Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Ndugu huu ni sawa na usajili kama ilivyojipambanua kwa timu za mpira hata kama mchezaji alikuwa anawafunga sana mkisha msajili iliawapatie ushindi na atafuata taratibu za klabu haunabudi nikumsajili tu.
 
kama chadema itakufa furahini basi kuliko kuweweseka
 
Nimepokea taarifa kwa masikitiko makubwa sana juu ya Mwenyekiti wa CHADEMA, FREEMAN AIKAEL MBOWE kuuza chama kwa shilingi bilioni 10 kwa fisadi Lowasa ambaye kwa mara kadhaa ametajwa kuhusika kwenye kashfa nyingi za ufisadi hapa nchini. Kwa mujibu wa taarifa hizo, Edward Lowasa amempa Freeman Mbowe in personal shilingi Bilioni 10 kama hongo ili aweze kuteuliwa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA.

Hakika hizi ni taarifa mbaya sana kwa wapenda demokrasia nchini na kwamba vita dhidi ya ufisadi sasa inakuwa ngumu. Hii ni kwa sababu hawa wapinzani ambao ndio tuliwategemea kuiamsha serikali dhidi ya mapambano ya rushwa ndo wameingia kwenye mkumbo wa kutoa na kupokea rushwa. Hii ni fedheha kubwa sana kwao na ni aibu kwa siasa za Tanzania. Mbowe kanajisi upinzani na amedhalilisha sana siasa za nchi yetu.

Kwa Lowasa kuhamia upinzani si tatizo. Ila tatizo ninaloliona hapa ni hili la kutoa shilingi bilioni 10 ili tu ateuliwe kuwa mgombea urais. Kama kiongozi wa chama anaweza kununuliwa kwa shilingi bilioni 10, vipi kuhusu rasilimali za nchi yetu? Tutamtofautishaje na wale machifu ambao walikubali kuwekeana mikataba na wakoloni kwa kupewa tu bunduki, vioo na vipande vya nguo huku wao wakitoa vipande vya dhahabu? Hakika inaniuma sana na inasikitisha sana.

Ni dhahiri sasa hatuna upinzani wa kweli nchini bali tuna wachumia tumbo. Freeman Mbiwe pupa na tamaa ya fedha inamfanya asione azma aliyonayo juu ya maelfu ya wafuasi wake ambao walimuona kama ni kiongozi jasiri na mchukia rushwa. Sasa katumbukia kwenye shimo. Nani atamnasua? Tafskari na chukua hatua.


Naona watu speed za kwenda chooni zinaongezeka tu, mdogo mdogo. Kuna TAKUKURU, ipo chini ya serikali, ya CCM, lini mshawahi wakamata au hata kuwahoji kuwa wao ni mafisadi?
Kama mna hakika na hiyo biashara haramu kufanyika, kwa nini vyombo vya dola havijachukua hatua. Hata nyie mnaotoa, kwa nini mnajificha nyuma ya pazia? Na wewe Weston Songoro, tangu lini umekuwa na mapenzi na upinzani? Siyo kwamba mnaona mmezidiwa?
 
Last edited by a moderator:
Ninachokiona ni ule usemi usemao adui muombee njaa, Siamini kama Kuna kipenzi cha chadema ambaye anamhitaji lowasa kuhamia chadema wanachadema wanachotaka ni lowasa awavuruge Ccm ili hstimaye kura Za Ccm zigawanyike na kurahisisha ushindi wa chadema au ukawa ikiwa watasimamisha mgombea mmoja. Nawasilisha.
 
Vipi mbona mnahangaika sana na Lowasa? Yaani Magufuli ameishachuja ghafla hivi, mlikuwa mstari wa mbele kumsifia kila siku alipotoka Dodoma lakini sasa hivi kimyaaa mnamuwaza Lowasa tu mtu ambae hadi sasa yupo kimya hajaongea chochote
 
Kwa hiyo huyo mzee wenu anayelindwa na gwanda asipitiwe na upepo bila Lowassa anaweza kuing'oa madarakani CHICHIEMU?
 
Hivi kweli mtu kama ni fisadi na ameiba pesa za uma mbona hakuna hata siku ambayo amekamatwa na kushitakiwa. Tunaimba fisadi, fisadi, fisadi tu kila wakati. Akamatwe basi akashitakiwe. Wanaodanganyika ni wananchi tu, ambao hawafuatilii vyombo vya habari. Mwananchi mwenye akili timamu anajua uozo wa serikali ilioko madarakani.
 
Mimi sioni ubaya wa Lowasa kuamia Chadema ...
Kama atafata taratibu za Chama basi nakukaribisha Tena kwa mikono miwili..
Tatizo sio Lowasa tatizo ni Ccm..
Hata Kikwete akikubalia na taratibu za chama tunamkaribisha Chadema
 
Mzalendo halisi c mlimsafisha kwa OMO!!
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa mh. Freemam Mbowe amemkaribisha Lowassa kujiunga na CHADEMA hakibagui mtu ili mradi tu afuate kanuni na taratibu za chama.

Source: Tanzania Daima, Mwananchi
 
Lowassa ana interest ya kugombea urais kwa vile inasemekana bado ni kipenzi cha watu wengi.
Atakayekaa na kuzia ndoto hizo ana balaa!!

Lowassa kwake sasa dili ni urais tu.
Natanguliza kuwapa pole ndugu zangu wa UKAWA maana hawana Kamati ya Maadili kama ya kwetu Gambaz!!
 
Lowassa ana interest ya kugombea urais kwa vile inasemekana bado ni kipenzi cha watu wengi.
Atakayekaa na kuzia ndoto hizo ana balaa!!

Lowassa kwake sasa dili ni urais tu.
Natanguliza kuwapa pole ndugu zangu wa UKAWA maana hawana Kamati ya Maadili kama ya kwetu Gambaz!!

Hii nayo ni thread? Kwa nini mnapenda kujaza server? Ujinga huu.
 
Maadili gani Sisiem Wanayo... Kwanza Hakuna Demokrasi Ndani ya CCM: Demokrasi ni Kwa ajiri ya Watu na ni ya Watu Wenyewe. Sasa

Kama KITENGO Kinapoka Maamuzi ya wengi halafu Unahita Maadili. Poleni Sana Kwa Kuweka Personal interest rather than Party Interest.

Naamini Kuna Wagombea Wengi tu Hawakufurahiswa na Jins KITENGO Kiliwafanya. Eti Kamati ya Maadili .
 
Hakuna siku ambayo itanifanya niichukie chadema nikiwa miongoni mwa wanachadema wazalendo kama Siku nitakayosikia Kuwa bwana Lowassa ni mwanachama mwandamizi wa chama chetu kinachojipambanua kwa kupinga ufisadi kama chama kitampokea lowassa Mimi lasmi nitaachana na siasa kwa sababu chama kitakuwa kimekiuka itikadi na falsafa yake na hilo ndilo litakuwa kaburi la chadema, tutafakari pamoja swala hili wana jukwaa.
 
Back
Top Bottom