarakani basi kubadilisha sehemu ya mfumo huu anbao labda ungeweza kuchukua miaka kadhaa kubadilika.

Kuna uwezrkano wa kushinda uraisi na hivyo kuendesha serikali.Sioni uwezekano huu mapema bila huo mpasuko wa ccm.........

Kama bado ccm watashinda uraisi basi kuna uwezekano wa kupata wabunge wengi wa uoinzani kuliko wa ccm na hivyo kutoa waziri mkuu wa kwanza wa upinzani.Hili likitokea kubadilisha mfumi ni rahisi kwani sheria zinapotungiwa wapinzani ni wengi kukiko ccm.........

Mambo mangapi ya msingi yanakwama bungeni kwa sababu ya uchache wa wapinzani?Kama kugombea kwa Lowassa kutaweza kuleta balance bungeni hatuoni kuwa ni mabadiliko yanaweza kufanyika kwenye sera na sheria?

Spika amekuwa akiendesha bunge kwa kadiri maelekezo ya serikali ya ccm yanavomuelekeza.Kwa kuwa na balance bungeni au pengine wapinzani wakawa wengi kuna uwezekano wa kuchagua spika kutoka upinzani na hatimaye kureview mavitu yote yaliyopitishwapitishwa na bunge hili la ndiyoo?

Kama upinzani utakuwa na nguvu kwenye bunge na/au kwenye serikali kuna uwezekani sasa wa kuandika katiba ya wananchi ambayo mfumo uliopo uliikwamisha kwa maslahi yake.

Sasa kama kweli unapenda mabadiliko kwa nini unakataa kinachoweza kuyaleta hayo mabadiliki uyatakayo?Kama unataka kuwa static na kupata cheo cha mtoa mapendekezo mazuri wa kudumu na yasifanyiwe kazi basi sawa.........endelea na msimamo.

Hivi Lowassa anahamia Chadema kwa vile anakubaliana na Sera na Ilani ya chama au ana sababu zingine? Chama ambacho ilani zake za uchaguzi wa 2005 na 2010 zinasema kwamba kikishika dola kitawachukulia hatua mafisadi wote walionewa haya na serikali ya CCM?

Pili, Anayeenda ikulu ni Ukawa au ni Chadema au ni Lowassa na genge lake wakina Karamagi na Rostam? Wakiingia Ikulu mtawezaje kuwadhibiti hawa wenye uwezo wa kuhonga mabilioni ya pesa bila kupepesa macho?
 
Km huyu jamaa wanaemwita DJ ambae IQ yake inatiliwa shaka kakiuza chama kwa EL, Akipewa nchi ataiuza pia. Tuweni makini na viongozi kama hawa.
 
Tena kakiuza kwa bilioni 10 tu kwa fisadi Lowasa
 
Politics is game of dynamics, uletewe striker kama Ronaldo na wafuasi million nyuma yake halafu uwakatae umekuwa kichaa!???
 
Mtaruka ruka sana mwaka!
Wanaouza TWIGA hamuwaoni!
Wanaouza meno ya TEMBO siyo wauzaji? Tulien
 
Acha ujinga kupambana na adui unatumia silaha yoyote itakayokuletea ushindi,by the way ni lini CCM ikaitakia CDM mema? ...na bado mtanyooka
 
Politics is game of dynamics, uletewe striker kama Ronaldo na wafuasi million nyuma yake halafu uwakatae umekuwa kichaa!???

Ukishinda mechi unachukua kombe mchezo umeisha. Ukishinda uchaguzi unaanza kazi muhimu ya kuongoza nchi.

Ni makosa makubwa kufananisha ushindi wa mechi na uchaguzi. We must think beyond uchaguzi.
 
Ukishinda mechi unachukua kombe mchezo umeisha. Ukishinda uchaguzi unaanza kazi muhimu ya kuongoza nchi.

Ni makosa makubwa kufananisha ushindi wa mechi na uchaguzi. We must think beyond uchaguzi.

Lowasa ni picha kazi itapigwa na wapiganaji kina mbowe, mbatia, lipumba nk..... Lowasa is a game changer
 
Inasikitisha sana pale mtu unapoamua kutoa taarifa za uongo na zilizojaa chuki bila kuwa na uhakika wa unachokiwasilisha kwa umma.PCCB wanafanya kazi 24 hrs kwa hiyo km unao ushahidi juu ya MBOWE na group lake kupewa hela na Lowassa, ebu fanya jambo la kishujaa ambalo litasababisha history ikukumbuke kizazi na kizazi.
 
Last edited by a moderator:
Atauza nini sasa wakati Tanzania ilishauzwa kitambo...
 
Mtaruka ruka sana mwaka!
Wanaouza TWIGA hamuwaoni!
Wanaouza meno ya TEMBO siyo wauzaji? Tulien

Tuhuma kama hizi zilitokea na zilizoeleka lkn CCM haikuuzwa. Leo hii DJ kapuuza maoni ya mtu alikipigania chama kwa miaka 20(Slaa) hadi kapata ulemavu wa mkono, mkewe alipigwa hadi mimba ikatoka unakumbatia MTU MCHAFU!!! Ama kweli watanzania hatujielewi.
 
Tuhuma kama hizi zilitokea na zilizoeleka lkn CCM haikuuzwa. Leo hii DJ kapuuza maoni ya mtu alikipigania chama kwa miaka 20(Slaa) hadi kapata ulemavu wa mkono, mkewe alipigwa hadi mimba ikatoka unakumbatia MTU MCHAFU!!! Ama kweli watanzania hatujielewi.

You call yourself hamjauzwa na ccm!
Kweli mmekunywa maji ya bendera!
Leo hii ndo mnajifanya mnauchungu na dokta siyo? ? Mbaffffffff kabisa

Ukawa wanajielewa sanaaaaa!
Tulien hivo hiyo sindano haichomoki had oktober! ! !
 
Back
Top Bottom