Tetty ni wewe kweli mwanasiasa wa CDM damu leo unajipambanua na wafanyabiashara za kisiasa?
Basi UWEZO wa kufikiri wa Watanzania UMEKOMAA kwani ni CCM imejipambanua kuwaondoa Mafisadi kitaalam na kubakia chama cha wakulima na wafanyakazi (wafanyabiashara waende UKAWA)
Ukwaju,signature yangu imekuingia vyema akilini.Haitakaa hata siku moja CCM iachane na wafanya biashara,wezi,wala rushwa,ufisadi ,madwa ya kulevya,majangili nk nk,mpaka pale wanachama wake watakapoamua kwa dhati sasa basi!!!!!!!!!!!!
Mimi ni upinzani toka umeanza,na wala silipingi wala sikatai,na wala sitaki kuhama chama ,chama changu ni CDM hata wakiniambiatoka,daima nitabaki kuwa CDM na nitawaambia ukweli daima sitawaficha,pakuwapa hongera nitawapa,kwa kuwapinga nitawapinga,kwa kuwaambia ukweli nitawaambia,nina tabia moja simuogopi mtu,ninamuogopa
MUNGU tu,si dharau MTU NINAWAHESHIMU watu wote bila kujali itikadi zao,ukanda watokako wala dini waaminizo.
CCM ilikuwa enzi za JKN sasa hivi kimebaki kuwa chama cha kitajiri au cha matajiri,rejea maelekezo waliyopewa wajumbe wao wa mitaa kwamba aslani asiende mtu kuchukua form ya kugombea uongozi bila kuwa na uwezo,tena uwezo kifedha.
Leo nataka kugombe udiwani,sijui kesho yangu nitakula nini,zamani form ilikuwa Tzs.20,000 leo naambiwa nitoe 1,500,000 ninazipata wapi,hapo bado hamjatuambia kwamba CCM ni ya MATAJIRI na WAFANYA BIASHARA?Hamjatuambia bado bila RUSHWA na UFISADI huwezi kuwa kiongozi CCM?
Haya na ubunge nako,nimedunduliza nimejipatia laki moja naambiwa hiyo haitoshi unatakiwa kuleta milion Tatu,duh,UKWAJU,nashindwa kukuelewa unapo sema CCM imejipambanua kuwaondoa mafisadi kitaalam,sasa sijui utaalamu wa miti shamba au kwa maana ya kisayansi.!
Swali la gitaa!!!!!Unaweza kumwondoa MWENYEKITI wako kwenye nafasi aliyonayo leo?Huyu si aliingia kwa pesa za yule tunayemwita leo FIASDI?Si ndiyo huyu alipita njia ile aliyopita shostiko wake?
Jibu rahisi,URAFIKI na UNDUGU umeingia kwenye sura nyingine ndani ya CCM,kama mzazi hajawahi kuwa kiongozi ndani ya CCM asiote kuwa.
Mmechaguliwa hata Mwenyekiti na KITENGO,aliwahi kusema URAIS WAKE NI WA KWAKE NA FAMILIA yake wengine hamna chenu,leo nikisema sentensi hii ni sawa na kusema UENYEKITI WAKE NI WAKE NA FAMILIA yake wengine siyo wadau wa uenyekiti wake nitakuwa nimekosea?
Ukwaju,hujafa hujaumbika,CCM hamuwezi kuwaondoa mafisadi humo ndani,labda mchome nyumba moto wengine wateketee kwa moto na wengine wapone,na watakao pona ndiyo watakuwa wachache waijenge upya nyumba hiyo ya CCM.
Kwa sasa UKWAJU hamtaweza,hata huyo mlichaguliwa hataweza,wachafu wako wengi zaidi ya wasafi.
Ni ukweli unaouma sana ,siyo kwa mana CCM tu ,bali kwa watanzania wote maana kutoka huko pia tunapata wawakilishi wetu ambao wamehonga kupata IWAKILISHI jiulize watazirudishaje pesa zao?Mimi na wewe tunajua ila hatutaki kuamini namna watakavyozirudisha.
UKWAJU
TANZANIA BILA RUSHWA tunaweza
PLAY YOUR PART
UKWAJU kwa uhakika
TUWE TANZANIA KWANZA VYAMA BAADAYE.Mbunge yeyote toka chama chochote atakayetoa rushwa ya aina yoyote hastahili kuwa muwakishi wetu.Kaka UKWAJU pamoja tunaweza.