Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

ACT .....Ayatoollah aliomba kiongozi wa Arusha aandae mkutano ........
 
Jibu rahisi mtawaambia nyie ni wachumia tumbo, waroho wa madaraka na mko tayari hata kuuza nchi ili mshike dola

Nadhani ni afadhali kuliko wanaonadi sera ya kufunga goli la mkono.
Hao wanauroho na damu za watanzania. Mashetani wekundu...hatari sana!
 
Huo ndo msemo tangu enzi, na hii inatokana na historia ambayo mababu zetu wameshuhudia kutoka enzi na enzi.
kwamba kimya kingi kinamshindo mkuu na mshindo wake hauvumiliki,.
kuongea sana wakati mwingine kunaonyesha udhaifu wako.
EDWARD NGOYAI LOWASSA ukimya wake takribani miaka saba ndio uliyemuweka akawa juu zaid ya chama, kwani baada ya kumhujumu kwa muda mrefu kuwa ni fisadi, gamba lakini hatimae wananchi wamejiuliza kwanini ni LOWASSA tuu, kwanin mtu huyu atupiuwe lawama zote hizi, ndipo wananchi walipochoka kusikia sauti hizo nakuamua kuungana nae kwenye safari ya matumaini.
sio kwasababu wananchi waliamua kumuunga mkono kwamba LOWASSA sio fisadi au sio msafi, bali ni ukimya wa LOWASSA ambao uliwaeka wananchi njia panda nakuona kuwa LOWASSA kasingiziwa. pamoja na kuwa jina lake limefanyiwa mizengwe na kukatwa na kamati ya maadili na kushindwa kufika Nec lakini bado LOWASSA kaendelea kuwa kimya mabapo bado kunawachanganya wananchi. Hii inamaana kwamba bado LOWASSA anawaaminisha wananchi kuwa alionewa na ndivyo wengi wanaamini mpaka sasa na hii imechangiwa na UKIMYA WA LOWASSA.
LOWASSA anazivuruga akili za watu, wananchi wanataka wasikie sauti yake, wajue anawaza nn, atoe tamko angalau hata salaam, wamuone hata kanisani, wanataka kujua anataka kufanya maamuzi gani, WANANCHI WANASUBIRI KWA HAMU KUBWAA..
Hata KIKWETE anahamu ya kujua LOWASSA anawaza nini, anataka nini, LOWASSA anamvuruga sana KIKWETE na timu yake, kiukweli LOWASSA ANAIVURUGA NCHI NZIMA.

Shost

Umenena vema sana...hata mm mwenyewe ukimya wa Lowassa unaniweka njia panda...angesema tu japo hata kidogo...
 
Sijawahi kuona kauli za kijinga katika maisha yangu kama hii. Eti tutampokea fulani...anayetajwa kama gwiji la ufisadi, kuwa mgombea wetu halafu tukishaingia madarakani ndio tutapambana na ufisadi. Hili ni jambo la jabu!
 
If you wage revolution without planning automatically that revolution will fail. Tumeona Libya na Iraq na maeneo mengine
 
Sijawahi kuona kauli za kijinga katika maisha yangu kama hii. Eti tutampokea fulani...anayetajwa kama gwiji la ufisadi, kuwa mgombea wetu halafu tukishaingia madarakani ndio tutapambana na ufisadi. Hili ni jambo la jabu!
Tuta takiwa kiking'oa kwanza chama kilicho laaniwa,ndipo tuanze kazi kujitengeneza.Naona ni upuuzi kufikiri tusiking'oe eti kwa sababu jitihada hizo zita changiwa na fisadi
 
Bado nchi ina mazuzu mengi na hilo litawaghalim wengi na hawa wanao jitambua kuonekana wote mazuzu
 
Sijawahi kuona kauli za kijinga katika maisha yangu kama hii. Eti tutampokea fulani...anayetajwa kama gwiji la ufisadi, kuwa mgombea wetu halafu tukishaingia madarakani ndio tutapambana na ufisadi. Hili ni jambo la jabu!
Mtu akiwa na kiu ya madaraka anaweza kutumia njia yoyote kufika pale ili kutimiza malengo yake binafsi. Jamani baadhi ya watu hawataki uongozi wa nchi kwa sababu wana uchungu saaaana na nchi na wana wa nchi bali wana uchungu saana na matumbo yao na matumbo ya ndugu zao.
 
Tuta takiwa kiking'oa kwanza chama kilicho laaniwa,ndipo tuanze kazi kujitengeneza.Naona ni upuuzi kufikiri tusiking'oe eti kwa sababu jitihada hizo zita changiwa na fisadi[/QUOTE

KUTOA FISADI IKULU NI NGUMU WATANZANIA TUPAMBANE NA MAFISADI WOTE HATA KAMA WAPO UKAWA, MSEMO WA MCHAWI MPE MWANAO AKULELE UMEPITWA NA WAKATI, UKIMKBIDHI MWANAO MCHAWI ATAMTAFUNA
 
Utashughulikiaje ufisadi bila kuing'ioa CCM kwanza?
What is your best approach?
 
Siasa ni kama mchezo wa mpira unapofanya kosa ndipo unapompa mwenzako nafasi ya kukupiga bao kwa kutumia kosa lilelile ulilolifanya.

CCM walifanya kosa kubwa sana ambalo mwisho wake utaishia kuwagharama kwa kushindwa kumchukulia Lowassa hatua za kisheria mapema pamoja na kwamba walikuwa wanaelezwa kuwa ni fisadi na hata wao walikuwa wanamjua kuwa ni fisadi.

Kwa kitendo cha CCM cha kumuacha Lowassa bila kumpeleka kwenye vyombo vya sheria ili vikathibitishe ufisadi wake moja kwa moja kinamvua Lowassa kwenye vitendo vya ufisadi awe alifanya au hakufanya.

Kwa hiyo hata kama wapinzani watamchukua Lowassa na kumtumia kuiondoa CCM madarakani watakuwa wamemchukua mtu safi asiye na kosa lolote kwa kuwa Lowassa hajawahi kupelekwa Mahakamani chombo pekee ambacho kinamamlaka ya kumtia mtu hatiani baada ya tuhuma alizokuwa ana tuhumiwa nazo kuthibitishwa kwanza, zaidi ya hapo Lowassa ataendelea kuwa mtu safi pamoja na kuwa na tuhuma za ufisadi.
 
Hii slogan ni mpya kwangu!kuing'oa ccm kwanza ufisadi baadae!nakumbuka list ya mwembe yanga huu ni mzaha!
 
Hamen mtu mamluk hatumuhitaj chadema fisad n baba liz yona na mramba
 
Siasa ni kama mchezo wa mpira unapofanya kosa ndipo unapompa mwenzako nafasi ya kukupiga bao kwa kutumia kosa lilelile ulilolifanya.

CCM walifanya kosa kubwa sana ambalo mwisho wake utaishia kuwagharama kwa kushindwa kumchukulia Lowassa hatua za kisheria mapema pamoja na kwamba walikuwa wanaelezwa kuwa ni fisadi na hata wao walikuwa wanamjua kuwa ni fisadi.

Kwa kitendo cha CCM cha kumuacha Lowassa bila kumpeleka kwenye vyombo vya sheria ili vikathibitishe ufisadi wake moja kwa moja kinamvua Lowassa kwenye vitendo vya ufisadi awe alifanya au hakufanya.

Kwa hiyo hata kama wapinzani watamchukua Lowassa na kumtumia kuiondoa CCM madarakani watakuwa wamemchukua mtu safi asiye na kosa lolote kwa kuwa Lowassa hajawahi kupelekwa Mahakamani chombo pekee ambacho kinamamlaka ya kumtia mtu hatiani baada ya tuhuma alizokuwa ana tuhumiwa nazo kuthibitishwa kwanza, zaidi ya hapo Lowassa ataendelea kuwa mtu safi pamoja na kuwa na tuhuma za ufisadi.

Kwa maono yako kwa vile serikali ya CCM haijawahi kumpeleka mtu yeyote kwenye vyombo vya sheria akathibitishwa kwamba yeye ni fisadi basi hamna mafisadi Tanzania. Hivyo Dr Slaa na orodha yake ya mafisadi walikuwa wanatupiga changa la macho?
 
Mtu akiwa na kiu ya madaraka anaweza kutumia njia yoyote kufika pale ili kutimiza malengo yake binafsi. Jamani baadhi ya watu hawataki uongozi wa nchi kwa sababu wana uchungu saaaana na nchi na wana wa nchi bali wana uchungu saana na matumbo yao na matumbo ya ndugu zao.
Hata yule aliyeuza nyumba za serikali alikuwa na uchu wa madaraka
 
Back
Top Bottom