Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Jamani huyu mtu LOWASA ataongea lini tupumzike na hili jina tuanze mambo mengine......kila kona ni Lowasa, kila nyumba ni Lowasa, ukifika bar ni Lowasa, ukiingia ofcn ni Lowasa,nikienda kucheza draft kote ni Lowasa, nikiongea na mke wangu dakika tatu badae kamtaja Lowasa......duh!
Umesema ukweli uliyonigusa muda siyo mrefu mke wangu kaniuliza muda siyo mrefu lowassa hajaongea tu!!?
Kuna watu wengi wanahuzuni sana na alichofanyiwa lowassa zaidi ata ya lowassa na wengi wa watu hawa wanamsikiaga lowassa tu na kumuona kwenye tv ila nafsi nyingi zinasononeka sana na kitendo hicho kitaangamiza ccm!!
 
Lowasa akiwa binadamu kama sisi lazima roho yake iumie kwa yaliyomsibu. Ila, kwa sababu ya busara zake za kutaka kufanya maamuzi magumu ndiyo maana ameamua kukaa kimya akisubiri muda mwafaka wa kulipiza.
Magamba yakae mkao wa kukatwa.FONT]
 
Nikiwa Mwanachama Mtiifu Wa Chama Cha Democrasia Na Maendeleo Chadema, Kuna Tetes Zimeenea Kwenye Vyombo Vya Habari Kuhusu Ujio Wa Edward Lowasa Katika Chadema Hii Habari Siipingi Ila Nataka Kutoa Msimamo Wangu Kidogo, Sikubaliani Na Lowasa Kugombea Urais Kwa Kupitia Ukawa, Kwa Sababu Lowasa Ni Fisadi Kama Mafisadi Wengine, Kauli Yake Aliyomwambia Rais Ni Kitu Gani Nilikifanya Wewe Haukujua? Hapo Tu Ina Maanisha Lowasa Alifanya Yeye Ila Mkubwa Wake Alijua, Je? Tutawaambiaje Wananchi? Lowasa Aje Chadema Ila Asigombee Urais, Ninamwamini Sana Dr Slaa
 
CHADEMA wala hatuhitaji mwanachama kama wewe usiyejua kutumia fursa kuondoa mfumo CCM ambao ni kandamizi kwa wananchi. Kwa taarifa yako ni kwamba Lowassa anakuja na atagombea. Ushauri kwako na wenzako wote wa CCM mlioingiwa na hofu ya EDO kuja CHADEMA, muwe tayari kwa mafuriko.
 
Hizi tetesi pia mi nimezipata pata mahali,hebu ngoja tuone.
 
wasubiri ma laundry men waje wakuambie usafi wake huo uchafu unaujua wewe na yule mzee
 
Hizi taarifa zinaweza zisiwe za kweli, ila ukimya wa kuzikanusha unatia shaka.

Kama Lowassa atasimamishwa kweli na UKAWA nitaamini kwamba sijui chochote kwenye siasa.
 
Ondoka Lowassa lazima aje lengo ni kuitoa CCM na tuko tayari kushirikianahata na shetani ili mradi tu mfumo huu wa CCM utoke. Kajiunge na team Membe mkasubiri mbeleko 2020.
 
CHADEMA wala hatuhitaji mwanachama kama wewe usiyejua kutumia fursa kuondoa mfumo CCM ambao ni kandamizi kwa wananchi. Kwa taarifa yako ni kwamba Lowassa anakuja na atagombea. Ushauri kwako na wenzako wote wa CCM mlioingiwa na hofu ya EDO kuja CHADEMA, muwe tayari kwa mafuriko.

Kwanza Kabisa Unaonyesha Jinsi Ulivyomkulupukaji Na Hamaki Ya Hali Ya Juu, Wewe Kama Ni Chadema Basi Umekuja Na Upepo Wa Kukatwa Kwa Lowasa, Mimi Niseme Tu Sihitaji Kujibizana Kwa Kashfa Ila Mimi Ni Chadema Nilijiuna Na Chama Mwaka 205 Na Sina Mpango Wa Kuhama Chama, Ila Nazungumza Ukweli Uliokwenye Moyo Wangu, Lowasa Amekuja Na Safari Ya Matumaini, Lakini Chadema Tumezunguka Nchi Nzima Tukiponda Safari Hiyo Ya Matumaini Tukiwaambia Wananchi Tunataka Safari Ya Uhakika, Sasa Lowasa Akija Na Hiyo Safali Ya Matumain Chadema, Na Amewatangazia Wananchi Kwamba Safar Ya Matumaini Iko Palepale Swali Langu Je? Tutawaambiaje Wananchi?
 
Jibu rahisi mtawaambia nyie ni wachumia tumbo, waroho wa madaraka na mko tayari hata kuuza nchi ili mshike dola
 
CHADEMA wala hatuhitaji mwanachama kama wewe usiyejua kutumia fursa kuondoa mfumo CCM ambao ni kandamizi kwa wananchi. Kwa taarifa yako ni kwamba Lowassa anakuja na atagombea. Ushauri kwako na wenzako wote wa CCM mlioingiwa na hofu ya EDO kuja CHADEMA, muwe tayari kwa mafuriko.

Kabisa mkuu huyu jamaa atakuwa ndorobo tu. Siasa haijui kabisa. CCM wenyewe wanamuogopa EL kama ni fisadi unaushahidi? Tuoneshe. Mi ninachojua watz wote mafisadi tunatofautiana kiwango tu. Msinidanganye bila wizi hakuna mtz angenunua gari wala kujenga nyumba. So mumwache EL yeye alikuwa sehemu poa zaidi akachota zaidi acheni wivu wa kijinga. Hatuwezi kuwa matajiri wote.
 
Siasa ni dynamic zinaenda zinabadilika.Adui wa jana ni rafiki wa leo na pengine rafiki wa jana leo ni adui.CUF leo ni rafiiki wa chadema ingawa alikuwa adui wa chadema huko nyuma.Vivyo hivyo kwa NCCR na chadema.Hivyo ndivyo siasa zinavyoenda kutegemea mabadiliko ya kifikra ya wakati husika.

Dr.Slaa alijiunga chadema baada ya kukatwa kwenye kura za maoni ccm mwaka 1995.Leo hii ni mhimili wa chadema hasa unapozungumzia nafasi ya uraisi.Kwa hiyo staili aliyojia Dr.Slaa ya kukatwa jina kinyume na taratibu ndiyo hiyo iliyomkuta Lowassa (kama akija chadema).Litakuwa sio jambo jipya.....

Lengo namba moja la chama chochote cha siasa ni kushika dola.Bila kushika dola(ama sehemu yake) chama kitaendelea kuwa cha mapendekezo tu kwa chama kinachotawala.Ni hiari ya serikali ya chama hicho kukubali au kuyakataa mapendekezo hayo.Tumeona mapendekezo mengi sana yamekataliwa kwenye bunge la jamhuri na lile la katiba.Ni kwakuwa tu watoa mapendekezo sio chama dola wala sehemu yake.Hapa unaona umuhimu wa kutocheza na nafasi ambayo inaweza kukifanya chama ama kiwe chama dola au sehemu yake.

Tatizo la nchi yetu ni mfumo wa uendeshaji wa nchi kuanzua serikali za mitaa mpaka serikali kuu.Na huu mfumo uliotokana na ccm hauwezi kubadilika bila kwanza kuitoa ccm yenyewe.

Kama Lowassa atahamia chadema pamoja na kampani yake hasa ya wabunge na madiwani basi tunaweza kama sio kuitoa ccm madarakani basi kubadilisha sehemu ya mfumo huu anbao labda ungeweza kuchukua miaka kadhaa kubadilika.

Kuna uwezrkano wa kushinda uraisi na hivyo kuendesha serikali.Sioni uwezekano huu mapema bila huo mpasuko wa ccm.........

Kama bado ccm watashinda uraisi basi kuna uwezekano wa kupata wabunge wengi wa uoinzani kuliko wa ccm na hivyo kutoa waziri mkuu wa kwanza wa upinzani.Hili likitokea kubadilisha mfumi ni rahisi kwani sheria zinapotungiwa wapinzani ni wengi kukiko ccm.........

Mambo mangapi ya msingi yanakwama bungeni kwa sababu ya uchache wa wapinzani?Kama kugombea kwa Lowassa kutaweza kuleta balance bungeni hatuoni kuwa ni mabadiliko yanaweza kufanyika kwenye sera na sheria?

Spika amekuwa akiendesha bunge kwa kadiri maelekezo ya serikali ya ccm yanavomuelekeza.Kwa kuwa na balance bungeni au pengine wapinzani wakawa wengi kuna uwezekano wa kuchagua spika kutoka upinzani na hatimaye kureview mavitu yote yaliyopitishwapitishwa na bunge hili la ndiyoo?

Kama upinzani utakuwa na nguvu kwenye bunge na/au kwenye serikali kuna uwezekani sasa wa kuandika katiba ya wananchi ambayo mfumo uliopo uliikwamisha kwa maslahi yake.

Sasa kama kweli unapenda mabadiliko kwa nini unakataa kinachoweza kuyaleta hayo mabadiliki uyatakayo?Kama unataka kuwa static na kupata cheo cha mtoa mapendekezo mazuri wa kudumu na yasifanyiwe kazi basi sawa.........endelea na msimamo.
 
Hata kanu ya kenya ilipo muita mwai kibaki fisadi.baada ya kusikia kua anakwenda upinzani waliweweseka hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom